Game on - CCM kukata rufaa ushindi wa Lema

Game on - CCM kukata rufaa ushindi wa Lema

Status
Not open for further replies.
Watakateje rufaa ilhali vikatio vyote tumeondoka navyo
 
jamani hii ni rufaa alikatiwa ccm sasa wataenda mahakama gani, labda magogoni kwa jk... Kwani na penyewe si nasikia kuna court??????


Umesahau mgomo wa sensa waislam walivogoma JK akasema weka ndani, walipoandamana akasema futa kesi. Je Unamaana hujui primary and high court ni magogoni siku hizi? Uko dunia gani wewe
 
Kwenye ukweli sometime usilete mambo ya nyumbani kwako hapo! Shenzi sana na hata hauna haya! Na mambo ya FACEBOOK usiyalete hapa!


Mchezo kama wa Dowans na TANESCO,akishinda huyu kesho mwenzake anakata rufaa!
 
Hivi kirusi chetu Zitto kimetoa pongezi kwenye fB au Twitter? Naona Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Msigwa wamerusha.


Hawezi rusha pongezi anaongozwa na roho ya umimi Zitto. kwanza haonekani jf wala fb toka Ben amwage mboga Aibu yamemkuta kijana....
 
Last edited by a moderator:
Ila matokeo ya kumrudishia ubunge Lema yanaweza kuifanya Xmas isiliwe vizuri kwenye kwenye familia ya wakina Mughwai maana kaka kashindwa na mdogo wake.

Ila kwenye hiyo rufaa juu ya rufaa inafunguliwa mahakama ya East Africa au the Hague? au huwa kuna rufaaa kwenye hukumu ya mahakama ya rufaa kwa Tanzania? au kuna kipengele cha kwenda kwa Arbitrator huko London kama ilivykuwa kwa Richmond/Dowans?
 
Jamani, Mahakama ya rufaa ndo ya mwisho. Labda aende mahakama kama aliyokuwa akisemea Joyce Banda ambayo TZ si mwanachama! Hilo tu!
 
acha waende maana kama majaji na mwanasheria mkuu wa serikali kashaamua yatakuwa kama yale ya Mama wa Ubungo anakata rufaa halafu anaingia mitini aibu wasubirie mwaka 2015 hapa watapoteza muda wao bahati nzuri leo niliwaona akina mama fulani wamevalia wavazi ya kijani mbona ilikuwa aibu sana
 
Acha umbumbumbu wa sheria,court of appeal ndo inatoa uamuz wa mwisho
 
Mchezo kama wa Dowans na TANESCO,akishinda huyu kesho mwenzake anakata rufaa!

Daah hii kali;Mahakama ya rufaa ikitoa maamuzi ya ndani HAYAWEZI PINGWA SEHEMU YYT ILE DUNIANI hasa kama HAKUKUWA NA SHTAKA LA UVUNJWAJI WA KATIBA YA NCHI na UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAM!

Kesi ya Ubunge wa Lema inaangukia kwenye kesi zinazoongozwa na sheria ya uchaguzi ya Tanzania!
 
Watakata rufaa katika mahakama ipi ya rufaa..........? Ya afrika mashariki au ICC?
 
I

Ila kwenye hiyo rufaa juu ya rufaa inafunguliwa mahakama ya East Africa au the Hague?

Mahakama hizo ulizozitaja hapo juu zinasikiliza kesi za uvunjwaji wa katiba na uvunjwaji wa haki za bindamu tu na sio kama hizi za ucnaguzi wa Arusha!

Mchungaji Mtikila kakimbilia kwenye mahakama ya EA kwa sababu ana amini kuwa kukatiliwa mgombea huru ni ukiukwaji wa katiba ya nchi kipengele kisemacho"KILA MTU ANA HAKI YA KUCHAGUA NA KUCHAGULIWA KWEYE SANDUKU LA KURA"!
 
Ha ha haaaaaa, utakuwa umbumbumbu wa sheria uliopitiliza!

Unachekesha wewe... sasa mbona CDM walikata rufaa waliposhindwa kwenye hukumu ya kwanza. Si wangeacha tu. Acha watu wacheze na fani zao. Ndio ajira inaendelea hivyo. Unafikiri Kimomogolo yule wakil kazi ameifanya bure. Wale mawakili wa serikali si walilipwa kwenda Arusha kwenye kesi? Kufa kufaana.
 
aaaah wapi , hakuna kitu kama hicho tena , hiyo ndiyo imetoka, kwa ufahamu wangu mdogo wa mambo ya sheria , mahakama ya rufani ikiisha toa uamuzi wake ,ndio unakuwa wa mwisho, unless otherwise utakuwa ni mchezo wa kitoto tena
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom