Gari la Mpendazoe lakamatwa

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Polisi katika kituo cha Karume jijini Dar es Salaam, imelikamata na kulishikilia kwa muda, msemaji wa Chama Cha Jamii (CCJ), Fred Mpendazoe.
Gari hilo lenye namba T 776 BAE, aina ya Corolla, lilishikiliwa jana kwa takribani saa sita, kwa madai kuwa kibali cha kuendesha kilikuwa kimeisha.
Wakati gari hilo likikamatwa, lilikuwa linaendeshwa na dereva wake, Vitalis Henzi Mpendazoe, anayesadikiwa kuwa mtoto wa Mpendazoe.
Akizungumza na gazeti hili jana nje ya kituo hicho, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema mtoto huyo alikamatwa eneo la Msimbazi Centre, wakati akitokea Kigogo kuelekea Ilala-Boma.
Alisema askari wawili waliokuwa kwenye pikipiki, walilitilia shaka na kuanza kulikagua, ambapo ilibainika bima yake ilikuwa imemalizika muda wa matumizi.

CHANZO: NIPASHE
 
Tatizo nini kwani unataka sheria ipindishwe kwasababu ni mpendazoe?kuweni makini kwa kuleta habari sio kujaza mistari na post tuu
 
Tatizo nini kwani unataka sheria ipindishwe kwasababu ni mpendazoe?kuweni makini kwa kuleta habari sio kujaza mistari na post tuu

Nahisi kama Umekurupuka vile, kwani mleta mada ametoa conclusion yeyote?
 
Kwani tatizo liko wapi ..?ndio maana tumeambiwa limeshikiliwa kituoni kwa masaa hayo no more.
 
Hii ni habari ya kawaida sana, kama halina kibali ni lazima likamatwe!
 
Mbona la mzee wa vijisenti limekuwa likitembea mpaka limeua?
 
Kama lengo ni kumzungumzia Mpendazoe kwamba hafuati sheria za usalama barabarani na kwa nini kwa kupitia CCJ anaona tendwa hatimizi majukumu yake kwa kutoisajili CCJ kwa muda wanaohitaji wao hii ni issue. Ajue kama msajili anapindisha sheria hata yeye anamatatizo pia. Msimlaumu mtioa mada kuna point pia. Siyo lazima gari lake liuwe kama la mzee wa vijisenti
 
Pengine mtoa mada alitaka kuonyesha jinsi watu wanaotaka kuja kuliongoza taifa letu baadaye wasivyokuwa makini na sheria za nchi wanayotaka kuiongoza baadaye. Hata hivyo kwangu naona Mpendazoe siyo issue kwenye siasa za sasa hivi.
 
Back
Top Bottom