Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Makampuni ya mafuta nchini yamewaandikia EWURA kulalamika dhidi kile kinachoonekana ni uchakachuaji wa mafuta ya diesel na petrol unaofanywa na kampuni inayoagiza mafuta nchini, Augusta Energy. Uchakachuaji huo, ambao pia unaathiri magari, ni ule wa kuchanganya diesel au petroli na ethanol kwa kiwango cha juu bila hata idhini ya serikali. Mafuta yaliyochanganywa na ethanol kwa kawaida yana bei ndogo zaidi, hivyo kampuni ikiagiza mafuta yaliychanganywa na ethanol na kuyauza kama yasiyo changanywa inapata faida kubwa sana.
Kuchanganya diesel au petrol na ethanol ni kitu cha kawaida bila gari kuathirika kwa kiwango cha 90:10, 10% ikiwa ethanol. Ukichanganya zaidi ya hapo lazima ubadilishe mfumo wa mafuta wa gari.
Rwanda, ambayo inapitisha mafuta yake Tanzania, tayari imeshakataa kupokea consignments za mafuta toka Tanzania kutokana na tatizo hili la uchakachuaji na ethanol. Rwanda huko nyuma ilifanya hivi pia kwa uchakachuaji wa kutumia mafuta ya taa, na hata kuwaweka ndani madereva wa Kitanzania waliobeba mafuta yaliyochakachuliwa.
Kisichoeleweka ni jinsi gani TBS wamekuwa wakiruhusu shehena ya mafuta yaliyochanganywa na ethanol iingie nchini wakati Tanzania haina utaratibu wa kutumia "blended fuel". Zaidi ya hapo, swali la kujiuliza ni kwa nini TBS waliruhusu kuingia nchini mafuta yaliyochanganywa na ethanol kwa kiasi cha juu sana cha kuharibu magari ya watu.
Original source: IPP media
Hao wanaoingiza mafuta ni wahuni wa pale magogoni unategemea nini?
Ela feki wao.
Madawa ya kulevya wao.
Wachakachua mafuta wao.
Mafisadi wao.
Watoroshaji wanyama pori wao.
Wenye hisa kwenye migodi ya dhahabu wao.
Yani ikulu pamekuwa pango la walanguzi.
Corruption is the lubricating oil of our government machinery.
TBS?
Yaani unazungumzia TBS? TBS si ni pambo tu?
Nasikia kuna kampeini inayolenga kuhakikisha kuwa mafuta hayaagizwi kwa pamoja inayoendeshwa na wafanya biashara mbali mbali wa mafuta wakishirikiana, EWURA na pamoja wanasiasa. Hata upandaji wa bei na matatizo yaliyotekea hapo nyuma ilikuwa ni juu ya hii. Hivyo tuwe makini na hili tusije kutumiwa
Ndugu yetu kama hujafanya utafiti afali usiseme kwani, mfumo huh ulianzishwa NA ewura how comes Auhujumu? Pia issue ya kuchakachua Huko nyuma hamkusikia kwa kuwa hii term was introduced by EWURA amabye alia za masks 2006 NA ndoo maana Huko nyuma hukuwa unasikia
Hao wanaoingiza mafuta ni wahuni wa pale magogoni unategemea nini?
Ela feki wao.
Madawa ya kulevya wao.
Wachakachua mafuta wao.
Mafisadi wao.
Watoroshaji wanyama pori wao.
Wenye hisa kwenye migodi ya dhahabu wao.
Yani ikulu pamekuwa pango la walanguzi.
Tanzania Bila Standard
wajameni huu uzi umikaa kiudaku hivi. Dizeli ichanganywe na ethanol! Hilo mbona ni sawa na kuchanganya dizeli na petrol?