Gari Jipya La Kisasa la TBC

Gari Jipya La Kisasa la TBC

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
download.jpg
 
Kwa hilo gari kupata Tbc kuna watu roho zitawauma we subiri uone watakavyoanza kutoka povu
 
FKB_3970.JPG
basi la milionea Bakhresa anayemiliki AZAM TV
 
[h=1]SHIRIKA LA TAIFA LA UTANGAZAJI (TBC) LAPATIWA MSAADA WA GARI LA KISASA LA KURUSHIA MATANGAZO KUTOKA KWA SERIKALI YA CHINA[/h]by JOHN BUKUKU on JUNE 27, 2014 in BIASHARA with NO COMMENTSOB6a.jpg
 
Dar es Salaam. Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), limepatiwa gari jipya la kisasa la kurushia matangazo ya nje (OB Van), ambalo kwa mara ya kwanza litatumiwa kwenye matangazo ya sherehe za miaka. 50 ya Muungano wa Tanzania kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Gari hilo kutoka Serikali ya China limeshawasili na tayari mafundi tisa wa Kichina wapo nchini ili kusaidia katika urushaji wa matangazo hayo ya sherehe za Muungano pamoja na kuendesha mafunzo kwa mafundi wa TBC.

Kundi la mafundi wa TBC lilikwenda China wiki chache zilizopita kujifunza jinsi ya kutumia gari hilo ambalo limeelezwa kuwa bora kwa kurushia matangazo ya televisheni ya nje kuliko jingine lolote hapa nchini kwa sasa.

Ofisa mwandamizi wa TBC1 ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema ili kukidhi matakwa ya matumizi ya gari hilo, shirika lao limewajibika kununua gari jingine jipya (pick up) lenye thamani ya Sh60 milioni kwa ajili ya kubebea mtambo rasmi wa gari hilo wa kurushia matangazo yake hayo.

Alisema sherehe rasmi za uzinduzi na makabidhiano ya gari hilo zitafanywa baada ya kumalizika kwa shughuli za sherehe za Muungano.
 
Sioni umuhimu wake kwa kipindi hiki, naamini kuwaandikisha kwenye daftari la kudumu wapiga kura ndio mpango mzima.
 
Sioni umuhimu wake kwa kipindi hiki, naamini kuwaandikisha kwenye daftari la kudumu wapiga kura ndio mpango mzima.

Wala halina tija yoyote kwa taifa, sasa sana ni kutumika tu na ccm kurushia propaganda zao chafu tu., kwani hata sasa huwezi tofautisha tv ya Taifa na ya chama!!
 
Ya Azam ni ya Kijerumani. Ni semi trailer. Ilikisiwa gharama yake ni Tsh 6bn/-

Hilo la TBC ni fupi kwa maana ni dogo kuliko lile la Azam. Hata hivyo hongera zao!
yaani wana kipindi maalum kulinadi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom