Fursa za kibiashara zipatikanazo Comoro

kabwigwa

JF-Expert Member
May 17, 2014
933
1,533
Habari wakuu,

Juzi asubuhi Jumamosi tarehe 26/05/2018 nilikua naangalia kipindi cha Clouds 360 on Saturday kinachoendeshwa na Siza na Gibson George.Mheshimiwa balozi wa Tanzania Comoro Mheshimiwa Sylvester Massele Mabumba alikua anazidadavua fursa kedekede zilizopo nchini Comoro.Kiufupi Comoro kuna fursa nyingi kwa mujibu wa mhe. Balozi na akawataka Watanzania wenye nguvu kiuchumi na wafanyabiashara wadogo kuwekeza na kufanya biashara huko.Kwa uchache fursa zenyewe ni kama zifuatazo;

1.Biashara ya chakula na vinywaji

Mheshimiwa balozi anasema asilimia kubwa ya vyakula inatoka kwetu, mchele, nyama ya ngo,mbe na mbuzi, mbogamboga na matunda nk, alitolea mfano papai la kawaida tu kwa Moroni linauza Tsh 7,000.Bado viungo mbalimbali kama iliki na karafuu bado vina soko kubwa.Vinywaji kama maji ya kunywa na juice pia zinatoka Tanzania.

2.Biashara ya Gereji /ufundi magari

Mheshimiwa Balozi anasema hakuna gereji Moroni zaidi ya kukuta magari yanatengenezewa tu mtaani na sio gereji kama tulizokua nazo Bongo.Kwa mafundi wa Tanzania hii ni fursa kama mtu ataenda kufungua gereji maana atakua kiproffessional zaidi hivyo kuaminika kibiashara.

3.Biashara ya bima

Hii ni biashara kwaajili ya waTanzania wanaofanya biashara Comoro na kwa Wacomoro wenyewe.Alitolea mfano namna wafanyabiashara wa Tanzania walivyopoteza ngombe na mbuzi ambao walikufa wakiwa baharini hivyo kupata hasara hivyo akawaasa wafanyabiashara kufungua insurance agencies maana wateja wapo.

4.Biashara ya Hoteli

Kwa wale wenye mitaji mikubwa ni fursa adhimu sana kwao na hakuna urasimu ndani ya siku moja unakamilisha usajili.Balozi anasema kuna hoteli kubwa moja five star na inamilikiwa na waTanzania

5.Fursa ya kufundisha Kiswahili na Kiingereza

Mheshimiwa balozi anasema Comoro wanahitaji sana waalimu haswa wa Kiswahili na akatolea mfano waTanzania wawili anaowafahamu ambao wanafundisha Kiswahili mjini Moron

6.Biashara ya usafirishaji

Hapa mheshimiwa balozi alitoa wito kwa wafanya biashara wakubwa kuanzisha safari za meli kutoka Tanzania mpaka Moron.Alitolea mfano kulikua na meli moja tu kutoka Zanzibar kwenda Comoro but ilikua haifiki Moron kabisa sababu ya kina Kidogo akatoa wito kwa wenye meli za wastani zifanye safari mpaka Moroni, pia meli ndogo kwaajili ya kusafirisha abiria ndani ya Comoro

Pia usafiri wa anga kuna fursa kubwa haswa hivi vi fly charter ni biashara kubwa sana

7.Biashara ya nishati ya umeme

Hapa ni kwa Serikali, Mheshimiwa balozi anasema kuwa Comoro wanatumia umeme wa jenereta. Grid yao ya taifa ni umeme unaozalishwa kwa jenereta hivyo si umeme wa uhakika.Tanzania inaweza ikazalisha umeme wa gas kisha ikawauzia Wacomoro.

Kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza wakafanya biashara ya majenereta na vifaa vyake kwa wingi.

8.Biashara ya magogo na mbao

Hii ni fursa kubwa sana kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwani Comoro kuna uhaba mkubwa sana wa mbao na magogo kwaajili ya kuchania mbao.Hivyo kama mtu atapeleka magogo huko maana yako hata mashine za kuchania Mbao bado ni deal.Kwa mujibu wa balozi anasema Comoro miti ya mbao ni michache sana hivyo wa Bongo wachangamkie fursa.

9.Biashara ya furnitures

Comoro wanategemea sana furniture kutokea Tanzania sofa, meza, nk so kwa Watanzania ambao ni mafundi sofa au wenye viwanda vya furniture wanaweza kuchangamkia hii fursa.Pia mafundi sofa na mafundi serelemala wa furniture wanaweza wakaji organise kisha wakafungua kiworkshop chao wakapiga hela nzuri tu.

10.Biashara ya Vanilla

Mheshimiwa Balozi anasema Comoro ni mzalishaji mkubwa sana wa vanilla duniani.Comoro vanilla kwao ni kama dhahabu na inabei kubwa wastani wa USD 500 kwa KG.Wakati wakulima wetu Bukoba na sehemu zingine Vanilla haifiki hata TSH 200,000 kwa KG.Hivyo basi mtu anaweza akanunua Vanilla Bongo kwa bei ya chini sana na akaenda kuiuza Comoro kwa bei ya juu sana.

11.Biashara ya screpa na spare za magari

Mheshimiwa baloz anasema magari mabovu ni mengi sana Comoro hii inatokana na wao kutokua na gereji za kisasa na mafundi wa kutosha.Hivyo basi unaweza ukapeleka spare za magari Comoro na unaporudi zako Bongo unarudi na spare used na screpa hivyo ukapiga hela double double.

Niishie hapa kwa leo ila balozi alisisitiza sana waTanzania watumie fursa hii maana Tanzania tuliwasaidia sana Comoro kupata uhuru wao pia hata mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea 2008 Tanzania ilisaidia sana Rais wa Comoro kurudishwa madarakan maana wanajeshi wetu walitumika kuzima mapinduzi hayo.
 
sema ukiambiwa hivi, nenda bana utaambiwa uwe mzawa kwanza, au biashara unayofanya hawepo mzawa.
 
magimbi yameenda kule na unga tani kadhaa kwa ajili ya mwezi ugali hawali ila uji wanakunywa ni wavivu kisen&g , bandarini kwao usipokua na mwenyeji mtz aishie kule fasta wanakuzika yani wanakuacha mikono mitupu wana njaa mno ila sijajua y hela yao inathamani vile
 
Mkuu funguka
 
Sasa kama screpa unasafirishaje kuleta Tanzania wakati hamna meli ya uhakika?
Ni kweli usafiri ni changamoto ndio maana mheshimiwa balozi aliwaomba waTanzania wenye nguvu kiuchumi wawekeze katika biashara ya usafirishaji kwanjia ya meli
 
Dah!! Ingekuwa usafiri wa meli wa uhakika screpa zingenihusu kabisa mkuu. Bakhresa au Azim Dewji wangepeleka meli Comoro,ingependeza zaidi
 
Habari wakuu,

Juzi asubuhi Jumamosi tarehe 26/05/2018 nilikua naangalia kipindi cha Clouds 360 on Saturday kinachoendeshwa na Siza na Gibson George.Mheshimiwa balozi wa Tanzania Comoro Mheshimiwa Sylvester Massele Mabumba alikua anazidadavua fursa kedekede zilizopo nchini Comoro.Kiufupi Comoro kuna fursa nyingi kwa mujibu wa mhe. Balozi na akawataka Watanzania wenye nguvu kiuchumi na wafanyabiashara wadogo kuwekeza na kufanya biashara huko.Kwa uchache fursa zenyewe ni kama zifuatazo;

1.Biashara ya chakula na vinywaji

Mheshimiwa balozi anasema asilimia kubwa ya vyakula inatoka kwetu, mchele, nyama ya ngo,mbe na mbuzi, mbogamboga na matunda nk, alitolea mfano papai la kawaida tu kwa Moroni linauza Tsh 7,000.Bado viungo mbalimbali kama iliki na karafuu bado vina soko kubwa.Vinywaji kama maji ya kunywa na juice pia zinatoka Tanzania.

2.Biashara ya Gereji /ufundi magari

Mheshimiwa Balozi anasema hakuna gereji Moroni zaidi ya kukuta magari yanatengenezewa tu mtaani na sio gereji kama tulizokua nazo Bongo.Kwa mafundi wa Tanzania hii ni fursa kama mtu ataenda kufungua gereji maana atakua kiproffessional zaidi hivyo kuaminika kibiashara.

3.Biashara ya bima

Hii ni biashara kwaajili ya waTanzania wanaofanya biashara Comoro na kwa Wacomoro wenyewe.Alitolea mfano namna wafanyabiashara wa Tanzania walivyopoteza ngombe na mbuzi ambao walikufa wakiwa baharini hivyo kupata hasara hivyo akawaasa wafanyabiashara kufungua insurance agencies maana wateja wapo.

4.Biashara ya Hoteli

Kwa wale wenye mitaji mikubwa ni fursa adhimu sana kwao na hakuna urasimu ndani ya siku moja unakamilisha usajili.Balozi anasema kuna hoteli kubwa moja five star na inamilikiwa na waTanzania

5.Fursa ya kufundisha Kiswahili na Kiingereza

Mheshimiwa balozi anasema Comoro wanahitaji sana waalimu haswa wa Kiswahili na akatolea mfano waTanzania wawili anaowafahamu ambao wanafundisha Kiswahili mjini Moron

6.Biashara ya usafirishaji

Hapa mheshimiwa balozi alitoa wito kwa wafanya biashara wakubwa kuanzisha safari za meli kutoka Tanzania mpaka Moron.Alitolea mfano kulikua na meli moja tu kutoka Zanzibar kwenda Comoro but ilikua haifiki Moron kabisa sababu ya kina Kidogo akatoa wito kwa wenye meli za wastani zifanye safari mpaka Moroni, pia meli ndogo kwaajili ya kusafirisha abiria ndani ya Comoro

Pia usafiri wa anga kuna fursa kubwa haswa hivi vi fly charter ni biashara kubwa sana

7.Biashara ya nishati ya umeme

Hapa ni kwa Serikali, Mheshimiwa balozi anasema kuwa Comoro wanatumia umeme wa jenereta. Grid yao ya taifa ni umeme unaozalishwa kwa jenereta hivyo si umeme wa uhakika.Tanzania inaweza ikazalisha umeme wa gas kisha ikawauzia Wacomoro.

Kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza wakafanya biashara ya majenereta na vifaa vyake kwa wingi.

8.Biashara ya magogo na mbao

Hii ni fursa kubwa sana kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwani Comoro kuna uhaba mkubwa sana wa mbao na magogo kwaajili ya kuchania mbao.Hivyo kama mtu atapeleka magogo huko maana yako hata mashine za kuchania Mbao bado ni deal.Kwa mujibu wa balozi anasema Comoro miti ya mbao ni michache sana hivyo wa Bongo wachangamkie fursa.

9.Biashara ya furnitures

Comoro wanategemea sana furniture kutokea Tanzania sofa, meza, nk so kwa Watanzania ambao ni mafundi sofa au wenye viwanda vya furniture wanaweza kuchangamkia hii fursa.Pia mafundi sofa na mafundi serelemala wa furniture wanaweza wakaji organise kisha wakafungua kiworkshop chao wakapiga hela nzuri tu.

10.Biashara ya Vanilla

Mheshimiwa Balozi anasema Comoro ni mzalishaji mkubwa sana wa vanilla duniani.Comoro vanilla kwao ni kama dhahabu na inabei kubwa wastani wa USD 500 kwa KG.Wakati wakulima wetu Bukoba na sehemu zingine Vanilla haifiki hata TSH 200,000 kwa KG.Hivyo basi mtu anaweza akanunua Vanilla Bongo kwa bei ya chini sana na akaenda kuiuza Comoro kwa bei ya juu sana.

11.Biashara ya screpa na spare za magari

Mheshimiwa baloz anasema magari mabovu ni mengi sana Comoro hii inatokana na wao kutokua na gereji za kisasa na mafundi wa kutosha.Hivyo basi unaweza ukapeleka spare za magari Comoro na unaporudi zako Bongo unarudi na spare used na screpa hivyo ukapiga hela double double.

Niishie hapa kwa leo ila balozi alisisitiza sana waTanzania watumie fursa hii maana Tanzania tuliwasaidia sana Comoro kupata uhuru wao pia hata mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea 2005 Tanzania ilisaidia sana Rais wa Comoro kurudishwa madarakan maana wanajeshi wetu walitumika kuzima mapinduzi hayo.
Mungu ambariki Mh. Balozi..
 
Mungu ambariki Mh. Balozi..
Sure mkuu tungekua na mabalozi wengine wanaoweza kuonesha fursa mbalimbali za biashara tungekua mbali.Fikiria Balozi alienda kuwapa pole wafanyabiashara ambao mifugo yao ilikufa,hakika kwa hili anafaa kupongezwa
 
Vipi political stability?

Maana naskia raisi amebadili katiba atawale milele!
Stability sijajua kwasasa but im sure iko poa kama kungea kua na lolote basi tungejua na sidhani kama Balozi anaweza kuwaambia watu wakawekezeze sehemu ambayo haina aman
 
Back
Top Bottom