mbunge mteule wa jimbo la hai, mheshimiwa kaka yetu wa ukweli freeman aikaeli mbowe ametangazwa rasmi kushinda ubunge kwa tiketi ya chadema.
Hapa hai mjini ni shamrashamra za hali ya juu na umati ni mkubwa mno. Wananchi walisubiri kwa hamu toka asubuhi kutangazwa mshindi kwani wakala wa mgombea wa ccm alitaka matokeo ya kata mojawapo yarudiwe kuhesabiwa mara tatu ila hali haikubadilika.
Katika hali isiyo ya kawaida mbunge anayemaliza muda wake hajakubali kusaini matokeo hayo yaliyombwaga kwa aibu.
Hapa matokeo yalikuwa wazi toka jana jioni kwani mawakala wa chadema (nikiwemo) walikutana na kujumlisha matokeo ya vituo vyote na kuonesha hata angepewa kura 5000,mgombea wa ccm asingeweza kufua dafu kwa mbowe.