Gari la kusambaza dawa linapobeba Maiti...

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
869
Wakuu,

Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita wametoa tamko la kukataa gari linalotumika katika kusambaza Dawa za Binadamu kwenye vituo vya afya pamoja na zahanati mbalimbali wilayani humo,lisitumike kubeba maiti kwa ajili ya kwenda kwenye mazishi.

Wametoa tamko hilo dakika 10 zilizopita katika kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kinachoendelea hivi sasa katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo.

Diwani wa kata ya Butobela Leonard Kiganga Bugomola ndiye aliyeanzisha hoja hiyo akidai amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa wilaya hiyo,jambo ambalo limekuwa likiwafanya baadhi ya wagonjwa kukataa kuchukua dawa wanazopatiwa kutoka kwenye vituo vya afya na zahanati kwa hofu ya kudhuruika.

Baada ya tarifa hiyo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Elisha Lupuga alimtaka Bwana afya wa wilaya hiyo John Shuma kulizungumzia suala hilo ambapo alikiri na kubainisha kuwa gari hilo limekuwa likitumika pia kubeba maiti ambazo zimekuwa zikikosa ndugu na hivyo kuharibika na kulazimika kuzikwa na Halmashauri ya wilaya,lakini akafafanua kwamba hakuna madhara kufanya hivyo kwa sababu baada ya shughuli hiyo yeye mwenyewe husimamia usafi wake.

Wakuu hili limekaaje??!!
 
Na hapa ndio mimi napenda sana siasa!
Kiukweli tukisema tufuatilie shughuli zinazofanyika hospitali hadi wagonjwa tunapona,basi ipo siku hao madiwani watasema wanataka hospitali zitumie vitanda/matandiko ambayo ni disposable! Mtu akilazwa,anapokuwa anaruhusiwa aondoke na kitanda,godoro na mashuka aliyotumia!

Bwana afya ametolea maelezo kadhia hiyo,na inavyoonekana yeye mwenyewe anasimamia usafi wa gari hilo,sasa hofu ya wananchi inatokea wapi? Hivi tunajua ICU(vyumba vya wagonjwa mahututi) vinavyofanyakazi?! Je,tutupe vifaa vyote vinavyotumika mle ndani?! Au wale wanaofia mle sio maiti?!

Mimi nadhani kuna mambo mengi sana ya msingi kuzungumzia ya kuliko hilo.Tena mimi naweza kupongeza uongozi wa hiyo hospitali kwa kuwa dawa zinapatikana.Vipi kama ambulance ikibeba dawa,kuna shida? Tusisahau kwamba ambulance ni kwa ajili ya kubeba wagonjwa ambao wakati wowote wanakuwa marehemu! Na mara kadhaa wagonjwa wanafia kwenye ambulance,vipi hapo,yenyewe haibebi maiti?!

Kama kweli wagonjwa ndio wamelalamika,mimi nadhani kwanza wangeaza kulalamikia wajawazito kulala mzungu wa nne vitandani,au kulala chini kwa kukosa vitanda,upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya,upatikanaji wa vifaatiba ktk hospitali na vituo vya afya.Au labda inawezekana wilaya hiyo imejitosheleza kwa kila kitu,si ndio maana'ke?!

Kwa hiyo madiwani hao wametoa gari ambayo itakuwa inafanya kazi hiyo,sio? Mimi mwanzo nilidhani inabeba ndugu wa wafanyakazi au inakodiwa,kumbe inabeba marehemu waliokosa ndugu wa kuwazika. Anyway,ni kweli kama kuna uwezekano wa kupata gari nyingine kwa ajili ya kazi hiyo,basi gari la dawa libaki kuwa la dawa,isipokuwa kama hakuna uwezekano huo,gasi halmashauri kupitia kwa hao madiwani waweke utaratibu wa kukodi/kutoa gari tatizo hilo linapokuwa limetokea.
 
Huku kwetu kuna magari yameandikwa MEAT VAN ambayo nyakati za asubuhi hubeba nyama na vilelile kuna meat vans bubu ambazo asubuhi hubeba nyama na mchana hubeba maiti! Cha msingi ni usafi tu kwani ndivyo uchumi wetu unavyoruhusu.
 
Ni uoga tu wa vifo lanii ama gari linasafishwa vizuri na no contamination sioni madhara yake...Miji mingi hapa BONGO magari yanabeba maiti na bado yanatumika kwenye shughuli nyeti nyingi tu na hatuoni madhara ya moja wa moja labda kama kuna masuala ya kitaalamu............
 
Sidhani kama kuna shida kwenye hilo ni usafi tu unatakiwa ni sawa na waliolalamika kusachiwa na askari wa kike,
 
Siku hizi siasa tu kila nyanja,hata panapohitaji maelezo ya kitaalam,inawekwa siasa. Hivi hao madiwani hawana vitu vingine vya msingi vya kujadili badala yake wanajadili jambo hili. Mbona watu wanakula misibani?
 
Back
Top Bottom