Fursa ya Kilimo cha Korosho Manispaa ya Lindi

Kwa kawaida heka moja linapandwa mikorosho 20 mpaka 25 kitaalamu ila 25 ndiyo inapendekezwa miche bora ya sasa inachukua miaka 2 mpaka kuanza kuzaa na kadri unavyohudumia miaka inavyoenda ndipo mti unazidi kukua na mazao yanaongezeka.

Uzalishaji wa mti mmoja unategemea pia huduma kusafisha shamba kupiga madawa sulphur booster n.k so kadiri unapo upa huduma nzuri basi na mazao pia yanaongezeka.

Huduma ya mkorosho mwanzoni huku miaka miwili ya mwanzo itakua migumu ndiyo maana unashauriwa kupanda na mazao mengine upate fedha za kuhudumia shamba pia ukipanda mazao mengine unapoyahudumia basi na miti ya mikorosho inapata huduma.

Katika project hii kuhudumia shamba jipya la heka moja haizidi 360,000 gharama zitapungua au kuongezeka kulingana na uamuzi wako labour force n.k.

Ila kama mkorosho umeanza kuzaa kadirio la juu kilo tano kutoka kwenye kila mkorosho inatosha kuhudumia mti mmoja ws korosho mti mmoja unatoa kilo 10 - 30 za mikorosho kulingana na uduma unazolipa shamba lako umri mazao yanaweza ongezeka au kupungua.

Na kwa makadirio heka moja inatoa tani 0.28 mpaka 0.40 inategemea huduma unazoupa mti au shamba na umri wa mikorosho yako inaweza zidi au pungua.

Sokoni kwa kilo moja unaweza pata 1000-4000 inategemea hali ya soko mfano kwa siku hizi sote tumeshuhudia kuwa bei katika minada imefika mpaka 3800-4080 kwa kilo ukitoa gharama hapo za uendeshaji kama ushuru n.k unapata si chini ya 3400-3680.

Soko ni la uhakika coz hapa watu wanapeleka minadani kama watu wakaungana wakatengeneza viwanda tusipeleke mnadani tukapeleka kiwandani basi fedha inaongezeka maana wote tunajua huko mitaani korosho iliyobanguliwa inauzwa vipi kwa kilo moja inafika 30,000.

"Katika project hii kuhudumia shamba jipya la heka moja haizidi 360,000 gharama zitapungua au kuongezeka kulingana na uamuzi wako labour force n.k" chief hapa umemaanisha hii gharama ya 360,000 kwa heka moja ni kwa muda wa miaka miwili hadi mkorosho utakapoanza kuzaa au ni zile gharama za mwanzo tu??
 
Mkuu kuna maeneo mawili mkoani Lindi natamani sana nifanye kilimo maeneo hayo 1) Mingoyo 2) na karibu na lake Mkoe.
Nikitaka kupata ardhi maeneo hayo nipeleke maombi hapo mkoani.
 
Sina cha kuandika nimeshapata Eka 10 zangu tayari.Nilibandika uzi siku kadhaa zilizopita kuhusu hii fursa lakini kuna watu walinipinga
 
Mkuu kuna maeneo mawili mkoani Lindi natamani sana nifanye kilimo maeneo hayo 1) Mingoyo 2) na karibu na lake Mkoe.
Nikitaka kupata ardhi maeneo hayo nipeleke maombi hapo mkoani.
Mingoyo ni halmashauri ya manispaa so peleka huko maombi yako ila kwa asilimia kubwa itakua ndiyo haya ambayo wanagawa ktk bproject hii
 
Sina cha kuandika nimeshapata Eka 10 zangu tayari.Nilibandika uzi siku kadhaa zilizopita kuhusu hii fursa lakini kuna watu walinipinga
Pole.
Mi nipo huku lindi so ni uhakika na mashamba yameisha umeshaenda kuoneshwa?
 
"Katika project hii kuhudumia shamba jipya la heka moja haizidi 360,000 gharama zitapungua au kuongezeka kulingana na uamuzi wako labour force n.k" chief hapa umemaanisha hii gharama ya 360,000 kwa heka moja ni kwa muda wa miaka miwili hadi mkorosho utakapoanza kuzaa au ni zile gharama za mwanzo tu??
Gharama ya kuanzia baada ya hapo ni kusafishia tu mikorosho wengine wanapiga dawa ya kuua magugu wengine wanapanda mazao mengine kunde xhoroko isipokuwa mbaazi n.k wanapohudumia hayo mazao na shamba pia linahudumiwa mpaka likianza kuzaa so ikishakua gharama zinakuwa ndogo sana ni madawa tu
 
Mkuu mkorosho unatumia madawa na mbolea ya aina gani ili uzae vizuri?
 
Korosho ina faida nyingi sana kula korosho nyeupe za kuchemshwa ni bora mara 100 kuliko kula pweza au mihogo mibichi. Ongeza heshima ya ndoa kula korosho nyeupe
Mkuu kwanza nakupongeza kwa kutangaza fursa hiyo japo mimi lo ndo naona....nimechelewa...
mimi nipo Dar ila huwa nafika sana maeneo ya Mtwara na lindi pia....kuna suala moja ambalo nashindwa kulipatia majibu nalo ni WIZI wa korosho pale ambapo zimeshakomaa,niliuliza wenyeji wa huku wenyewe wanaibiwa,wengine wanaamua kufuga nyoka shambani,wengine inabidi ujenge kajumba umuweke Mtu hapo...wewe hili unalizungumziaje?
 
Back
Top Bottom