Nakumbuka nilipokuwa kijana mdogo kule kwetu tulikuwa na waislamu wachache lakini wakarimu sana,enzi hizo hizo watu walikuwa wanafuturu hadharani ukifika muda wa kufuturu ,jamvi lilitandikwa nje na yoyote aliyekuwa anapita maeneo ya makazi hayo hata asie muislamu alikaribishwa bila kuulizwa hata dini yake,maadamu ni mwanadamu unapita basi ilikuwa ni karibu,tena karibu ya moyoni na si ya kiswahili,enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya ''kuuza futari''barabarani au mahotelini ,wakati huo ilikuwa ni thawabu kubwa kumkaribisha mpita njia kufuturu kwenye mkeka barazani nje,siku hizi mambo yamebadilika futari ni sebuleni na kwa wanaojuana tu.