Gari ya Jaji yasababisha ajali baada ya kutanua, vijana wa ujenzi Mwenge-Morocco wagongwa

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
8,206
2,000
Utanuaji wa magari ya Serikali sasa yameanza kusababisha maafa.

Leo jioni gari Kilimo Kwanza la Jaji mmoja, pale Mwenge limesababisa ajali na kupelekea daladala lililouwa linamkwepa huyo mkubwa kugonga wajenzi wa barabara Mwenge-Morocco.

Vijana kadhaa wajenzi wamegongwa na kukimbizwa Muhimbili.

Hali zao haijulikani.

Serikali inalifumbia macho tatizo la madereva wake.

Wananchi twafwa!

UPDATE
=======
Gari ya Jaji iliyosababisha ajali ni J66.
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,626
2,000
Kuanzia mwenge eneo lote hadi lugalo ni eneo la ambalo magari mengi ya serikali, jeshi na viongoz hutanua na kusababisha ajari lakini huwa hawasimami!
Na hakuna wa kuhoji!
Wakigonga huwa hata hawasimami!
Wewe nae! Umeambiwa Mwenge/Moroko wewe unabadili gia na kuwa Mwenge/ Lugalo! Barabara hiyo anaijenga mwanao yule aliyemaliza la saba mwaka jana?
 

M2WAWA2

JF-Expert Member
Aug 15, 2014
488
1,000
HIVI KATIBA INASEMAJE?

VIONGOZI WAO HAWAPASWI KUWEPO NA KUSUBIRIA FOLENI?

KWAMBA WAO WANA HARAKA SANA KURUDI KWENYE FAMILIA ZAO KULIO SISI WENGINE?

EBU YULE MSEMAJI WA KUJITEGEMEA, MWANA HARAKATI HURU, MTETEZI WA RAIS AJE NA HASEME HAPA
 

Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,946
2,000
Nikitafakari yanayomtokea Trump leo hii, madaraka ni koti la kisenge sana mamamae!

Unaota ndoto za mchanaa!!! Marekani kuna taasisi zenye nguvu kama vile Bunge na Mahakama; unategemea Ndugai siku moja kumtia mbaroni JIWE? Huko marekani Pelosi ndivyo alivyomfanyia Trump!!!

Tume ya Warioba ilikuwa inapendekeza kuwa na mihimili inayojitegemea na yenye nguvu na Ndio maana watawala wakaogopa na kuipiga spana!!
 

DreezyD98

Verified Member
Nov 6, 2020
554
1,000
Dah😓. Na kuna ile tabia ya wanajeshi kupita wrong side kisa foleni kuna siku wataua wananchi wasio na hatia.
 

Aladeen04

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
1,938
2,000
Kuna mshenzi mmoja alitukosa juzi na STL ya kodi zetu zebra ya Mwanjelwa pale sina hamu jamaa hawana ustaarabu kabisa sijui huwa wanawaza nini wenzie wamesimama tunaoenda kwa miguu tuvuke kaja na mi speed yake huku katanua dah
 

gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
1,730
2,000
Ndo raha ya nchi kuwa na wabunge sare sare maua, acha tuhamishie hii barabara ya Morocco nayo chato, ikiwezekana hata Ubungo exchange tuihamishie chatto
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom