Gambo amwambia DED na viongozi Arusha hatishiwi Nyau

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amewaambia viongozi wa wilaya ya Arusha na mkurugenzi wa jiji la Arusha(DED) kuwa hatakubali kukwamishwa na viongozi wa jiji la Arusha wakati akitekeleza majukumu yake.

Gambo ameyasema hayo wakati akiongea kwenye mkutano wa Baraza la wanawake wa UWT uliofanyika kwenye hotel ya Mount Meru jiji hapa na kusisitiza kwamba hataacha kuwatetea wananchi licha ya vikwazo vingi anavyopitia kwenye mikutano yake ya kutatua kero za wananchi.

"Nimesikia kwamba wamepanga kunikamata, sitaogopa mtu Mimi ni mbunge ninayetimiza wajibu wangu sitishiwi Nyau na waache kufanya Mambo ya kishabiki" Alisema Gambo

Aliongeza kuwa Kuna mkakati unaoendeshwa na mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dkt. John Pima wa kuwazuia watendaji kushiriki mikutano yake inayoendelea katika mitaa mbalimbali katika Jimbo la Arusha.

"Mkurugenzi amewahi kuwatoa watendaji wa halmashauri katika kikao changu lakini kwa sababu ni mgeni naamini anaendelea kujifunza atazoea" Alisema

Gambo anatuhumiwa kuwashawishi wafanyabiashara wa maduka wasilipe Kodi baada ya kuamuru maduka yaliyofungwa kwa sababu ya kutolipa Kodi yafunguliwe Jambo ambalo linaikosesha mapato serikali.

Gambo.jpg
 
Nakaona hako kaDC ka arusha kama kanaharajati flani hivi kajinga kasikojua la kufanya .kana dhani ofisi ya DC ni sawa na ile ya uvccm iringa
 
Hivi siasa bado zipo
Sio siasa hizi, ni kwamba kila mtu anapambana kukamilisha targets zake za kazi
Aliwahi kuniambia boss wangu ukiona kwenye uongozi wako idara zinakubaliana tuu kila kitu bila kuulizana na kuelezana changamoto ujue kuna tatizo😂😂

 
Back
Top Bottom