Gabriel Mwita wa CHADEMA unataka Nini?

Gabriel Mwita wa CHADEMA unataka Nini?

sasa gentleman,
nadhani wew ndio unatumia usaliti vibaya kwa kumsingizia msema ukweli mwita, hali ya kua wasaliti wabobevu tena wenye laana kama mzee slaa ndio wanaonekana watu safi wenye roho safi kama pamba right ndani ya Chadema?🐒

Acha kumlinganisha Dr Slaa na huyo mchumia tumbo. Dr Slaa aliomba msamaha na chama kimemrudisha. Pia Dr Slaa ni Asset.
 
no reform no elections ni null and void agenda ya kitapeli ya Yahaya gentleman 🐒

Mama anataka reforms ndio maana akaja na 4Rs. Sasa CHADEMA wanamsaidia kwamba apeleke reforms kwenye mfumo wa uchaguzi anakataa.
 
reforms zilishafanyika ndio maana Lisu na watangaza nia wa Chadema wengine watashiriki kikamilifu uchaguzi wa October mwaka huu gentleman 🐒

Reforms za kubadilisha jina la Tume na mabadiliko ambayo yanaisaidia CCM ?. Tufanye reforms za maana ili tuendeshe uchaguzi usiokiwa na matatizo.
 
..Bakwata kupitia Katiba Mtendaji Alhaj Mruma wamesema kunahitajika reforms zaidi.

..Shura ya Maimamu kupitia Shekhe Ponda wameitaka serikali kufanya reforms zaidi.

..Ndugu zangu acheni kushupaza shingo.

Kweli kabisa, Reforms zinahitajika.
 
Gabriel Mwita haogopi uchaguzi.CHADEMA ili mpate dola lazima mshiriki uchaguzi na kuchaguliwa.Ni chama mfu tu kinachoogopa uchaguzi kwa visingizio vya kitoto
Kwani, kama lengo lake ni ubunge mbona akihamia CCM anaweza kupata tu! Kwani lazima awe Chadema? Siyo pandikizi kweli huyu?
 
Reforms za kubadilisha jina la Tume na mabadiliko ambayo yanaisaidia CCM ?. Tufanye reforms za maana ili tuendeshe uchaguzi usiokiwa na matatizo.
Gentleman,
reforms unazotaka wewe binafsi fanya kwenye familia na kwenye katiba ya chama chako sio kusumbua wengine 🐒
 
Gabriel Mwita haogopi uchaguzi.CHADEMA ili mpate dola lazima mshiriki uchaguzi na kuchaguliwa.Ni chama mfu tu kinachoogopa uchaguzi kwa visingizio vya kitoto
ulikulia na kujifunzia kiswahili wapi mkuu.? ni wapi chademe walikwambia wanagomea uchaguzi? ina maana vikao halali vya chama vilivyoamua NO REFORMS huko nyuma chini ya Mbowe vilikuwa vinatishia nyau? hawa wakina mwita walikuwa wapi siku zote?
 
Mama anataka reforms ndio maana akaja na 4Rs. Sasa CHADEMA wanamsaidia kwamba apeleke reforms kwenye mfumo wa uchaguzi anakataa.
tulisha toka huko gentleman, huenda waliosusia kikosi kazi cha reforms ndio wanastuka kutoka usingizini hivi sasa 🤣
 
huyo muungwana,
ni miongoni mwa wanachadema waandamizi wenye ushawishi mkubwa zaidi ndani ya Chadema aliefanikisha no reform no elections kupuuzwa kabisa miongoni mwa wanachadema hususan watangaza nia za kugombea urais,ubunge na udiwani.

Infact ,
ndie aliemlazimisha hata Lisu kutangazwa kua miongoni mwa wanachadema waandamizi waliotangaza nia za kugombea urais Uchaguzi mkuu wa October,

na kuifanya useless no reform no elections kua completely nonsense, null and void kuanzia sasa kuelekea Uchaguzi mkuu 🐒
Chawa wa CCM mambo ya CHADEMAyanakuhusu nini ?Msengerema wewe
 
Acha kumlinganisha Dr Slaa na huyo mchumia tumbo. Dr Slaa aliomba msamaha na chama kimemrudisha. Pia Dr Slaa ni Asset.
aliomba msamaha upi gentleman huyo Mzee,
wa kupora wake za watu, kuikana familia yake, kusaliti chama au kudokoa pesa za kanisa?

na aliomba lini hivyo?🐒
 
Kwenye vyama vya siasa kuna wasaliti/usalama wa kufanya au kutoa kauli zinazo kingana na chama chao. Hawa wasaliti wapo kila kona ya kazi na jumuiya ili kuleta kauli tata ya kuwa changanya watu wenye msimamo mmoja na kuwatoa kwenye huo msimamo.
Kwa Chadema ya hivi sasa trust me anaangaliwa Lissu na Heche Tu. Labda kidogo na Lema. Hao ndio wenye ushawishi kwa wanachama wote nchi nzima na ndio wenye kuweza kubadili upepo. Waliobaki wote ni useless, barking dogs, hawana nguvu wala ushawishi master.
 
No reforms No election. Full stop
Sasa watu wanatangaza nia za kugombea urais na ubunge ili iweje? Tatizo lenu wafuasi wa chadema mnafanya mambo kwa kukariri: mnaimba tu No reform No election, wakati lisu anayewakaririsha yeye anatangaza nia ya kugombea urais. Wewe huoni kuna walakini hapo?
 
Gabriel Mwita wa CHADEMA unataka Nini?

Nina swali moja Kwa huyu kada wa CHADEMA Gabriel Mwita , Je Gabriel Mwita unataka Nini?.

Kwanza, nakuuliza Gabriel Mwita unataka nini kwa sababu maamuzi ya kupitishwa kwa tamko la no reforms no election yalifanywa na vikao vyote halali vya Chama. Kuanzia Kamati kuu, Baraza Kuu na hatimaye Mkutano Mkuu wa Chama. Leo mnataka Chama kubadilisha maamuzi yake kisa wanachama 55 wanataka kugombea ubunge na udiwani?. Yani shida yako ni kugombea ubunge bila kuangalia mapungufu ya kwenye mfumo wetu wa uchaguzi. Haya bwana.

pili, nakuuliza Gabriel Mwita unataka nini kwa sababu uligombea ubunge Musoma mjini mwaka 2020 na unajua ulichofanyiwa kwenye ule uchaguzi ukaanguka. Ikumbukwe Musoma mjini ndio Jimbo pekee Tanzania Bara ambapo Rais Magufuli alipata kura chache zaidi kuliko majimbo mengine yani asilimia 55 tu ya kura na hapo ni baada ya kuiba Sana.

Wewe mwenyewe Gabriel ulilalamika kuchezewa faulo na CCM, lakini leo nashangaa unataka kugombea ubunge kwenye mazingira yale yale. Najiuliza shida ni nini?. Ni kweli unataka kugombea ubunge au una jambo lako mwenyewe moyoni baada ya kuwekwa pembeni na chama? Maana watu wanakupigania upate nafasi nzuri ya kushiriki uchaguzi katika mazingira bora yenye haki ila wewe una wakebehi na kuwaona hawafai.
Haya bwana.

Tatu, nakuuliza wewe Gabriel Mwita unataka nini maana mwaka 2024 kulikuwa na shinikizo la CHADEMA kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, ila baadae Kamati Kuu chini ya Mh Mbowe ikapitisha azimio la kushiriki uchaguzi ule. Wewe mwenyewe ni shahidi kwa yaliyotokea, sina haja ya kuongea maana yalikuwa wazi. Je mnataka turudi huko?

Na nikuambie tu mkishiriki uchaguzi huu, dola itawabamiza hakuna na hakuna atakayewaonea huruma mkisiginwa na dola maana mnashiriki uchaguzi huku mkijua matokeo yake ni yepi. Sasa hiyo ni akili au matope? Unaenda kushiriki uchaguzi ambao unajua kushinda ni ndoto kutokana na mazingira mabovu.Kama unashiriki uchaguzi ilimradi ushiriki na sio kushinda kazi kwako bwana Gabriel Mwita.

Mwisho naomba nikushauri mambo matau yafuatayo Ndugu Gabriel Mwita:

1. Kama unataka kukijenga chama na kuwa kiongozi mkubwa wa chama huko mbeleni, Jenga tabia ya kuheshimu vikao vya chama. Vikao vyote halali vimekubali chama kisishiriki uchaguzi mkuu kama hakuna mabadiliko kwenye madhaifu yaliyopo kwenye sheria na mfumo wa uchaguzi Tanzania. Inakuaje leo unalazimisha chama kubadilisha mwelekeo ghafla baada ya Mkutano Mkuu kuridhia?. Huo ni utovu wa nidhamu na kiburi.

2. Kama unataka kugombea ubunge na unaona una ushawishi wa kushinda , tafuta chama kinachokubalika hata CCM , NCCR kagombee, maana kugombea ni haki yako siyo lazima iwe CHADEMA. Kuendelea kulazimisha unataka ugombeee kupitia CHADEMA huku ukijua kwa Sasa chama kinapambania mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi inaonesha wewe una lako jambo kama sio kirusi ndani ya chama.

3. Kama unaona Chama kilifanya maamuzi yasiyo sahihi , nafasi uliyonayo ni kuomba mkutako mkuu wa dharura kupitia njia ya kikatiba ambapo Jambo lako litajadiliwa na likionekana ni la msingi chama kitabadilsha msimamo na kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Soma Pia: CHADEMA yamng'oa Katibu wa Sekretarieti wa chama, Julius Mwita baada ya kuibuka mzozano kwenye kundi sogozi

kwa kukuaga tu, nakushauri ya kwamba usiongee yote ukamaliza maana kwenye siasa hujui litatokea nini kesho. Leo waweza kuona sifa kwa kumshambulia Mh. Lissu ila kesho mamlaka yaweza kukubaliana na hoja za Lissu na kukaa meza moja kubadilisha mfumo wote wa uchaguzi, mtafanyaje?

Kesho nitajibu hoja zako zote ulizitoa kwenye press ya leo.
Asante
1. Wameahidiwa fedha za kampeni na za chakula za familia zao na Samia Suluhu Hassan, ambazo actually ni mapesa ya waarabu wa Dubai na Oman kwa gharama ya rasrimali zetu Watanganyika (bandari zetu, misitu yetu, mbuga zetu za wanyama, madini yetu, gesi yetu). Ahadi zimewapagawisha baadhi ya viongozi na vijana wa CHADEMA kuliko kawaida mpaka wametupa akili zao pembeni na kuamua kuwa wajinga kabisa...!!

2. Wengine wameahidiwa kuachiwa baadhi ya majimbo ya ubunge wengine udiwani nk (kwenye u-Rais huko hapana, ni mali ya CCM hiyo). Sasa wanaona uongozi mpya na kaulimbiu ya NO REFORMS NO ELECTION inakwenda kuharibu na kuwakosesha ulaji wao huu wa bure toka CCM....

## Kwa kifupi ni kuwa ishu wala si kugombea na kwenda kushinda. Ishu hapa ni kupambana ili maokoto haramu yanayonuka damu za watu yasije kuwapita

3. Hayo ☝🏻☝🏻ni sehemu ya makubaliano ya yale maridhiano ya Samia na Mbowe Freeman...

##Nakuhakikishia jambo moja, kuwa kwa kadiri chokochoko hizi zinavyozidi kuendelea, inawezekana kabisa yakatolewa mambo mazito ambayo pengine hatuyajui....

Kwenye hilo ☝🏻Mimi sitashangaa hata kidogo kuja kujua kuwa Freeman Mbowe yupo ktk mikakati hii miovu ya kuhujumu chama ambacho kwa nguvu na jacho lake amekijenga kwa miaka 30....!!

Muda ni hakimu mzuri. Hakika utasema...
 
Sasa watu wanatangaza nia za kugombea urais na ubunge ili iweje? Tatizo lenu wafuasi wa chadema mnafanya mambo kwa kukariri: mnaimba tu No reform No election, wakati lisu anayewakaririsha yeye anatangaza nia ya kugombea urais. Wewe huoni kuna walakini hapo?
You're missing a point...

Hakuna anayesusia uchaguzi bro...!

Nia zipo, kugombea tutagombea na kwa hakika tutawashinda CCM kwa zaidi ya 90% under one condition: REFORMS kwanza za mfumo mzima wa kikatiba na kisheria wa chaguzi zetu zote ili wote tuwe tunaingia kucheza ktk uwanja ulio sawa kwa wote..!!

Na kwa hiyo kutangaza nia au dhamira wala sio shida na sio kosa. Kila mtu atangaze na ajiandae kwa hakika kwa sababu uchaguzi ni lazima utafanyika tu...

Unalotakiwa kuzingatia ni hili👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

Kwamba, it doesn't matter ni mwaka huu 2025 au tutasogeza mbele uchaguzi ili kwanza tushughulike na REFORMS za kikatiba na kisheria ili kuutengeneza huo uwanja sawa na wa haki wa kushindanisha sera ktk chaguzi zetu. Na baada ya hapa hawa kina Emmanuel Mwita wataingia kwenye uchaguzi. Kwa sasa let's fight for changes first...

That's ☝🏻☝🏻☝🏻the point you're missing bro...

Is it so difficult to understand that ndugu UmkhontoweSizwe ?
 
Back
Top Bottom