Gadna amjibu Jide, akataa kuomba msamaha

sonofobia

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
908
3,441
1463732460605.jpg
1463732488647.jpg


Haya ndio majibu ya G Habash kupitia mwanasheria wake.
 
Kazi ipo, naona wamekutana wajuaji kwa wajuaji, hii mambo ya sheria ni mambo ya kitaalamu hii, ngoja tuone.
 
...hahahahahaha,,halafu jamaa kamjibu siku moja kabla ya show,sasa cjui nikumdhibiti kesho asiropoke kitu jukwaani au?
 
MATTERS OF THE HEARTS AND BROKEN ONES IN SPECIAL CASES ARE VERY COMPLEX TO BE HANDLED WITHOUT SENSE OF CARE......
JIDE HAS TO LISTEN AND LEARN FROM THE SONG "GAMBLER" BY KENNY ROGERS......TIMING IN DOING ANYTHING IS ONE OF THE ESSENTIAL INGREDIENTS TOWARDS SUCCESSFUL EXECUTION OF THE MOVE.
 
Ukisoma barua zote mbili ni dhahili wanasheria was Jide bado sana kwenye fani ya sheria.
Wajipange upya au waondoke na aibu
Mimi niliwahi kuuliza humu, ni wapi jina la Jide lilitajwa kwenye ile video clip? Hata kama kimaudhui alimkusudia huyo, lakini kisheria huwez kuthibitisha pasi na shaka kuwa aliyetajwa ni Jide. Sheria ni ngumu jamani. Nadhan kila mmoja aendelee na hamsini zake!
 
Mbona huyu jamaa anaonekana mwoga? Nilidhani yuko bold kumbe anatukana halafu anajificha! Aendelee kutetea misimamo yake asikimbie.

Maoni yangu, ni kwamba ndoa ni mahusiano rasmi ya watu wawili.
Kila mtu ana mazuri na matatizo yake ya ndani na nje. Kikubwa ni kuheshimiana tu kwa sababu kuachana ni sauti tosha kwamba hamwezi kuendelea kuwa pamoja.

Tabia za kuanza kupigana madongo ni ushamba na umaskini wa fikra. Kila mtu aendelee na maisha yake kwa kuwa hakuna mtu ataishi maisha ya jana. Jana yao ilikuwa mbovu ndiyo maana wakaafikiana kuunda kesho zao katika mfumo mpya.

Matusi na kashfa baada ay kutengana ni dalili ya kukosa mwelekeo mpya, kukaa njia panda lakini bila uwezo wa kurudi nyuma. Watapata mwelekeo sahihi wa maisha kwa kutulia na kupanga ustaarabu mpya ili kutorudia makosa, kutokuendeleza uchungu miongoni mwao na kuwa na future nzuri zaidi. Hakuna amani katika matusi, hakuna hatima katika kukurupuka, na hakuna satisfaction katika maisha artificial!.

Waachae ujinga, wasonge mbele kila mtu na maisha yake. Watajisifia kuwa walifanya maamuzi sahihi kama watakuwa na mwisho uliobora kuliko walikotoka, kitu ambacho hawakipati kwa kudhalilishana!.
 
Back
Top Bottom