Fursa za kibiashara zilizopo Kenya/Tanzania

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,431
1,250
Wakuu Naomba tutumie Uzi huu ku-post fursa za kibiashara zilizopo kwa jirani zetu Kenya ambazo watanzania tunaweza kuzitumia vivo hivyo kwa zilizopo Tanzania.Kwa kuchokoza, huko Kenya maeneo ya Mombasa inasemekana kuna kuna soko zuri la Karanga mbichi, Wakenya hebu tuelezeni kuhusu hilo
 
Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
9,578
2,000
Wakuu Naomba tutumie Uzi huu ku-post fursa za kibiashara zilizopo kwa jirani zetu Kenya ambazo watanzania tunaweza kuzitumia vivo hivyo kwa zilizopo Tanzania.Kwa kuchokoza, huko Kenya maeneo ya Mombasa inasemekana kuna kuna soko zuri la Karanga mbichi, Wakenya hebu tuelezeni kuhusu hilo
Fursa nyingi zipo Tatizo urasimu upande wa Tanzania,ukifika mpaka utajuta kuwa na biashara,ni kama umebeba kitu cha haramu,utakavyohangaishwa,na maofisa husika.
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
9,569
2,000
Kaka hata unga wa sembe toka TZ ni mali huko Kenya kwani huko kuna dona tu,nina jamaa zangu ambao huniagizia niwatumia unga wamahindi huwa nawanunulia pale Manzese na hufurahia sana,pia pumba za mahindi ni biashara nzuri Kenya hasa kwa ajili ya chakula cha mifugo kwani kama nilivyosema hapo mwanzo wenzetu husaga unga wa dona kwa hiyo huwa hawana pumba,kuna Wakenya huja Manzese na hujaza malori hizo pumba.
Kama alivyosema mdau tatizo ni vibali huko mipakani,usumbufu ni mkubwa,hizo biashara huenda mjomba au shangazi wako awe waziri ndipo utafanikiwa
 
chief muswati

Member
Apr 27, 2019
38
95
Wakuu Naomba tutumie Uzi huu ku-post fursa za kibiashara zilizopo kwa jirani zetu Kenya ambazo watanzania tunaweza kuzitumia vivo hivyo kwa zilizopo Tanzania.Kwa kuchokoza, huko Kenya maeneo ya Mombasa inasemekana kuna kuna soko zuri la Karanga mbichi, Wakenya hebu tuelezeni kuhusu hilo.wakenya tupeni ufafanuzi
 
Top Bottom