Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Miezi michache baada ya wanandoa Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na Gardner Gabriel Fikirini Habash kutalikiana kwenye Mahakama ya Mwanzo Manzese Sinza jijini Dar, mwanaume huyo amemuanika ‘mtu wake’ wa sasa a.ka. ‘mwendokasi’ akisema ndiye mrithi wa mikoba ya mwimbaji huyo nyota wa Muziki wa Kizazi Kipya.
Katika Viwanja vya Escape One, Kawe, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, ambako mwimbaji mahiri wa Muziki wa Dansi Bongo, Christian Bella alikuwa akifanya shoo ya kutimiza miaka 10 katika ‘game’, Gardner alionekana na mrembo huyo akizunguka naye kimahaba kutoka eneo moja kwenda lingine huku wadau wake wakihoji ni nani!
Garder alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alikiri kuwa ni kweli kwa sasa anamiliki kifaa kipya kinachokwenda kwa jina la Vestina.
“Yes! Ndiye huyo kaka. Huyo ndiye mtu wangu kwa sasa na kama nilivyowahi kukudokeza, nimekuwa naye kwa muda mrefu kidogo, lakini sikuweza kumwanika mapema kwa sababu zinazoeleweka au ninazozijua mwenyewe,” alisema Gardner.
Mwandishi: “Vipi kuhusu Jide sasa, ndiyo n’tolee moja kwa moja kwa sababu ya talaka?”
Gardner: “Jide kitu gani bwana? Huyo ndo’ mwendokasi wangu kwa sasa.”
Gardner alimtaja binti huyo aliyekataa kusema umri wake kuwa anaitwa Vestina Jax, mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari hizi alilitaka kufahamu kama kuna mipango yoyote ya kufunga ndoa katika siku za karibuni baina yake na mrembo huyo, lakini Gardner alikataa kusema lolote juu ya hilo.
“Duu! Acha basi kaka! Kwa hilo sina comment,” alisema mtangazaji huyo ingawa habari za ndani zaidi zinasema kuwa, mrembo huyo ndiye mkewe mratajiwa.
Source: Bongo Movie