vitu vingine bhana tz walipigana vita sababu ipo wazi kabisa kuwa nduli alilimega eneo la tz akidai ni lake au ilikuwa ni UONGO
Achana na historia za shuleni ambazo zimejaa uongo mwingi! Ingawaje ni kweli pale ambapo tulifikikia ilikuwa ni lazima tuingie vitani lakini jiulize tulifikaje fikaje pale!!
Kila mtu anafahamu Idd Amin alikuwa mwendawazimu lakini uendawazimu wake kwa Tanzania ulianza rasmi baada ya sisi wenyewe kuanza kumchokonoa!
REMEMBER, baada ya Idd Amin kumpindua Obotte ambae alikuwa Swahibu mkubwa wa Mwalimu, Dr. Obotte akakimbilia Tanzania na sisi kumpa hifadhi!
Hapakuwa na ubaya wowote kwa Mwalimu kumpa hifadhi Obotte!
Baada ya wafuasi wa Obotte kusikia mtu wao ameruka na ndege toka Singapore hadi Dar es salaam na kuchukua hifadhi, nao kwa mamia kama sio maelefu wakavuka mpaka kutoka Uganda hadi Tanzania. Na wenyewe tukawapa hifadhi!
Hadi hapo, Mwalimu hakufanya kosa kuwapa wafuasi wa Obotte hifadhi Tanzania!
Alipokuja kulikoroga Mwalimu, wafuasi wale wa Obotte wakapelekwa kambi ya JKT, Handeni Tanga! Huko wakawa wanachukua mafunzo ya kijeshi ili warudi Uganda kumpindua Idd Amini... hii ilikuwa ni covert operation!
Na kweli, mwaka 1971 wafuasi wa Obotte wakavuka mpaka kutoka Tanzania na kurudi Uganda kufanya jaribio la kumuondoa Amin madarakani! Sijui walikosea wapi manake walifyekwa vibaya mno... wakakimbia kurudi Tanzania! Na tangu hapo ule uendawazimu wa Amin ndo ukahamia rasmi Tanzania!!!
Now tell me... wewe ungekuwa ndo Idd Amin ungevumilia uchokozi kama huo?! Tanzania tulikuwa na sababu zipi za msingi za kutaka kumrudisha Dr. Obotte madarakani, tena kwa mtutu wa bunduki?!