Elections 2010 Fuya Kimbita agoma kusaini matokeo ya ushindi wa Mbowe

Status
Not open for further replies.

Vawulence

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,928
2,101
Mbunge mteule wa jimbo la Hai, mheshimiwa kaka yetu wa ukweli Freeman Aikaeli Mbowe ametangazwa rasmi kushinda ubunge kwa tiketi ya CHADEMA.
Hapa Hai mjini ni shamrashamra za hali ya juu na umati ni mkubwa mno. Wananchi walisubiri kwa hamu toka asubuhi kutangazwa mshindi kwani wakala wa mgombea wa ccm alitaka matokeo ya kata mojawapo yarudiwe kuhesabiwa mara tatu ila hali haikubadilika.
Katika hali isiyo ya kawaida mbunge anayemaliza muda wake hajakubali kusaini matokeo hayo yaliyombwaga kwa aibu.
Hapa matokeo yalikuwa wazi toka jana jioni kwani mawakala wa CHADEMA (nikiwemo) walikutana na kujumlisha matokeo ya vituo vyote na kuonesha hata angepewa kura 5000,mgombea wa ccm asingeweza kufua dafu kwa Mbowe.
 
mbunge mteule wa jimbo la hai, mheshimiwa kaka yetu wa ukweli freeman aikaeli mbowe ametangazwa rasmi kushinda ubunge kwa tiketi ya chadema.
Hapa hai mjini ni shamrashamra za hali ya juu na umati ni mkubwa mno. Wananchi walisubiri kwa hamu toka asubuhi kutangazwa mshindi kwani wakala wa mgombea wa ccm alitaka matokeo ya kata mojawapo yarudiwe kuhesabiwa mara tatu ila hali haikubadilika.
Katika hali isiyo ya kawaida mbunge anayemaliza muda wake hajakubali kusaini matokeo hayo yaliyombwaga kwa aibu.
Hapa matokeo yalikuwa wazi toka jana jioni kwani mawakala wa chadema (nikiwemo) walikutana na kujumlisha matokeo ya vituo vyote na kuonesha hata angepewa kura 5000,mgombea wa ccm asingeweza kufua dafu kwa mbowe.

katangazwa na msimamizi wa uchaguzi au wanahai?
 
Hongera Mbowe sasa nenda kakomae kule Arusha kabla hawajachakachua
 
Am from Hai, Loooong Live my Home place, wananchi wa hai hamkuniangusha, kama mimi ambavyo sikuwaangusha hapa ubungo!
 
YEES MBOWE...!!

Nguvu ya Umma...Nguvu ya Mungu...

Yule Msimamizi feki atakuwa anaugulia yale makofi na aibu kubwa...!

Ukombozi hauhitaji mzaha....YES WE CAN!
 
Bila shaka mpaka time hizi Msimamizi wa Uchaguzi atakuwa amekwishamtangaza rasmi!
 
Good !!! kaka Mbowe mpitie Mzee Ndesa hapo town mpande Arusha fasta tuna haja sana na hilo jimbo
 
Hongera Freeman, sasa fanya hima ukomboe Kawe, Arusha na Ubungo kwa DAR ni tishio. Hakikisheni yale matokeo ya awali yaliyosainiwa jana na mawakala mnayo mkononi. Kataeni zoezi la kurudia kura.
 
mbona tunasikiliza star tv wanasema hai kwa mbowe bado hawajatangaza wanadai mpaka saa nne usiku ndio watatangaza
 
Wakuu HAI bado Mbowe hajatangazwa Rasmi...inawezekana ameshinda lakini bado wananchi wanasubiri...hii ni kwa mujibu waStar TV ambayo ipo Live sasa hivi....tuepuke jamani kutangaza habari kuonesha kuwa ni rasmi kumbe bado hazijawa rasmi ki hivyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom