Gari ya Jaji yasababisha ajali baada ya kutanua, vijana wa ujenzi Mwenge-Morocco wagongwa

Utanuaji wa magari ya Serikali sasa yameanza kusababisha maafa.

Leo jioni gari Kilimo Kwanza la Jaji mmoja, pale Mwenge limesababisa ajali na kupelekea daladala lililouwa linamkwepa huyo mkubwa kugonga wajenzi wa barabara Mwenge-Morocco.

Vijana kadhaa wajenzi wamegongwa na kukimbizwa Muhimbili.

Hali zao haijulikani.

Serikali inalifumbia macho tatizo la madereva wake.

Wananchi twafwa!
Mtu kama huyo kwa nini unamkwepa? Kama yeye hajali maisha na aje ajibamize uso kwa uso.
 
Ndo raha ya nchi kuwa na wabunge sare sare maua, acha tuhamishie hii barabara ya Morocco nayo chato, ikiwezekana hata Ubungo exchange tuihamishie chatto
Daaa!! ingekuwa ugali mtamu ni ule wenye mboga saba mezani, basi Mbeya ingefaidika sana.
Lakini sasa Mbeya ina ugali na maharage tu mezani, daaaa!! watoto wameanza kunawiri bwana! huwezi amini!
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya.........!
 
Iliniuma sana, nilikuwa 10m away na yule wa VX V8 aliyetanua sikuona hata akijali, aliondoka. WTF wenye madaraka wanayatumia vibaya hivyo? Hakufa mtu?
Mungu mkubwa!
Hakuna aliyepoteza maisha lakini wafanyakazi wa ujenzi JF tumefuatilia kupitia wa waliokuwepo, kuna waliovunjika miguu na kuna waliopondwa vifua na hata wengine kujeruhiwa mwilini.
Hata abiria kwenye basi kuna walioumia.
 
Kwanini hao hawakukimbizwa Ligalo Hospital ambapo ndo karibu na kupelekwa Muhimbili?? Tufanyie utafiti na hilo pia
 
Aisee hakuna madereva wapuuzi kama hawa madereva wa serikali, nimejionea hayo matatizo hapa Dodoma Dereva wa STK/STL anatanua sehemu yoyote, ana overtake sehemu yoyote hata kwenye blind corner na wana dharau sana wanaona nyinyi wengine kama sio watu ama hawaoni kama sie wengine tuna haki ya kutumia hizo barabara

Shame on you Gvt's drivers.
 
Uzi bila kapicha tu naona kama ni fix tu
IMG-20210114-WA0060.jpg

Huyo daladala alikuwa ana mkwepa J66.
Pocha kwa hisani ya wajenzi wafanyakazi.
Hapo ni Mwenge mataa kuelekea mjini.
Dereva wa daladala ilibidi alikwepe sKilimo Kwanza la mtu mkubwa na kuingia mtaroni.
Wafanyakazi ndio waliojeruhiwa.
 
Utanuaji wa magari ya Serikali sasa yameanza kusababisha maafa.

Leo jioni gari Kilimo Kwanza la Jaji mmoja, pale Mwenge limesababisa ajali na kupelekea daladala lililouwa linamkwepa huyo mkubwa kugonga wajenzi wa barabara Mwenge-Morocco.

Vijana kadhaa wajenzi wamegongwa na kukimbizwa Muhimbili.

Hali zao haijulikani.

Serikali inalifumbia macho tatizo la madereva wake.

Wananchi twafwa!

UPDATE
=======
Gari ya Jaji iliyosababisha ajali ni J66.
Serious allegations against a Judge.
Napata tatizo nikifikiri yafuatayo:

1.Dereva anafanya makosa,Traffic Offence, na Jaji anamuangalia tu!

2. Jaji anafahamu sheria za Traffic Ordnance. Na anajua dereva wake anafanya a criminal act kwa kutanua.

3.Kwa kujua hilo, Jaji ni an accomplice to a criminal act.

4. Sioni sababu kwa nini Jaji asiunganishwe kwenye mashitaja ya ajali.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom