Gadget Show April 11-15 Birmingham, UK . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gadget Show April 11-15 Birmingham, UK .

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Richard, Apr 3, 2012.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Maonyesho maalum ya bidhaa za kiteknolojia yanatarajiwa kufanyika mwezi huu katika mji wa Birmingham nchini Uingereza kuanzia tarehe 11 hadi 15.

  Maonyesho hayo ambayo hukutanisha kampuni mbalimbali zinazotengeneza vifaa mbali mbali za kiteknolojia vikiwemo Televisheni za kawaida na zile zitumiazo muonekano wa pande 3 au 3 Dimension 3D, simu za mikononi, computer ndogo ya mkononi (Ipad).

  Kampuni kama za Acer, Medion, LG, Kodak, Lenovo, Philips, Samsung na Sony zote zitakuwa zikionesha bidhaa zao.

  Kuna kanda au zones kumi ambazo kila moja itakuwa ikitoa nafasi kwa mashuhuda kuona jinsi technolojia inavyobadilika kila kukicha.

  International Future Zone- hapa vifaa vipya vya kutumika wakati ujao vitaonyeshwa kikiwemo kifaa kinachoitwa "Necomimi smart cat ears" ambacho kinatengenezwa na kampuni ya Neurosky. Ni kifaa ambacho kinaifanya akili yako iwasiliane na utashi wako na kufanya kazi ya kuwezesha mwili na uwezo wa binadamu kuweza kuwasiliana na kifaa hiki.

  Music Zone- hii inajulikana.

  Home Gadget Zone- vifaa vipya vya kutumia nyumbani vitaonyeshwa hapa.

  Active Zone- Vifaa vya kutumia nje kama mtu unafanya shughuli kama za kukimbia, au mazoezi basi kutakuwa na vifaa mbalimbali vya kusaidia mambo hayo.

  In Car Zone - Hapa vifaa vyote vya music kwenye gari au car entertainment system na GPS vitakuwepo.

  Photographic Zone - Hapa magwiji wa huduma hii Canon na Polaroid watakuwepo miongoni mwa washiriki wengine ambao wanatoa vifaa shiriki au accessories kama kampuni ya Lowepro.

  Zones zingine ni kama Game, Hall of Fame na Showcase stage na Hub theatre.

  Moja ya vifaa ambavyo vimenivutia ambacho pia kitaonyeshwa kwenye maonyesho hayo ni kile kinachoitwa Western Digital TV streaming live media player ambacho kinaunganishwa na Televisheni ili kuona picha za video.

  Mara nyingi tumezoea kuangali picha za video katika mtandao wa You Tube, kutoka kwa marafiki au hata familia kwa kutumia computer lakini sasa kifaa hiki kitakuwezesha kuona video hizo kupitia kwenye Televisheni. Kinaunganishwa na waya wa HDMI na pia waya za USB ili kuunganisha vifaa vingine kama Camera za mkononi badala ya kusubiri kuhamishia kwenye computer.

  Pia format yoyoye ile inaweza kutumiak iwe MKV, MP4, XVID, AVI, WMV, na MOV na unaweza kukiunganisha na home wireless network kwa kutumia protocal ya 802.11n, unaweza ku-play content moja kwa moja kutoka kwenye internet kwenye sehemu kama Spotify, Youtube na Facebook.

  Kwa habari mpya kwenye website zinaonyeshwa kwenye dashboard kwa kutumia ujazo wa RSS na pia unaweza kucheza games ukiwa mtandaoni mwa internet.

  Maonyesho hayo yatafanyikia kwenye maholi namba 7 hadi 12 ndani ya kituo cha maonyesho kiitwacho National Exhibition Centre na ukitumia GPS Post Code ni B40 1NT.

  Haya wale wapenzi wa technology karibuni katika maonyesho haya.
   
 2. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #2

 3. P

  Pazi JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 2,918
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
  Mr Richard Ratiba yangu ikienda Vizuri Pengine nitakuwepo hapo "NEC"
   
Loading...