Furaha yangu kwa Azam TV, Tanzania

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
828
Ninawapa pongezi kwa kutoa zawadi kwa wateja wenu kwa kuwauliza maswali mepesi, uamuzi mliochukua ni furaha kwa wateja wenu.

Pesa taslimu kiasi cha 1000,000. (milioni moja) kwa wakati huu wa janga la Corona ni nyingi sana kwa kumuuliza swali lepesi na kuhakikisha king'amuzi kiwe na kifurushi.

Kama haitoshi (Mzee Bakhresa amependa tucheke naye, hongera kuwaonesha biashara inavyotakiwa kufanywa) Azam TV itatoa magari, sio gari bali magari. Hizi ni salamu kwa Dstv na Startimes.

Namalizia kwa kusema Azam TV Burudani kwa Wote, (ikiwezekana inunue Dstv Tanzania.)
 
Back
Top Bottom