Gamondi: Sijawaona Aziz Ki na Diarra kambini mpaka sasa

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,914
6,032
Stephen Aziz Ki na Djigui Diarra bado sijawaona kambini na walipaswa kuwa wamerejea kutoka kwenye majukumu yao ya timu zao za taifa”

- Kocha Miguel Gamondi, Yanga Afrika.

Yapi maoni yako??
 
Hata me hii habari imenichanganya sana.
FB_IMG_1711709581009.jpg
 
Toka Mamelodi ilipotangazwa kucheza na Yanga, uongozi wa Yanga ulishaanza kujenga mazingira ya jinsi ya kujitetea na zahma iliyo mbele yao. Mapema sana viongozi na mashabiki walishaanza kuchanganyikiwa.

Walitaka wachezaji wao wasiitwe timu ya taifa wakati huo huo wakalalamika saaana kwa nini Dickson Job hajaitwa, hiyo ni dalili ya watu waliochanganyikiwa. Wakaja kwenye majeruhi ya Pacome mara ishu ikabuma kwa kuitwa na kwenda timu ya taifa, eti anaenda kuangaliwa na madaktari wa timu ya taifa, dalili nyingine ya watu waliochanganyikiwa. Wakaja kwenye vitisho vizito dhidi ya watakaovaa jezi za Mamelodi, baada ya kelele nyingi na barua nzito kutoka CAF, wakanywea.

Sasa hivi wanasema kina Diarra hawajarudi mpaka sasa na wale ambao walisema wameshapona wanadai wanaweza kuwakosa. Dalili za watu waliochanganyikiwa. Hizi taarifa ndiyo kabisa zitafanya mashabiki wao hata wale wa bure wasije uwanjani.

Hii mechi Yanga ingekaza bila kucheza hizi mind games ingeweza kutoboa. Tatizo imefanya mambo yamekuwa mengi.
 
Kama hawatapangwa na game yanga akapoteza basi uongozi wa yanga unatakiwa kuchunguzwa kwa kuhujumu timu

Wachezaji waliocheza game j3 na j4 wanashindwaje kufika Tanzania mpaka siku 3 kutoka ufaransa? Na hapo Africa magharibi?

safari ya Massa 8 mpaka 10 wachezaji wanachukua Massa 48 kurudi?

halafu pakome kama alikuwa mgonjwa aliwezaje kukaa kwenye benchi la timu ya taifa?

Kama ikitokea ikawa kweli basi yanga haina uongozi !!!

game ya robo fainali inatakiwa kila mtu ajitoe atoe mchango wake kwa maslahi ya mpira.

binafsi siendi uwanjani mpaka hapa !!
 
Ndiyo maana timu ilitakiwa kuwasilisha CAF Majina ya wachezaji 30

Hivyo sioni kama ni excuse ya maana wakati huu

Wanasema Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge 😜
 
Toka Mamelodi ilipotangazwa kucheza na Yanga, uongozi wa Yanga ulishaanza kujenga mazingira ya jinsi ya kujitetea na zahma iliyo mbele yao. Mapema sana viongozi na mashabiki walishaanza kuchanganyikiwa.

Walitaka wachezaji wao wasiitwe timu ya taifa wakati huo huo wakalalamika saaana kwa nini Dickson Job hajaitwa, hiyo ni dalili ya watu waliochanganyikiwa. Wakaja kwenye majeruhi ya Pacome mara ishu ikabuma kwa kuitwa na kwenda timu ya taifa, eti anaenda kuangaliwa na madaktari wa timu ya taifa, dalili nyingine ya watu waliochanganyikiwa. Wakaja kwenye vitisho vizito dhidi ya watakaovaa jezi za Mamelodi, baada ya kelele nyingi na barua nzito kutoka CAF, wakanywea.

Sasa hivi wanasema kina Diarra hawajarudi mpaka sasa na wale ambao walisema wameshapona wanadai wanaweza kuwakosa. Dalili za watu waliochanganyikiwa. Hizi taarifa ndiyo kabisa zitafanya mashabiki wao hata wale wa bure wasije uwanjani.

Hii mechi Yanga ingekaza bila kucheza hizi mind games ingeweza kutoboa. Tatizo imefanya mambo yamekuwa mengi.

Mbona umeandika uongo na maelezo yaliyojaa hisia zako?

Yanga wangetaka wachezaji wao wasiitwe kwenda kwenye timu zao za taifa wangetoa statement kwenda kwenye hizo timu kuwa wachezaji wake hawawezi kwenda na hata wangezingizia majeruhi. Kwani kwa akili yako walioitwa wote walienda? Si kuna wachezaji wa vilabu vingine wameitwa na hawakuenda na sababu ikiwa majeraha. Hivyo hata kwa Pacome na wengineo Yanga wangetaka wasiende wangetoa taarifa kuwa Pacome ni majeruhi na hakuna kitu wangefanywa na hizo nchi.

Kuhusu kuvaa jezi za Mamelod aliyekataa ni waziri wako wa michezo na hakukataa za Mamelod pekee bali za timu zote za pinzani (Al Ahly na Mamelod) je wewe ulimsikia kiongozi gani wa Yanga akikataza?

Kuhusu Diarra na Aziz Ki kutofika kama ni kweli bado, huwa inatokana na mazingira magumu ya ndege kuja Tanzania.

Kuhusu majeruhi, pengine mchezo wa mpira umeanza kufatilia juzi hapa. Mchezaji kupona jeraha ni swala moja ila kuwa fit ni swala lingine. Kocha alichokiongelea hapo ni ishu ya fitness ya mchezaji kucheza kwenye ngumu. Nyie mnawaona tu uwanjani Aucho yupo mazoezini au Pacome yupo mazoezini na wenzake ila je anatimamu wa asilimia mia? Hilo ndilo linaloongelewa na kocha.

Kuwa mwanamichezo, sio kila mara unakuwa unatawaliwa na akili za kishabiki shabiki hata kufanya reasoning inakushinda
 
Yanga na Pacome wasingeweza kuacha hiyo fursa ya kuitwa kwa mara ya kwanza ndiyo maana ishu ikabuma wakaona we nenda tu hii nafasi ni adimu.

Ni klabu yenyewe iliyosema ameenda kuangaliwa na madaktari wa timu ya taifa, wewe hilo linakuingia akilini kweli mchezaji anaitwa kwa mara ya kwanza, tena anaitwa baada ya mwingine kuachwa kutokana na kuwa majeruhi, halafu aende kuangaliwa majeraha yake? Kama alikwenda akiwa majeruhi basi mliwadanganya kuwa yuko fit kiafya ili fursa isimpite, vyovyote iwavyo kuna udanganyifu ulifanyika.

Mengine nitakujibu baadae nikitulia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom