Vituo saba vya Afya, Zahanati vyaanza kutoa huduma Wilayani Mbogwe

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Katika mkakati wa Serikali kuboresha huduma za afya nchini, vituo saba vya afya, zahanati katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita, leo Jumanne Oktoba 10, 2023; vimeanza kutoa huduma baada ya kufunguliwa rasmi.

Akizungumza wakati wa halfla ya ufunguzi huo iliyofanyika katika Kituo cha Afya cha Bukandwe, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Dk Jacob Rombo, amesema ufunguzi wa vituo hivyo ni utekelezaji wa azma ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha huduma za msingi na za muhimu kwa wananchi zinafika bila kusuasua.

Dkt. Jacob ambaye alikuwa akimwakilishwa Mkuu wa wilaya hiyo, amesema katika kuhakikisha kuwa wananchi wa Mbogwe wanaboreshewa huduma, tayari Serikali katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 imetoa Sh1.4 bilioni kama fedha za maendeleo ambapo katika fedha hizo, Sh500 milioni zimeelekezwa katika sekta ya afya.

“...vipaumbele ni kuhakikisha pesa hizo zinanunua vitendea kazi, madawa pamoja na mahitaji ya msingi katika vituo vya afya na zahanati hizo,” amesema na kuongeza;

“...pamoja na Serikali kutoa fedha hizo, imeendelea kuajiri watumishi wa kada ya afya ambapo kwa mwaka wa fedha ulioisha (2022/2023) watumishi 48 walipangiwa na kupokelewa...tumewapokea watumishi 14 na sasa kwa idadi hiyo inaifanya wilaya kuwa na jumla ya watumishi 62 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.”

Katika hatua nyingine, Katibu Tawala, Jacob amewataka watumishi wa kada ya afya wilayani humo kuwa na lugha nzuri na yenye staha kwa wagonjwa na kuwakumbusha kuwahudumia Watanzania wa wilaya hiyo kwa usawa bila ubaguzi wa hali wala mali.

Amesema, azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuona huduma muhimu kwa wananchi zinatolewa kwa viwango na ubora na kwamba yeye kama kiongozi wa watumishi wa Serikali wilayani hapo hayupo tayari kuona wananchi wanalalamika kupatiwa huduma isiyokidhi viwango tarajiwa.
 
Back
Top Bottom