Gabon kuanzisha mafunzo ya Kiswahili mashuleni

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
Tanzania imeombwa kuisaidia Gabon kubuni, kuanzisha na kusimamia mitaala inayofaa kuanzisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika shule za nchi hiyo kutokana na uamuzi wa Serikali ya Gabon kuanza kufundisha lugha hiyo tangu elimu ya msingi. Aidha, Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba amemwomba binafsi Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kusaidia kumpatia mwalimu binafsi wa kumfundisha lugha ya Kiswahili ikiwa ni jitihada zake za kuonesha mfano wa kuimarisha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili kwa wananchi wake.
Gabon inakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kukumbatia na kuamua kufundisha Kiswahili shuleni nje ya nchi za Jumuiya ya Mashariki za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda hata kama lugha ya Kiswahili inazungumzwa na mamilioni ya watu nje ya eneo la Jumuiya hiyo ndani na nje ya Afrika.

Kwa hisani ya Radio Tehran, Iran
 
Kwa kweli ni lugha adhimu sana lakini watu wengi wanaikitumia hawalijui hilo.
 
huyo aliyeombwa kupeleka mwalimu binafsi yeye mwenyewe kiswahili chake hakijanyooko sentensi mbili katikati kiingeleza
 
Nilipoion hii habar kwenye wall ya radio iran nikashangaa sana ina maana rais alipoombwa hakukua na waandish wa habar??????maana hakuna hata redio 1 au gazeti 1 lililoripoti,then nikajiuliza anaetaka aende wapi???????mi nataka niombe,nina shahada ya ualim,kisw na history
 
Ni hatua nzuri japo majirani zetu wa Uganda hawakipi kiswahili kipaumblele kabisa
 
Back
Top Bottom