Fursa ya biashara ndani ya visiwa vya Comoro

Mimi ni mfanyabiashara Tanzania na Comoro. Nilianza mwaka jana lakini mafaniko ni makubwa kwan kuna fursa nyingi sana sababu visiwa vya Comoro 96% wanategemea vitu pamoja na chakula kutoka nje.

Hivyo hupelekea kuwa na mahitaji kubwa ya hasa vyakula lakini changamoto hasa inayopelekea biashara ya Comoro kusua sua ni usafirishaji lakini fursa ni nyingi sana pia changamoto nyingne ni mmoja hasa kwa Watanzania hamna umoja kabisa wa kibiashara kwan hata kwenye upende wa usafirishaji Wacomoro ndio wanakodi meli tena hapa Tanzania na kijipatia pesa nzuri sana

Wakati tunauwezo wa kujikusanya wafanya biashara na kukodi chombo tutafanya supply kwa wakati sababu kuna kipindi Comoro nzima haina kitunguu ama vinywaj kama juice sababu tu hamna meli za kwenda lakini fursa ni nyingi sana

Herr muller
Bado unafanya business mkuu??
 
Alichoongea mtoa mada ni kweli kabisa kuhusu fursa za biashara Comoro, nakumbuka mwaka 2018 tuliungana watu kadhaa tukajichanga ili tukodi meli ya kupeleka bidhaa Comoro na biashara tuliyoikusudia ilikuwa mbuzi. Tulifanikiwa kweli kukodi hiyo meli kwa mmiliki kutoka Zanzibar kwa milioni 46.

Baada ya kukamilisha process zote za vibali mbuzi walichelewa kidogo kupatikana kutokana na idadi tuliyokusudia so ikabidi tupeleke kwanza mizigo ya wafanyabiashara wengine then meli ikirudi ndo tuanze biashara yetu ya mbuzi kama kawaida. Tulimchagua mwenzetu mmoja aende na meli na kupokea malipo yote ila baada ya kuondoka na ile meli na kupata malipo akatokomea.

Tulifuatilia sana hadi kwenda mahamani ila ndo hivyo tena haikuwezekana ikabidi kila mtu ashike njia yake maana wengi walikuwa very disappointed, mpaka leo plan nzima ya biashara ipo kwenye pc yangu huwa naiangalia tu but I know oneday hii biashara nitaifanya tu sijakata tamaa.
Duh poleni sana
Haya maisha yanatufundisha kutomuamini mtu yoyote linapokuja swala la fedha
 
Kwanza kabisa tukija kwenye upende wa pesa yao : comoro wanatumia Euro na comoro France (kmf) .pesa Yao ni mara 5 ya pesa yetu yan kmf 1 = Tsh 5 ..na kwa upende wa euro pia wametuzi kwao Euro 1= KMF 500 wakat kwetu Euro 1= Tsh 2,600/= iyo hupelekea biashara kuwa na faida kubwa ...turud kwenye bidhaa zinazoitajima sana ni:

Mboga mboga kama vitunguu,hoho,carrot,cabbage
Nyama ya ng'ombe/mbuzi
Ng'ombe / wazima
Juice hasa za Azam
maji
magimbi
magodolo
fenichers
nguo but hasa nguo za. ndan
matunda
tissue na vitu ving tuu ....

Sent using Jamii Forums mobile app
Vitu vingi vipo mbeya Tena unazoa tu bei za kutupa
 
Mimi ni mfanyabiashara Tanzania na Comoro. Nilianza mwaka jana lakini mafaniko ni makubwa kwan kuna fursa nyingi sana sababu visiwa vya Comoro 96% wanategemea vitu pamoja na chakula kutoka nje.

Hivyo hupelekea kuwa na mahitaji kubwa ya hasa vyakula lakini changamoto hasa inayopelekea biashara ya Comoro kusua sua ni usafirishaji lakini fursa ni nyingi sana pia changamoto nyingne ni mmoja hasa kwa Watanzania hamna umoja kabisa wa kibiashara kwan hata kwenye upende wa usafirishaji Wacomoro ndio wanakodi meli tena hapa Tanzania na kijipatia pesa nzuri sana

Wakati tunauwezo wa kujikusanya wafanya biashara na kukodi chombo tutafanya supply kwa wakati sababu kuna kipindi Comoro nzima haina kitunguu ama vinywaj kama juice sababu tu hamna meli za kwenda lakini fursa ni nyingi sana

Herr muller
Mkuu asante kwa kushare fursa nzuri kama hizi ubarikiwe sana. Huu moyo mzuri sana, nadhani na mimi kwako leo navuna nilichowahi kupanda humu JF. Niliwah kushare sana fursa humu ndani Jf miaka ya 2013 bahat mbaya tu nilikaa nje ya tanzania muda mrefu nikajikuta sikumbuki password ya account yangu. Na laini nilipoteza so nimeshindwa kurecover kabisa account yangu mpaka nikafungua mpya.

Mkuu
Naomba nisikuchoshe kukuuliza maswali mengi yahusiyo fursa, badala yake nisaidie kujibu haya machache niweze kuchukua hatua ya kuja mwenyewe kufanya research.

1.Kwanza je kuna meli ya abiria kuja comoro? Kma ipo napandia bandari gani?
2.Pili visa kuja uko inacost bei gan?
3.Je kuna usafiri wa ndege? unaweza kufaham nauli ni kiasi gani na ni kampuni gani ?
4.Katika kuja kufanya reasearch nataka kulala hotel isiyozidi shs 20,000, je zipo za bei nafuu?
5.Mimi naongea lugha 3, kiswahili, english, na kireno. Comoro wanatumia lugha gan? kama si english kuna huduma za watafisiri?
6.Je unaweza kufahama ubalozi wa comoro kwa tz uko maeneo gan?
7. Comoro ni nchi kama tanzania na ina raisi, naomba kujuwa ni mkoa gani au provence zipi zifaa kwa biashara. maana nisipoelewa hilo naweza jikuta naenda kufanya reaserch simiyu badala ya daresalaam

Natanguliza shukran.
 
Vitu venye uhitaji Comoros
Nyama fresh meat
Milk
Rice
Na nazani ni fursa nzuri kwetu watanzania kwenda huko njia rahisi ya kusafirishia ni kupitia mtwara na Kuna meli kule ya mizigo kabisa ilikuwa ishamalizika kutengenezewa sijajua mama safari zimeanza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom