Gari la kusambaza bia lapata ajali mnazi mmoja, dsm

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Kama dakika 5 hivi zilizopita imetokea ajali iliyohusisha gari la kusambaza bia la TBL maeneo ya mnazi mmoja Dsm. Ajali hiyo imetokea katika makutano ya barabara ya bibi titi na uhuru ambapo gari hiyo aina ya Isuzu ilifunguka ghafla milango ya upande wa abiria (ubavuni) mara tu taa za kuongozea magari ziliporuhusu. Gari hiyo ilikuwa ikitokea maeneo ya kariakoo na kuelekea mjini kupitia barabara ya Uhuru.

Karibu robo tatu ya crate za bia zilimwagika na zingine kuvunjika. Kama si juhudi za cashier/salesman akisaidiana na askari wa polisi waliokuwa wakilinda benki ya NBC iliyo hapo karibu, basi kungetokea na hasara kubwa zaidi kwani vijana kama 300 hivi walivamia gari hilo na kuanza kuiba bia mpaka salesman huyo alipotoa bastola na kupiga juu ambapo vijana hao walipoona hivyo wakaamua kutawanyika. Mpaka naondoka eneo la tukio hakuna majeruhi niliowaona, ingawa kuna vijana waliokanyagana sana na kuumizwa na vipande vya chupa wakati wakigombania kuiba bia hizo.

Nawashauri madreva kuepuka njia hizo zinazoelekea kwenye makutana ya Bibi titi na uhuru kwani zoezi la kuokota bia na vipande vya chupa inaendelea na hivyo kusababisha foleni kubwa ingawa trafiki tayari wapo eneo la tukio.

Ni hayo tu wadau!!!
 
Tusker bariiiidi upo?......Yule mshikaji wako Makonyagi sijui atakuwa kaishia huko?(joke)
 
Blurp.... Blurp..... Nilikuwa nafanya tathimini ya Tusker zilizovunjika kupitia yule jamaa aliyedaiwa kutoa Bastola Haaaa!!!:eek: (Salesman ana Bastola????!!!!) Asante Salesman kumbe mnatulinda hiviiii!!!!:eek:....All in all ajali hiyo mbaya ya vyupaaa zilizovunjika zaidi ni vya Safari: KWA NIABA YA WANYWAJI WA TUSKER NAWAPA POLE WANYWAJI WA SAFARI...:(:(:(:( Jamani Mako...nyagi yuuu wapi??? Brulp....:???::cry::cry::cry:
 
Back
Top Bottom