WABHEJASANA
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 4,225
- 869
Wakuu,
Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita wametoa tamko la kukataa gari linalotumika katika kusambaza Dawa za Binadamu kwenye vituo vya afya pamoja na zahanati mbalimbali wilayani humo,lisitumike kubeba maiti kwa ajili ya kwenda kwenye mazishi.
Wametoa tamko hilo dakika 10 zilizopita katika kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kinachoendelea hivi sasa katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Diwani wa kata ya Butobela Leonard Kiganga Bugomola ndiye aliyeanzisha hoja hiyo akidai amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa wilaya hiyo,jambo ambalo limekuwa likiwafanya baadhi ya wagonjwa kukataa kuchukua dawa wanazopatiwa kutoka kwenye vituo vya afya na zahanati kwa hofu ya kudhuruika.
Baada ya tarifa hiyo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Elisha Lupuga alimtaka Bwana afya wa wilaya hiyo John Shuma kulizungumzia suala hilo ambapo alikiri na kubainisha kuwa gari hilo limekuwa likitumika pia kubeba maiti ambazo zimekuwa zikikosa ndugu na hivyo kuharibika na kulazimika kuzikwa na Halmashauri ya wilaya,lakini akafafanua kwamba hakuna madhara kufanya hivyo kwa sababu baada ya shughuli hiyo yeye mwenyewe husimamia usafi wake.
Wakuu hili limekaaje??!!