Fuvu la binadamu ndani ya Ofisi ya Diamond

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
  • Fuvu la binadamu lakutwa limewekwa kwenye meza ya Diamond pembeni ya picha ya mwanawe Tifah.
  • Diamond asema ni kweli ni fuvu la binadamu, ila ni pambo tu kama mapambo mengine, yeye anamtegemea Mungu.
Diamond-2.jpg

Wakati mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii ndumba kwenye muziki wake ambao sasa umemfikisha mbali kimataifa, staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’, ameshikwa uchawi kufuatia kukutwa laivu kwa fuvu la binadamu ndani ya ofisi zake.

Fuvu hilo liko mkono wa kushoto mezani kwa Diamond huku jirani yake kukiwa na picha ya mwanaye, Latiffah Nasibu ‘Princess Tiffah’ iliyokuwa kwenye fremu.

Shuhuda mmoja aliyehudhuria hafla ya kusaini mkataba wa dili jipya alilosaini Diamond la Ubalozi wa Tomato Sauce ofisini kwake hapo alilithibitishia kuwepo kwa fuvu hilo lilozua gumzo kwa mashuhuda wachache wa tukio hilo.

“Ni kweli kuna fuvu la binadamu mezani kwa Mond (Diamond) but (lakini) sikufanikiwa kulishika kwa mikono yangu,”

Shuhuda mwingine aliripoti pia:

"Kuna ishu tumeishuhudia kwa macho yetu hapa ofisini kwa Diamond. Hata sisi imetushtua, ...hapa WCB, kwanza Diamond mwenyewe yupo. Ukifika ofisini kwake, tena kwenye meza yake (Diamond) mwenyewe kuna fuvu la binadamu kabisa.”

"Jamani ni fuvu la binadamu kabisa lenye mifupa. Inawezekana ndiyo chanzo cha utajiri wake na skendo inayomkabili ya uchawi katika kazi zake. Ninyi fuatilieni mtapata ukweli."

Mapema wiki hii, wageni mbalimbali waliofika kwenye ofisi za mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB), Diamond au Mond zilizopo Mapambano-Sinza jijini Dar, walitonya kuwa, wengi walishtushwa na fuvu hilo baada ya kuliona mezani kwa mwanamuziki huyo.

“Hata mimi nimelishuhudia hilo fuvu kwa macho yangu wala sijasimuliwa na nina picha zake kwenye simu yangu (huku akiperuzi kwenye smartphone). Kiuweli limezua sana minong’ono. Baadhi ya watu wanadai ni mambo ya uchawi na wengine wanasema ni moja ya alama ya Freemasons (jamii ya siri inayohusishwa na utajiri). Unajua fuvu la binadamu ni moja ya Alama za Freemasons na kama unavyojua Diamond amekuwa akitajwatajwa."

“Wapo wengine wanadai labda mambo hayo ndiyo chanzo cha utajiri wa jamaa (Diamond) wa
ghafla lakini yeye mwenyewe ndiye mwenye kuufahamu ukweli."

“Lakini unajua kunapokuwa na ishara kama hizi (kukutwa kwa fuvu) ni rahisi sana kwa mashabiki wake ambao ni wengi kuhusisha na huu utajiri wake unaotajwa kufikia (shilingi) bilioni nane kwa sasa,” alidai mgeni huyo.

DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya kupokea ushuhuda na madai hayo mazito ya Diamond kuhusishwa na uchawi na Freemasons kufuatia kukutwa kwa fuvu hilo ofisini kwake, gazeti hili lilimfuata Diamond ofisini kwake lakini alikuwa ametoka.

Alipotafutwa kwa njia ya simu alifunguka kwa kifupi huku akidai kuwa fuvu hilo ni pambo tu kama mapambo mengine.

“Ni urembo au pambo kama mapambo mengine, hakuna kitu kama hicho,” alisema Diamond na alipobanwa kueleza alikolitoa na gharama zake alisema:
“Usidanganyike, hakuna anayeweza kumuweka mtu juu zaidi ya Mwenyezi Mungu.

“Mimi naswali sana na namtegemea Mungu kwa kila kitu na kweli ananipigania.
“Unajua watu wengi wamekuwa wakizungumza oooh…natumia uchawi lakini ukweli ni kwamba maombi, ubunifu, juhudi na heshima ndivyo vitu vinavyoweza kumfanya mtu yeyote kupata mafanikio katika kitu akifanyacho au jambo alifanyalo.”

HUKO NYUMA
Mara kadhaa Diamond amekuwa akihusishwa na matumizi ya nguvu za giza katika kufanikiwa lakini amekuwa akisisitiza kuwa siri ya mafanikio yake ni kujituma, kutafuta fursa na kuipenda kazi yake ya muziki ili sanaa ya Bongo ifike mbali.

Source: Diamond ashikwa uchawi | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
 
Hilo sio fuvu la binadamu, hiyo ni mfano wake, mbona yapo mengi tu hayo. Hao jamaa wakikosa cha kuandika huwa wanajaribu kutunga lolote lile
 
Hii ni kesi kubwa sana aisee.

Hta kama si ushirikina lakini ni tatizo kubwa mno

Sheria za wapi hizo zinazosema ni kosa kumiliki pambo la mfano wa fuvu???

Tofautisha fuvu la binadamu na pambo la gold lenye mfano wake.. Hii kitu imekuwa ikitumika sana kwenye urembo wa cheni za kuvaa shingoni, mikanda ya kuvalia nguo (hata mimi nilitumia), n.k vyote havina tofauti na hiyo ya kuweka mezani...

Tatizo la watu wengi tumeshazoea kufeli, kiasi kwamba mtu fulani akifanikiwa basi anatumia ndumba au Freemason.. Dogo alipokuwa ulaya muda mwingine alilazimika kupiga shows 4 ndani ya wiki moja nchi 4 tofauti bado hamtaki afanikiwe? Anaandika proposal za kuomba ubalozi na anafanikisha anapiga mtonyo hapo uchawi unakuja vipi? Dogo anakesha studio kuhakikisha kesho yake iko poa bado usifanikiwe? Mtu ameajiri managers zaidi ya 4, na wafanyakazi wengine wa kutosha, jumlisha agents kwenye nchi jirani bado asifanikiwe? hahahahaha

Anayeamini mafanikio yanakuja na uchawi hana utofauti na mwanachama wa Freemason...!!!
 
Mimi sijaelewa ni fubu halisi la binadamu au ni sanamu ya fuvu la mfano wa binadamu.
Huyo kajiwekea urembo wa sanamu la fuvu la binaadamu ofisini sasa watu wamepata la kuandika. Pasi na shaka alijua kabisaaa nini kitatokea kabla kuliweka ofisini kwake. Si unajua watu wanaotaka kila uchao wawepo kwenye magazeti?
 
Lingekuwa la uchawi angeliweka live kila ataeingia alione bila ck kupita kumuongelea Simbaa hamjauza magazeti yenu basi kazi mnayo watanzania tupo nyuma sana mtu akifanikiwa tu mchawi kwa hiyo furaha kuendelea kuwa masikini badala ya kuwa na wivu wa maendeleo tuna wivu wa kudis mali za wengine hehehehe kwaheri
 
mtu kuwa na fuvu la binadamu si angekamatwa .......jaribu wewe uwe na fuvu la binadamu bhasi .... huo uongo wa mchana......
 
Kama la mjusi au Mbuzi sawa lakini binadamu ambae ana ndugu na jamaa labda Watoto ni swali la kujiuliza alikufaje? Ni nani? Hapo polisi watafuatilia tu

Huwezi kuweka fuvu la binadamu ukasema ni pambo kama mapambo mengine.

Ana moyo kuweka skull mezani, I don't buy that crap
 
DIAMOND anajua kucheza na akili za waTZ, ni yeye tu aamue kuwa kati ya wasanii matajiri Afrika. kama kila kitu chake ni habari kwanini akose ubalozi,show,kuuza,kushika chati za juu, DIAMOND fulsa hiyo itumie vizuri.
 
Back
Top Bottom