Kama hii habari ni ya kweli, basi tuna tatizo sana. Kuna wakati inabidi maamuzi yafanyike kwa maslahi ya nchi. Hatuwezi kuendelea na kesi za changuzi kwa miaka! Nchi hii tuna matatizo mengi mno, kuna maeneo sasa hivi watu wanakufa njaa mfano Ngorongoro (Gazeti la Raia Mwema week hii), lakini tunapoteza hela kwa kesi zisizo na kichwa wala miguu!
Na jambo la kusikitisha kwenye hii kesi ya Lema, mtu ambaye inasemekana ndiye alikashfiwa hajaleta mashtka. Batilta yuko Nairobi anaendelea na shughuli zake, huku nyumbani tunapoteza muda, hela kwa madai kuwa kakashfiwa. Mbona yeye kakaa kimya?