Gari kwa mkopo

Gari kwa mkopo

Search Google nilikuwa nawaangalia jamaa wanaitwa Magari chap chap wanakupa gari kwa kulipia nusu then iliyobaki utalipia ndani ya miaka miwili. Unawaachia kadi mpaka utakapomaliza deni lao.
Atakuja kujuta gari la milion 13 unalipa plus riba milion 21
 
Kama tayari una salary slip 3 zama NMB, NBC au CRDB ukakope mkopo ambao makato yake hayaendi zaidi ya miaka mitatu.
NB: Pata gharama halisi za kununua hiyo gari toka Japan na ushuru wake na bima na takataka ndogondogo ili ujue unahitaji mkopo wa shilingi ngapi. Usinunue gari iliyotumika bongo kwa hela ya mkopo, utalia.
Kuna yard ipo pale manzese kona ya kuingia mabibo wanakopesha gari. Nadhani wanaitwa africars
Umempatia ushauri mzuri ila kwa kuongezea tu;
Hapo Africars wao wameungana na kampuni ina FIN finance; ili ukope unatakiwa kuwa na walau 40% ya gharama ya jumla ya gari.
Hawa FIN wanakuongeza pesa na kuwalipa AFRICARS pesa yote.
Kisha wewe na FIN ndio mnaanza kukatana katika muda mtakaokubaliana.
Riba yao sio haba, inabidi ujipange na uwe tayari kulipa.
 
Hapa ndipo mnapofeli waajiriwa, leo utatamani gari, kesho nyumba, keshokutwa biashara, vyote utahitaji kuchukua mkopo, mwishoe utaona kazi mbaya haina mshahara mzuri kumbe wewe ndiyo mbaya. Utajili utabaki kwa wachache tu.

Sio wote wanataka kua matajiri af acha kudanganya wenzako akunaga tajiri aloajiliwa na anaishi kwakutegemea mshahara
 
Kopa pesa bank kanunue gar usifanye makosa ya kwenda yard kukopa gar makato yake huwa ni makubwa sana
Gar ya 18million ukienda kopa yard inaenda ad 24 million so ni vema km umekamilisha na unavigzo vya kukopesheka ni bora ukope pesa ukanunue gar

Lakin pia ndg zangu tuacheni sana kutafta ushauri Mungu amekupa akili ebu tupende kuumiza akili zetu kutafta solusheni ya mattzo yetu tuache kuomba ushauri wa kla kitu mwisho wa sku ukijibiwa vibaya unaanza lalama

Dunia ya leo vitu ving viko wazi na information nying zinapatkika kwa urahisi kwann mnaomba ushauri ovyo ovyo

Unataka gar ya mkopo ingia mtandaoni wasiliana na wauza magar watakupa utaratibu ulonyooka na wenye kueleweka
Unataka mkopo wa pesa nenda bank husika watakupa maelezo mazur nayakueleweka

Ndio jf kuna watu wa kila kada ila ni
Mara chache sana uzi wako kusomwa na wahusika ambao watakupa majb sahihi

Kuache kuomba omba sana ushauri iyo ni ishala ya upungufu wa akili na maamuzi
 
Kama kuna mdau hapa,ana taarifa juu ya namna ambavyo mtu anayeanza kazi anaweza kupata mkopo wa gari,bila ya kuwa na pesa taslim,ila awe anakatwa kila mwisho wa mwezi.je afanyeje kupata mkopo wa hivyo?
Mdogo wangu naomba nikushauri kwenye maeneo yafuatayo:

1. Angalia mshahara wako kwanza; ukitoa gharama zako za chakula, pango, kusaidia wazazi, na gharama nyingine. Unaweza kuwa na uwezo wa kuweka benki kiasi gani kama savings? Kama ni chini ya Milioni 1, kwa sasa hauhitaji gari bali unahitaji chanzo kingine cha mapato. Mkopo utakutesa sana na utachanganyikiwa.

2. Makampuni ya kukopesha yapo mengi tu ila yote yana riba kubwa sana. Unakopa gari ambayo thamani yake ni 16,000,000/- halafu wanakukata kidogokidogo ndani ya miaka 3 lakini ukimlisha na interest(riba) unakuta umenunua hiyo gari kwa 28,000,000 au 30,000,000/-
Na wakati mwingine wanahitaji walau uwe na 40% halafu mkopo inabaki kwenye 60% ambayo ndio itakayolipiwa na interest.
Unapata gari lakini unaishi kwa mateso sana. Hapa maisha yako yatavurugika kwa kiwango cha juu sana.

3. Kwa mfano bado ukaamua kuendelea na suala la kukopa na ukafanikiwa, gari ni liability, linahitaji huduma za service walau kila baada km 4000, kuna ajali za hapa na pale, hii ina maana kuwa gari halipunguzi gharama zako za maisha. Utabaki na hela kwa ajili ya kulihudumia?
4. Miaka kadhaa iliyopita nilianza kazi kama wewe na nikawa na hamu ya kununua gari, mzee wangu akaniambia jambo la kwanza ni kuweza kumudu mambo madogo ya maisha kabla ya kukimbilia kwenye gari. Kwa kuwa sikuwa na matumizi mengi, nilikuwa na uwezo wa ku-save kila mwezi 50% ya mshahara wangu, baadaye nikaanzisha biashara huku nikiwa kazini; ndani ya miaka 2 nikawa na pesa ya kutosha kuagiza gari kutoka Japan (used car).

Ninachotaka kukushauri ni kuwa usiwe na haraka.

Ila kwa kuwa ulitaka makampuni yanayoweza kukukopesha basi unaweza kuanza na haya:

1. Car Loans - NCBA Tanzania
2. platinum credit ltd mkopo simu namba 0658883703
3. Login • Instagram
4. StackPath
Mambo mengine ya kuzingatia

Leseni ya kukopesha

Hakikisha kwamba mkopeshaji unayemchagua amepewa leseni kwa mujibu wa sheria. Habari hii inaweza kupatikana kutoka kwa hifadhidata za umma zinazodumishwa na wasimamizi wa sekta. Ushirikiano na mkopeshaji aliyeidhinishwa pekee ndio utakaolinda haki zako za watumiaji iwapo kutatokea mizozo.

Fanya Utafiti

Pia ni muhimu kutafiti kampuni kabla ya kuzipa taarifa zozote za kibinafsi au za kifedha. Angalia hakiki na vyanzo vingine vya habari. Kuajiri wakili mwenye uzoefu wa mali isiyohamishika kukagua hati zote ni wazo nzuri ikiwa unanunua bidhaa kubwa kama vile nyumba. Wanaweza pia kukusaidia kuthibitisha uhalali wa mkopeshaji.

Mkopeshaji Mwenya Sifa Nzuri

Unapaswa kufanya kazi na mkopeshaji mwenya sifa nzuri anayekagua mkopo, mapato na mali ya wakopaji wanaowezekana. Jihadhari na wakopeshaji ambao hawafanyi ukaguzi wa kina na hawathibitishi hali ya kifedha ya wateja. Pia, kila wakati tafuta hitilafu katika hati za mkopo, kama vile maelezo ya kibinafsi yasiyo sahihi, ikiwa ni pamoja na Usalama wa Jamii au nambari ya kulipa kodi. Hakikisha kuwa mkopeshaji ana anwani halali ya mahali ulipo, na tovuti yao inapaswa kuwa imejaa maelezo kuhusu mchakato wao wa kukopesha, bidhaa na ada.

Kiwango cha riba

Kufanya utafiti ya kiwango bora cha riba unaweza kukusaidia kuokoa pesa nyingi wakati wa mkopo. Wakopeshaji tofauti wana viwango tofauti, kwa hivyo kulinganisha ofa ni muhimu kabla ya kutulia kwa moja. Zaidi ya hayo, kuchagua mkopo wa muda mrefu kwa kawaida kutasababisha malipo ya chini ya kila mwezi, lakini jumla ya gharama ya mkopo itakuwa kubwa.

Malipo ya Amana

Wakopeshaji wengi wanahitaji angalau malipo mdogo wakati wa kuchukua mkopo wa gari. Kwa ujumla, ikiwa unaweza kulipa amana kubwa, ndivyo mpango utakavyokuwa bora zaidi. Malipo ya amana pia hukusaidia kupata masharti bora ya mkopo na inaweza hata kupunguza kiwango chako cha riba kinachohitajika na / au malipo ya kila mwezi.

Jumla ya Gharama

Hakikisha unazingatia jumla ya gharama za kuchukua mkopo wa gari, ikiwa ni pamoja na usajili, bima, na ukarabati, pamoja na bei ya ununuzi wa gari. Kufanya utafiti kidogo kunaweza kukusaidia kupanga bajeti kwa usahihi zaidi na kuhakikisha mkopo wa gari lako inafaa.

Kila la Kheri
.
 
Hapa ndipo mnapofeli waajiriwa, leo utatamani gari, kesho nyumba, keshokutwa biashara, vyote utahitaji kuchukua mkopo, mwishoe utaona kazi mbaya haina mshahara mzuri kumbe wewe ndiyo mbaya. Utajili utabaki kwa wachache tu.
usikariri maisha bro,
mtu kuanza kazi haina maana kwamba hakuwa na maisha before, wengine wanataka nafasi kurahisisha mambo yao ya pembeni!
 
Mwishowe itabidi atoe jicho
 
Hapa ndipo mnapofeli waajiriwa, leo utatamani gari, kesho nyumba, keshokutwa biashara, vyote utahitaji kuchukua mkopo, mwishoe utaona kazi mbaya haina mshahara mzuri kumbe wewe ndiyo mbaya. Utajili utabaki kwa wachache tu.
Mwenzako ametaka gari,hata hajasema hizi shida zingine wala kusema kwamba anashida ya hizi vitu vingine, why unaanza kumlaumu kuwa hajui anachokifanya?🤔

Wajua sio vema kumvunja moyo mtu anapotaka kufanya jambo lake lolote mradi tu sio baya? Kununua gari sio kitu kibaya,na yeye ameomba kuelekezwa wapi atapata kwa mkopo.
 
Kama unataka kukopa kopa bank
Usikope microfinance au kampuni ya mtu
Huko utatapeliwa utalipa mil 30 gari ya 15 m
Wajinga wale. Wana riba hadi ya 50% ,BOT walishakataza ila jamaa hawasikii.
 
Watu kama hao , huwa wanataka uwe na nusu ya hela ya thamani ya gari.... Halafu wanaweza kukupa mwaka au zaidi kulipa mkopo uliobakia
Kuna wanaotaka uwe na 50% ya gari,kuna ambao wanataka uwe na CIF ya gari tu ,kodi wanalipia wao ndio mkopo upo huko,na kuna moja nimesahau jina, wanataka uwe na 20% ya total cost ya gari wao wanalipia 80% inayobaki then kadi wanabakia nayo.
 
Back
Top Bottom