Gari la kununua kwa watu wa kipato cha chini

Kagomba

Member
Joined
May 21, 2012
Posts
15
Reaction score
0
Habari wanajamii. Naomba msaada wenu wakuu kuhusu aina ya gari la kununua kwa mtu ambaye bajeti ya mafuta kwa mwezi ni Sh 200,000. naishi Kivule ambapo barabara ni ya mashimo na nafanya Posta mpya. Kuna kaniambia eti nichukue Escudo. Naomba ushauri wataalamu wa magari hasa kuhusu hizo point ya barabara na mafuta:A S tongue:. Asanteni
 
BAJETI YAKO YA MAFUTA IMENONA. Hivi unajua bajeti hiyo hata xtail nissan unadunda nayo. Bila tatizo.
Simaanishi ununue xtrail but nimependa unono wa bajet yako.

Kuna jamaa angu ana Duet kwa mwezi elfu 80 wese.
Ngoja waje kukushaur
 
Nimewahi tumia Escudo kwa maeneo kama yako.
Nakushauri ununue Escudo.
Kwanza ipo juu halafu ni roho ya Paka na pia mafuta ni kawaida sana
.
Huyo anaesema Duet hajua gari hizo kwenye njia mbovu ni mwezi tu utaanza kusikia balaa lake.

Escudo zinavumilia mikikimikiki ya njia kama hizo.

Hao juu jama kasema mafuta Elf 80 kwa mwezi inamaana ni wastan wa 3,000 kwa siku,je kutoka maeneo yapi kwenda wapi kwa siku?
Na wee umesema budget ya Tsh:200,000 kwa mwezi je ni kutoka maeneo gani,maana ni wastan wa Tsh:7,000 kwa mwezi kwa hesabu yako
 
Well said, Kivule nakujua namna kulivyo hovyo hasa wakati wa masika. Gari inayomfaa ni Escudo.
 
Habari wanajamii. Naomba msaada wenu wakuu kuhusu aina ya gari la kununua kwa mtu ambaye bajeti ya mafuta kwa mwezi ni Sh 200,000. naishi Kivule ambapo barabara ni ya mashimo na nafanya Posta mpya. Kuna kaniambia eti nichukue Escudo. Naomba ushauri wataalamu wa magari hasa kuhusu hizo point ya barabara na mafuta:A S tongue:. Asanteni

kwa bajeti hii, title ya post yako inapaswa kubadilishwa...na pia kwa bajeti hii nunua hata landcruser 3500cc
 
Kwa maeneo unayoishi(kivule),naungana na wachangiaji apo juu escudo iz the best,,,,,go on with your plan,,,all the best mkuu
 
Habari wanajamii. Naomba msaada wenu wakuu kuhusu aina ya gari la kununua kwa mtu ambaye bajeti ya mafuta kwa mwezi ni Sh 200,000. naishi Kivule ambapo barabara ni ya mashimo na nafanya Posta mpya. Kuna kaniambia eti nichukue Escudo. Naomba ushauri wataalamu wa magari hasa kuhusu hizo point ya barabara na mafuta:A S tongue:. Asanteni

Nunua Suzuki Kei. Ina milango minne na ukubwa wa injini yake ni cc 650 tu. Lita moja itakupeleka zaidi ya kilomita 20.

Suzuki_Kei_003.JPG
 
Huyo ana pesa anazingua watu tu, hii kitu ni kwa ajili ya sisi wakaidi wa mjini, hii kitu ukiweka full tank mpaka unasahau....wakati mwingine unahisi labda gauge imeharbika, maana mafuta hayaishi! Sema kwa barabara za kivule sijui kwa sababu sijawahi enda!
 
Kwa bajeti hii hata prado unasukuma bajeti imenona mi nakaa kisukuru bajeti yangu 90000
 
Nimeamini kuwa Jamiiforum ni kisima cha maarifa. Nawashukuru sana mnaoendelea kuchangia ila naiomba kusema kidogo khs hiyo bajeti ya 200,000 kwanza ni bajeti ya kila mwezi, pili kumbukeni ninafanya kazi siku tano kwenda kazini napumzika jpili tu. Tatu ninaishi Kivule (wasiojua iko pande za Kitunda) na job iko Posta mpya. Je ndugu zangu kwa bajeti hiyo bado tu itanipeleka mwezi mzima? ndio maana nilisema kipato kidogo na kutaka gari la bajeti hiyo. Suzuko Kei nina wasiwasi itakongoroka mapema. Nadhani wazo la Suzuki Jimny laweza kuwa mwafaka ila sijui issue ya spare parts zake
 
nunua nissan hardbody itakufaa hii gari ina nguvu sana.
 
Baada ya Escudo naunga mkono huyo alieweka hicho Kisuzuki.
Hivyo vigari ni roho ya Paka. labda viwe vimechakachuliwa katika matoleo.
 
Back
Top Bottom