Gari Aina Ya "TEKI" Limeharibu Barabara!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Kuna Gari jipya limeingia kwenye msafara kwenye Barabara maarufu ya
"DipuWolidi" iliyotengenezwa hivi karibuni na familia ya "Sero-Kali."
Tatizo hasa ni Mwanga wa "Full Light" unaotolewa na hili gari aina ya "TEKI" unaotumia System maarufu ya kisasa ujulikanayo kama "Why-Rakha" Mwanga huu unasambaa na kumulika kwa kasi na kulifanya gari la "TEKI" kuwaangazia hata wale wasiokuwa Barabarani.
Yaani kuanzia "Barabarani",
"Makasirini"hadi "Vigengeni" na "Jumuiko"za mitaani.

Huku pia likiwaacha mbali wale wanaolitumia gari la mzee "Sero-Kali".

Na tatizo kubwa ni jinsi huu Mwanga aina ya "Why-Rakha"unavyosambaa kwa kasi kuyazidi mataa mengine yanayotumika na Familia ya mwenye Barabara almaarufu "Sero-Kali".

Mzee "Sero-Kali" amechanganyikwa kujawa na hasira,Sababu haoni vizuri mbele!
Wakati wale wanaotumia mwanga wa "Why-rakha" wakizidi kumtangulia huku wakiacha mashimo makubwa Barabarani "DipuWolidi"
Ambayo yanamchelewesha mzee "Sero-Kali"kufika Duu-by!
Sasa "MamaSero-Kali" pia amehamaki na amekanyaga "Eksi-leta" na "Usu-kani"kwa hasira na yeyote anayeshangilia Pembeni ya Barabara!

Washabiki tuko jukwaani tukishuhudia kupitia Ma-Juu kwaa.

....Wa kuelewa tukutane kipindi cha pili....
View attachment 2746821
 
...Hatimae Mama sero-Kali anaelekea Ntwara kupambana na Mwanga wa "TEKI"
 
Back
Top Bottom