Gamba la c.c.m ni hili hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gamba la c.c.m ni hili hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kulwa12, Oct 23, 2011.

 1. k

  kulwa12 Senior Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KUMEKUA NA MJADALA NA MITAZAMO MBALIMBALI NA HASA BAADHI YA VIONGOZI WA C.C.M KUSHINDWA KUJUA AU KUWA NA TAFASIRI HALISI YA NINI HASA MAANA NA MADHUMUNI YA OEPRATION YA KUJIVUA GAMBA, NINI HASA KIDFANYIKE,NINI MATATIZO NA NINI KILICHOKIFIKISHA CHAMA HAPA TULIPO? MATOKEO YAKE OPERATION KUJIVUA GAMBA IMECHUKUA SURA YA VITA YA MAKUNDI NDANI YA CHAMA,DHIDI YA WATU FULANI NDANI YA CHAMA NA MITAZAMO BADALA YA MATATIZO HALISI YALIYOSABABISHA C.C.M IFIKE HAPO ILIPOFIKA.NAOMBA KUMLEJEA MWALIMU NYERERE KATIKA KUJENGO HOJA ZANGU.

  (1) NINI LENGO KUU LA CHAMA HIKI (C.C.M) BAADA UHURU?

  WIKI CHACHE BAADA YA UHURU,MWALI NYERERE ALIJIUZURU NAFASI YAKE YA UWAZIRI MKUU NA UONGOZI WA SERIKALI ILI AKAJENGE UPYA CHAMA CHA TANU,NAOMBA NINUKUU MAMBO KADHAA KATIKA HOTOBA YAKE YA UAMUZI HUU ALIOITOA TAREHE 22,JANUARY,1962.
  KWANZA, "OUR NEW OBJECTIVE-THE CREATION OF A COUNTRY IN WHICH THE PEOPLE TAKE A FULL ACTIVE PART IN FIGHT AGAINST POVERY,IGNORANCE AND DISEASES ...TO ACHIEVE THIS PURPOSE ITS NECESSARY TO HAVE AN ABLE GOVERNMENT WHICH HAS FULL SUPPORT AND CO-OPERATION OF THE PEOPLE..ITS ALSO NECESSARY TO HAVE A STRONG POLITICAL ORGANIZATION ACTIVE IN EVERY VILLAGE,WHICH ACTS AS A TWO WAY ALL WEATHER ALL WEATHER ROAD,ALONG WHICH THE PURPOSES,PLANS AND PROBLEMS OF THE gOVERNMENT CAN TRAVEL TO THE PEOPLE,AT THE SAME TIME AS THE IDEAS,DESIRES AND MISUNDERSTANDING OF TH EPEOPLE CAN TRAVEL DIRECT TO THE GOVERNMENT.THIS IS THE jOB OF NEW TANU (C.C.M)" (MWISHO WA KUNUKUU),KWA TAFASIRI YANGU ISIYO RASIMI MLM NYERERE ALISEMA "LENGO LETU JIPYA NI KUUNDA NCHI AMBAYO WATU WOTE WATASHIRIKI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UMASIKINI,UJINGA NA MAGONJWA..ILI KUFIKIA LENGO HILI NI MUHIMU KUWA NA SERIKALI YENYE KUUNGWA MKONO KWA DHATI NA USHIRIKIANO KAMILI KUTOKA KWA WATU..PIA NI MUHIMU KUWA NA TAASISI YA KISIASA IMARA YENYE UHAI KATIKA KILA KIJIJI,NA AMBAYO ITAKUA KAMA BARABARA YENYE NJIA MBILI NA INAYOPITIKA KATIKA MAJIRA YOTE YA HALI YA HEWA,KUPITIA YENYEWE MALENGO,MIPAMGO NA MATATIZO YA SERIKALI YATAENDA MOJA KWA MOJA KWA WATU ,NA WAKATI HUOHUO MAWAZO,MATAMANIO NA MATATIZO YA WATU YATASAFIRI MOJA KWA MOJA KUIFIKIA SERIKARI.HII NDIO KAZI MPYA YA TANU (C.C.M)". JE BADO C.C.M INATEKELEZA MALENGO HAYA YA KUANZISHWA KWAKE? JE BADO INAFATA MISINGI ILE ILE YA KUANZISHWA KWAKE NA KUTEKELEZA JUKUMU LA KUANZSIHWA KWAKE KWA WANANCHI? JE BADO C.CM NI CHOMBO CHA WANANCHI? TAFAKARINI

  (2) NINI WAJIBU NA KAZI YA CHAMA (C.CM) KWA SERIKALI TAWALA NA KWA WANANCHI?

  TAREHE 7,JUNE.1968,MWALIMU NYERERE ALITOA HOTUBA YENYE KICHWA CHA HABARI "THE PARTY MUST SPEAK FOR THE PEOPLE",NAOMBA KUNUKU MANENO MACHACHE, "OUR PEOPLE'S GOVERNMENT MUST BE BACKED UP BY STRONG PARTY DEEPLY ROOTED IN THE PEOPLE,AND CAPABLE OF PROVIDING A LIVING LINK BETWEEN THE PEOPLE AND THE GOVERNMENT",TAFSIRI ISIYO RASIMI (SERIKALI YETU ZA WATU LAZIMA ISAIDIWE NA CHAMA IMARA CHENYE MIZIZI ILIOJIKITA KATIKA WATU,NA CHENYE UWEZO WA KUWANGANISHI HAI KATI YA WATU NA SERIKALI" ).
  NAOMBA NINUKUU TENA " "THE PARTY HAS TO HELP THE PEOPLE TO UNDERSTAND WHAT THE GOVERNMENT IS DOING AND WHY...IT HAS TO ENSURE THAT THE GOVERNMENT STAYS IN CLOSE TOUCH WITH THE FEELINGS,THE DIFFICULTIES AND THE ASPIRATIONS OF THE PEOPLE.IT HAS TO SPEAK FOR THE PEOPLE" (CHAMA KINATAKIWA KIWASIDIE WANANCHI KUELEWA NINI SERIKALI INAFANYA NA KWANINI...KIHAKIKISHE SERIKALI INAKUA KARIBU NA WATU,HISIA ZAO,MATATIZO YAO NA MATAMANIO YAO.LAZIMA KIWE SAUTI YA WATU")

  NAOMBA NINUKUU TENA "IT IS THE GOVERNMENT WHICH IS THE INSTRUMENT THROUGH WHICH THE PARTY IMPLEMENT THE WISHES OF THE PEOPLE AND SERVE THEIR INTERESTS...THE PARTY HAS TO DETERMINE THE BASIC PRINCIPLES ON WHICH THE GOVERNMENT ACT"
  (SERIKALI NI CHOMBO AMABACHO CHAMA KINATEKELEZA MATAKWA NA MATAMANIO YA WATU..CHAMA NDIO KINATAKIWA KUTAMBUA MISINGI NA KANUNI AMBAZO CHINI YAKE SERIKALI ITAFANYA KAZI ZAKE"
  JE .C.CM INATEKELEZA WAJIBU WAKE KWA WANANCHI NA KWA SERIKALI KWA UPANDE MWINGINE? TAFAKARI.

  (3) NINI MCHANGO WA CHAMA KWENYE UTENDAJI WA VIONGOZI(SERIKALI) KWA WATU WANAONGOZA?

  NAOMBA KUNUKUU TENA HOTUBA HIYO HIYO (THE PARTY MUST SPEAK FOR THE PEOPLE),
  PRESIDENT,MINISTERS,MEMBERS OF PARLIAMENT..IF THEY ARE GOOD,THEY ARE GOOD,THEY ARE GOOD LARGELY BECAUSE THEY ARE BACKED UP BY A STRONG POLITICAL PARTY,WHICH KNOWS AND UNDERSTAND THE PEOPLE'S NEEDS AND PEOPLE'S FEELINGS...AND IF LEADERS ARE ABUSING THEIR POSITION,OR GETTING OUT OF TOUCH WITH THE PEOPLE,ITS LARGELY BECAUSE THE PARTY IS FALLING TO SPEAK FOR THE PEOPLE,AND ACT AS PEOPLE'S WATCHDOGS" (RAIS,MAWAZIRI,WABUNGE KAMA NI WAZURI,NI WAZURI KWA KIWANGU KIKUBWA KWA SABABU WANASAIDIWA NA CHAMA IMARA,KINACHUJUA MAITAJI NA HISIA ZA WATU..NA KAMA VIONGOZI WANA TUMIA VIBAYA NAFASI ZAO NA KUPOTEZA MASHIKO KWA WANANCHI,KWA KIWANGO KIBWA NI SABABU CHAMA KIMESHINDWA KUWA MSEMAJI WA WATU NA KWA MLINZI WA HAKI ZA WATU).
  JE VIONGOZI NA WATENDAJI WA SERIKALI WANATEKELEZA MAJUKUMU YAO KADIRI YA MATAKWA YA CHAMA? JE CHAMA KINA UADILIFU WA KUWEZA KUWA CHOMBO CHA KUSIMAMIA UTENDAJI NA UADILIFU WA VIONGOZI WA SERIKALI? JE C.C.M BADO NI MSEMAJI WA WATU KWA SERIKALI??TAFAKARI.

  (4) NINI DALILI NA HATIMA YA CHAMA (C.C.M) KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE??

  KAMA CHAMA KIKISHIWNDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA UFANISNI KWA SERIKALI YAKE TAWALA NA KWA WANANCHI,HASA YA KUWA CHUMBO CHA KUIUNGANISHA SERIKALI NA WATU NA WATU NA SERIKALI KWA UPANDE MWINGINE,HILI LIKITOKEA HUTOKEA HALI YA KUITILAFIANA/KUTOELEWANA KATI YA SERIKALI NA WANANCHI NA MWISHO WAKE NI WANANCHI KUTUMIWA NA BAADHI YA WATU WENYNE MASILAHI BINAFSI KUHUJUMU MAENDELEAO YAO YENYEWE NA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI,KAMA MWALIMU NYERERE ANAVYO AINISHA " PEOPLE MAY BECOME HOSTILE TO THEIR GOVERNMENT BECAUSE THIS MISUNDERSTANDING...THEN ALLOW THEMSELVES TO BE USED AGAINST THEIR OWN GOVERNMENT BY PEOPLE WHO WISH TO USE PEOPLE'S POWER FOR PERSONAL ADVANTAGE" ("WANANCHI WANAWEZA KUJENGA UHASAMA NA SERIKALI YAO KWA SABABU YA MCHANGANYIKO NA MWISHOWE NI KUKUBALI KUTUMIWA DHIDI YA SERIKALI YAO WENYEWE NA WATU WANAO PENDA KUTUMIA NGUVU YA UMMA KWA MANUFAA YAO BINAFSI)
  JE NINI MCHANGO WA C.C.M KWA HALI YA CHUKI YA WANANCHI DHIDI YA SERIKALI TAWALA? JE CHAMA KINATIMIZA WAJIBU WAKE WA KUWAFANYA WANANCHI WAELEWE NINI SERIKALI YAO INAFANYA NA WASITUMIWE KWA MSILAHI YA WATU BINFSI?? TAFAKARI!

  (5) NI C.C.M AINA GANI INAWEZA KUISIMAMIA,KUKOSOA NA KUIAMBIA SERIKALI NINI CHA KUFANYA?

  NAOMBA TENA NIMNUKUU MWALIMU NYERERE '..ONLY PARTY WHICH IS ROOTED IN THE HEARTS OF THE PEOPLE..ONLY SUCH PARTY CAN TELL THE GOVERNMENT WHAT ARE PEOPLE'S PURPOSES,AND WHETHER THESE ARE BEING CALLED OUT EFFECTIVELY" ("CHAMA PEKEE KILICHJIKITA KATIKA MIOYO YA WATU NDIYO KINAWEZA KUIAMBIA SERIKALI NINI MATAKWA YA WATU NA KAMA YANATEKELEZWA KWA UFANISI") JE C.C.M BADO NI CHAMA AMBACHO KIMEJIKITA KWENYE MIOYO YA WATU? JE KINAJUA MALENGO YA WANANCHI? JE C.C.M INAWEZA KUISIMAMIZA SERIKALI NA KUIELEZA NINI MATAKWA YA WANANCHI?? BILA HOFU WALA KUFICHA? TAFAKARI!!

  HITIMISHO:
  NAAMINI KABISA MATATIZO NA CHANZO KIKUBWA KILICHOFANYA C.C.M IFIKE HAPO ILIPOFIKA ALEO NI KWENDA KINYUME AU KUFANYA MAMBO KADHAA NILIOYATAJA HAPO JUU,NA ISIPOZINGATIA KWA MAKINI MASULA HAYO KATIKA KUJIVUA GAMBA HAKIKA MWISHO WA C.C.M UMEFIKA.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  siasa, siasa, siasa, siasa..............................
  njaa, njaa, njaa, njaaaaaaaaaaaaaaaaaa........
  shida shida shida...............................
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  we have to libyalize the country soon
  we are tired of this guta politics kwa kweli.
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Jifunze kuandika. Unapaswa kuelewa matumizi ya herufi kubwa na ndogo.
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  ignore hizo punctuation, hiyo dozi je umeipata? au unaogopa/hutaki kusikia ccm inakufa!
   
Loading...