Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, kwa kushirikiana na Mawakala mbalimbali wakiwemo kampuni tanzu ya Mkapa Foundation (Imara Horizon), Connect General Supplies Co. Ltd, Sassy Solutions Co. Ltd, pamoja na Larali Global Solutions, inawatangazia Watanzania wenye sifa kutuma maombi ya ajira kwa nafasi 800 za udereva.
Nafasi hizi zimetangazwa na kampuni ya usafirishaji ya MOWASALAT kutoka nchini Qatar, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kupanua fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania nje ya nchi. Waombaji wanahimizwa kuwasilisha maombi yao kwa kufuata taratibu rasmi, huku wakizingatia vigezo vilivyowekwa ili kufaidika na ajira hizi za kimataifa.