Fursa za kibiashara zipatikanazo Comoro

Fursa za kibiashara zipatikanazo Comoro

Safi saana balozi Kwa muongozo huu, mabalozi wengine wanapaswa kuiga, balozi utadhani mchumi vile
 
Nasikia kwa matapeli ni balaa hila kwa biashara ni kuzuri sana
 
Safi sana ndugu balozi, jiwe hakukosea kukuweka huko..na mabalozi wengine wajitokeze waseme neno!
 
Sure mkuu tungekua na mabalozi wengine wanaoweza kuonesha fursa mbalimbali za biashara tungekua mbali.Fikiria Balozi alienda kuwapa pole wafanyabiashara ambao mifugo yao ilikufa,hakika kwa hili anafaa kupongezwa
Kwa nin hao wafanyabiashara wetu wasipeleke nyama iliyotayari ? Hata wanasafirisha mifugo had inawafia?
 
Nadhani Changamoto itakuwa uwepo wa kontena zenye friji kuhakikisha nyama hairibiki

Hili ni tatizo lkn ni fursa mkuu kwahiyo Kama unaweza kupata kontena za namna hiyo ukawapa hili wazo wanao safirisha ng'ombe na ukaanza kuwakodisha hizo kontena utakuwa umekuwa mjasiriamali original maana utakuwa umetatua tatizo huku unapata kipato
 
Ngoja nijipange nikafanye business tour nione physical opportunities.
 
Safi sana ndugu balozi, jiwe hakukosea kukuweka huko..na mabalozi wengine wajitokeze waseme neno!

Wako wapi mabalozi wengine? kama mabalozi wetu wote wa nchi zote wangekuwa wanatuambia fursa zilizopo na information sahihi kwenye nchi wanazotuwakilisha ingependeza sana.
 
Muwe na tafakuri kidogo ni kweli fursa zipo tena nyingi tu.. Ila pia risk ni kubwa hasa kwenye miundombinu... Comoro inafikika kwa njia mbili tu majini na angani
 
Mshana unaweza kuwa na ufahamu wa kiasi cha nauli tokea bongo kwa ndege na meli pia?
 
Hakuzungumzia chochote kuhusu construction industry?
Habari wakuu,

Juzi asubuhi Jumamosi tarehe 26/05/2018 nilikua naangalia kipindi cha Clouds 360 on Saturday kinachoendeshwa na Siza na Gibson George.Mheshimiwa balozi wa Tanzania Comoro Mheshimiwa Sylvester Massele Mabumba alikua anazidadavua fursa kedekede zilizopo nchini Comoro.Kiufupi Comoro kuna fursa nyingi kwa mujibu wa mhe. Balozi na akawataka Watanzania wenye nguvu kiuchumi na wafanyabiashara wadogo kuwekeza na kufanya biashara huko.Kwa uchache fursa zenyewe ni kama zifuatazo;

1.Biashara ya chakula na vinywaji

Mheshimiwa balozi anasema asilimia kubwa ya vyakula inatoka kwetu, mchele, nyama ya ngo,mbe na mbuzi, mbogamboga na matunda nk, alitolea mfano papai la kawaida tu kwa Moroni linauza Tsh 7,000.Bado viungo mbalimbali kama iliki na karafuu bado vina soko kubwa.Vinywaji kama maji ya kunywa na juice pia zinatoka Tanzania.

2.Biashara ya Gereji /ufundi magari

Mheshimiwa Balozi anasema hakuna gereji Moroni zaidi ya kukuta magari yanatengenezewa tu mtaani na sio gereji kama tulizokua nazo Bongo.Kwa mafundi wa Tanzania hii ni fursa kama mtu ataenda kufungua gereji maana atakua kiproffessional zaidi hivyo kuaminika kibiashara.

3.Biashara ya bima

Hii ni biashara kwaajili ya waTanzania wanaofanya biashara Comoro na kwa Wacomoro wenyewe.Alitolea mfano namna wafanyabiashara wa Tanzania walivyopoteza ngombe na mbuzi ambao walikufa wakiwa baharini hivyo kupata hasara hivyo akawaasa wafanyabiashara kufungua insurance agencies maana wateja wapo.

4.Biashara ya Hoteli

Kwa wale wenye mitaji mikubwa ni fursa adhimu sana kwao na hakuna urasimu ndani ya siku moja unakamilisha usajili.Balozi anasema kuna hoteli kubwa moja five star na inamilikiwa na waTanzania

5.Fursa ya kufundisha Kiswahili na Kiingereza

Mheshimiwa balozi anasema Comoro wanahitaji sana waalimu haswa wa Kiswahili na akatolea mfano waTanzania wawili anaowafahamu ambao wanafundisha Kiswahili mjini Moron

6.Biashara ya usafirishaji

Hapa mheshimiwa balozi alitoa wito kwa wafanya biashara wakubwa kuanzisha safari za meli kutoka Tanzania mpaka Moron.Alitolea mfano kulikua na meli moja tu kutoka Zanzibar kwenda Comoro but ilikua haifiki Moron kabisa sababu ya kina Kidogo akatoa wito kwa wenye meli za wastani zifanye safari mpaka Moroni, pia meli ndogo kwaajili ya kusafirisha abiria ndani ya Comoro

Pia usafiri wa anga kuna fursa kubwa haswa hivi vi fly charter ni biashara kubwa sana

7.Biashara ya nishati ya umeme

Hapa ni kwa Serikali, Mheshimiwa balozi anasema kuwa Comoro wanatumia umeme wa jenereta. Grid yao ya taifa ni umeme unaozalishwa kwa jenereta hivyo si umeme wa uhakika.Tanzania inaweza ikazalisha umeme wa gas kisha ikawauzia Wacomoro.

Kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza wakafanya biashara ya majenereta na vifaa vyake kwa wingi.

8.Biashara ya magogo na mbao

Hii ni fursa kubwa sana kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwani Comoro kuna uhaba mkubwa sana wa mbao na magogo kwaajili ya kuchania mbao.Hivyo kama mtu atapeleka magogo huko maana yako hata mashine za kuchania Mbao bado ni deal.Kwa mujibu wa balozi anasema Comoro miti ya mbao ni michache sana hivyo wa Bongo wachangamkie fursa.

9.Biashara ya furnitures

Comoro wanategemea sana furniture kutokea Tanzania sofa, meza, nk so kwa Watanzania ambao ni mafundi sofa au wenye viwanda vya furniture wanaweza kuchangamkia hii fursa.Pia mafundi sofa na mafundi serelemala wa furniture wanaweza wakaji organise kisha wakafungua kiworkshop chao wakapiga hela nzuri tu.

10.Biashara ya Vanilla

Mheshimiwa Balozi anasema Comoro ni mzalishaji mkubwa sana wa vanilla duniani.Comoro vanilla kwao ni kama dhahabu na inabei kubwa wastani wa USD 500 kwa KG.Wakati wakulima wetu Bukoba na sehemu zingine Vanilla haifiki hata TSH 200,000 kwa KG.Hivyo basi mtu anaweza akanunua Vanilla Bongo kwa bei ya chini sana na akaenda kuiuza Comoro kwa bei ya juu sana.

11.Biashara ya screpa na spare za magari

Mheshimiwa baloz anasema magari mabovu ni mengi sana Comoro hii inatokana na wao kutokua na gereji za kisasa na mafundi wa kutosha.Hivyo basi unaweza ukapeleka spare za magari Comoro na unaporudi zako Bongo unarudi na spare used na screpa hivyo ukapiga hela double double.

Niishie hapa kwa leo ila balozi alisisitiza sana waTanzania watumie fursa hii maana Tanzania tuliwasaidia sana Comoro kupata uhuru wao pia hata mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea 2008 Tanzania ilisaidia sana Rais wa Comoro kurudishwa madarakan maana wanajeshi wetu walitumika kuzima mapinduzi hayo.
 
Mmh mara ya mwisho kwa ndege ilikuwa $350 miaka 5 nyuma na kwa jahazi ilikuwa 35-45 elfu... But very risk
 
Mpaka sasa hiyo ndio nauli ya ndege...ni ghali sana...Kama unaenda Dubai vile. Ila kwa kuwa unaenda kutafuta business connections, basi si vibaya ukafumba macho na kwenda kuangalia fursa hizo.
 
Hakuzungumzia chochote kuhusu construction industry?
Construction ipo mkuu nilivyoviandika hapa siku note sehem yoyote hivyo nliandika vile nilivyovikumbuka tu
 
Habari wakuu,

Juzi asubuhi Jumamosi tarehe 26/05/2018 nilikua naangalia kipindi cha Clouds 360 on Saturday kinachoendeshwa na Siza na Gibson George.Mheshimiwa balozi wa Tanzania Comoro Mheshimiwa Sylvester Massele Mabumba alikua anazidadavua fursa kedekede zilizopo nchini Comoro.Kiufupi Comoro kuna fursa nyingi kwa mujibu wa mhe. Balozi na akawataka Watanzania wenye nguvu kiuchumi na wafanyabiashara wadogo kuwekeza na kufanya biashara huko.Kwa uchache fursa zenyewe ni kama zifuatazo;

1.Biashara ya chakula na vinywaji

Mheshimiwa balozi anasema asilimia kubwa ya vyakula inatoka kwetu, mchele, nyama ya ngo,mbe na mbuzi, mbogamboga na matunda nk, alitolea mfano papai la kawaida tu kwa Moroni linauza Tsh 7,000.Bado viungo mbalimbali kama iliki na karafuu bado vina soko kubwa.Vinywaji kama maji ya kunywa na juice pia zinatoka Tanzania.

2.Biashara ya Gereji /ufundi magari

Mheshimiwa Balozi anasema hakuna gereji Moroni zaidi ya kukuta magari yanatengenezewa tu mtaani na sio gereji kama tulizokua nazo Bongo.Kwa mafundi wa Tanzania hii ni fursa kama mtu ataenda kufungua gereji maana atakua kiproffessional zaidi hivyo kuaminika kibiashara.

3.Biashara ya bima

Hii ni biashara kwaajili ya waTanzania wanaofanya biashara Comoro na kwa Wacomoro wenyewe.Alitolea mfano namna wafanyabiashara wa Tanzania walivyopoteza ngombe na mbuzi ambao walikufa wakiwa baharini hivyo kupata hasara hivyo akawaasa wafanyabiashara kufungua insurance agencies maana wateja wapo.

4.Biashara ya Hoteli

Kwa wale wenye mitaji mikubwa ni fursa adhimu sana kwao na hakuna urasimu ndani ya siku moja unakamilisha usajili.Balozi anasema kuna hoteli kubwa moja five star na inamilikiwa na waTanzania

5.Fursa ya kufundisha Kiswahili na Kiingereza

Mheshimiwa balozi anasema Comoro wanahitaji sana waalimu haswa wa Kiswahili na akatolea mfano waTanzania wawili anaowafahamu ambao wanafundisha Kiswahili mjini Moron

6.Biashara ya usafirishaji

Hapa mheshimiwa balozi alitoa wito kwa wafanya biashara wakubwa kuanzisha safari za meli kutoka Tanzania mpaka Moron.Alitolea mfano kulikua na meli moja tu kutoka Zanzibar kwenda Comoro but ilikua haifiki Moron kabisa sababu ya kina Kidogo akatoa wito kwa wenye meli za wastani zifanye safari mpaka Moroni, pia meli ndogo kwaajili ya kusafirisha abiria ndani ya Comoro

Pia usafiri wa anga kuna fursa kubwa haswa hivi vi fly charter ni biashara kubwa sana

7.Biashara ya nishati ya umeme

Hapa ni kwa Serikali, Mheshimiwa balozi anasema kuwa Comoro wanatumia umeme wa jenereta. Grid yao ya taifa ni umeme unaozalishwa kwa jenereta hivyo si umeme wa uhakika.Tanzania inaweza ikazalisha umeme wa gas kisha ikawauzia Wacomoro.

Kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza wakafanya biashara ya majenereta na vifaa vyake kwa wingi.

8.Biashara ya magogo na mbao

Hii ni fursa kubwa sana kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwani Comoro kuna uhaba mkubwa sana wa mbao na magogo kwaajili ya kuchania mbao.Hivyo kama mtu atapeleka magogo huko maana yako hata mashine za kuchania Mbao bado ni deal.Kwa mujibu wa balozi anasema Comoro miti ya mbao ni michache sana hivyo wa Bongo wachangamkie fursa.

9.Biashara ya furnitures

Comoro wanategemea sana furniture kutokea Tanzania sofa, meza, nk so kwa Watanzania ambao ni mafundi sofa au wenye viwanda vya furniture wanaweza kuchangamkia hii fursa.Pia mafundi sofa na mafundi serelemala wa furniture wanaweza wakaji organise kisha wakafungua kiworkshop chao wakapiga hela nzuri tu.

10.Biashara ya Vanilla

Mheshimiwa Balozi anasema Comoro ni mzalishaji mkubwa sana wa vanilla duniani.Comoro vanilla kwao ni kama dhahabu na inabei kubwa wastani wa USD 500 kwa KG.Wakati wakulima wetu Bukoba na sehemu zingine Vanilla haifiki hata TSH 200,000 kwa KG.Hivyo basi mtu anaweza akanunua Vanilla Bongo kwa bei ya chini sana na akaenda kuiuza Comoro kwa bei ya juu sana.

11.Biashara ya screpa na spare za magari

Mheshimiwa baloz anasema magari mabovu ni mengi sana Comoro hii inatokana na wao kutokua na gereji za kisasa na mafundi wa kutosha.Hivyo basi unaweza ukapeleka spare za magari Comoro na unaporudi zako Bongo unarudi na spare used na screpa hivyo ukapiga hela double double.

Niishie hapa kwa leo ila balozi alisisitiza sana waTanzania watumie fursa hii maana Tanzania tuliwasaidia sana Comoro kupata uhuru wao pia hata mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea 2008 Tanzania ilisaidia sana Rais wa Comoro kurudishwa madarakan maana wanajeshi wetu walitumika kuzima mapinduzi hayo.
Hayo wanayasema tu kwenye vyombo vya habari ila ukiritimba uliopo hapo bandarini kwenye kusafirisha mizigo ni balaa!kuna jamaa namfahamu alikuwa na contena 6 za maharage na asali!!amehangaikia vibali hapo kila mtu anamwambia nenda kwa yule hadi anafanikiwa kupata hivyo vibali anafikisha huko maharagwe yameshakuwa unga tu yameharibika alichoambulia ni asali tu!!alipata hasara ya karibia milioni 80!!usifikilie hizo fulsa watu hawazioni ila urasimu uliopo kwenye ofisi husika za kutoa vibali mala Tfda,tbc kila mtu ana mtupia mpira mwenzake!!tunakwamishana wenyewe kwa wenyewe!!ndio maana huwa nikimsikia kiongozi anasema hivyo huwa "NAMCHEKIIII,kisha nasemaa yaaan!!!!!halafu kufanya biashara ya nje hususani mazao ni ngumu kwani haitabiriki unachukua order ya mtu unaanza kukusanya mzigo malaa paa serikali imepiga marufuku usafirishaji wa mazao kwenda nje!!kuanzia sasa!!hawatoi hata muda ili kama kuna watu wana mizigo yao wamalizie kwanza!!mimi kuna mwaka yalinikuta acha tu yasikie kwa mwenzako ila nashukuru mwenye mzigo alinielewa,ndio maana wafanyabiashara wengi hasa wa Rwanda na Drc wamekuwa waoga kufanya biashara za kununua mazao nchini!!
 
Back
Top Bottom