Gari la Mbunge Mkono lateketezwa kwa moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la Mbunge Mkono lateketezwa kwa moto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngambo Ngali, Jul 29, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Gari la Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nimrod Mkono, limeteketezwa kwa kuchomwa moto baada ya kudaiwa kuwagonga watu wawili na kusababisha kufa papo hapo.

  Inadaiwa kuwa gari hilo aina ya Nissan Patrol lenye namba T 173 AZW liliwagonga watu hao wakati wakisafiri kwa kutumia pikipiki katika Barabara Kuu ya Musoma- Mwanza.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz, alithibitisha dereva wa pikipiki hiyo, Magori Magori (39) na abiria wake, Wambura Kitongori (40), wakazi wa Nyabange kufa kwa kugongwa na gari hilo juzi katika eneo la Mkiringo.

  Boaz, alisema wakati ajali hiyo ikitokea mbunge huyo hakuwamo kwenye gari hilo na kwamba dereva wake, Petro Andrea (43), alikimbia na kulitekeleza eneo la tukio na kusababisha kuteketezwa kwa moto.

  Alisema gari hilo liliwagonga watu hao na kufa wakati likitokea mjini Musoma kuelekea Busegwe.

  Alisema baada ya ajali hiyo kutokea wananchi wa eneo hilo walifika katika tukio na kulichoma moto gari hilo na kuteketea kabisa.

  Kamanda huyo, alisema polisi mkoani hapa wanaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo na kuwasaka waliochoma gari hilo kwa sababu kitendo hicho ni kosa la jinai.

  "Tunaendelea na uchunguzi wa ajali na wale waliohusika na tukio na watakaokamatwa katika kuhusika na tukio hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwani kuchoma moto gari hata kama limesababisha ajali ni kosa la jinai, " alisisitiza.

  Alitoa wito kwa wakazi wa Mara kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na
  kuliachia Jeshi la Polisi kufanya kazi yake ili hatua stahili za kisheria zzichukuliwe dhidi ya makosa mbalimbali.


  Miili ya marehemu hao ilichukuliwa na ndugu zao na kuzikwa katika Kijiji cha Nyabange.


  CHANZO:
  NIPASHE

  Hilo ndo jeshi letu laolisi, no mention at all dereva aliyeuwa wanamchukulia hatua gani hasira zao zote zinaishia kwenye waliochoma gari.

  Kwa namna hii kweli tutegemee wananchi watakubali kufanya kama ambavyo bwana RPC anasema Ona kwenye red. Maisha ya watu ni secondary gari ya muheshimiwa ni primary.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ipo siku mafisadi watachukuliwa sheria mkononi maana wananchi watakuwa wamechoshwa na utendaji wa vyombo vya kutoa na kusimamia haki
   
 3. k

  kavdeo Member

  #3
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nadhani alimgonga mwanaharakati wa Chadema
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  I feel sorry for the deceased and Hon. Nimrod Mkono
   
Loading...