Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
na wanawake ambao wamepingana nao huwa na wasifu ufuatao..............
1) wako zaidi ya miaka 35.......
2) wana elimu ya chuo...............
3) wana ex-boyfriends kibao.....................
4) mibadala yao ni pamoja na kuwa "single" au "come and stay"................
5) hawajui kazi za nyumbani na hawapo tayari kujifunza kwa madai ya kuwa ni utumwa kwao........wanapendelea "housegirl" awatimilizie mapungufu hayo...........................mapishi ya kisaidizi tajwa siwajua ni mchemsho na mafuta na chumvi kibao...............haunogi hata chembe baada ya mwenye jiko kulipiga teke.................
6) hawataki kuzaa zaidi ya watoto wawili..................hili ni jema........
7) wanaumme wengi huwaogopa wasije wakawatawala...............
8) wako tayari kuzaa na hata na mume wa mtu kwa visingizio ya kuwa walikuwa wanataka mtu wa kuzaa naye tu na wala siyo vinginevyo.....................................lol
9) huchukia mfumo dume na kupambana nao kadri iwezekanavyo..........
Lakini, wanadai wanaume wengi wanaogopa wanawake wasomi na ndio maana hawako kwenye nasafi nzuri ya kuolewa, ukilinganisha na wale wenye elimu ya kati, sababu kubwa ni wanaume kuogopa challenge....................
so what?
Kuna mmoja nilimuuliza humu kama haitaki ndoa akanijibu fasta kweli kwamba haitaki..
Ngoja nisubiri nione kama atakuja kujibu haya makombora kama yanamsadifu ama la, hususani penye red..
Nanihii, where are you? Lol.......
Mutambuzi uko sahihi kabisa..................lakini changamoto zao wengi twaona ni karaha tupu wakati wako wengi wanaoheshimu asilia..........
Hizi sababu zako ni za juu juu sana..
Umewahi kufikiria ya kwamba kuna wengine
wali nyanyaswa (abused) wakiwa wadogo na hata
ukubwani mfano
Physical, mental, Emotional, & Sexual .. mfano wa
watu awaliobakwa..
Naomba ufikirie chambua kabla ya kupayuka..asante
I salute you for these words!! Nashukuru umethibitisha mwenyewe kuwa wenye matatizo sio wanawake ila nyie wenyewe wanaume ndo mnaogopa challenge....period!!! Kila nikijaribu kuipima akili yenu naona kama wote imeganda upande mmoja, mnawaza vya ajabu sana. Hivi challenge maana yake ni kutoiheshimu asilia?? Asante kwa ufafanuzi wa pili kuwa changamoto zao mwaziona ni kama karaha, hahahah while in real sense sio karaha. . . . . . .crap!!!
Ndio maana Makungwi na Manyakanga wanawashauri, ili ndoa zenu zidumu, inabidi wanawake mjifanye wajinga........... Hebu niambie mwanamke aliyesoma sheria, kama kaolewa na mume mwenye ordinary education, unafikiri akitaka haki bin haki ndoa hiyo itadumu? kwa mume itatafsiriwa kwamba anataka kumtawala kwa sababu ya elimu yake............!
Kujifanya mjinga once in a while sikatai lakini si kwa kila kitu bana, eti ifuatwe akili yenu tu.....NO!! So wataka kutuambia tuishi tu kwenye ndoa ili kuwafurahisha nyie tu sio?? Btw, sheria is a career na haihusiani na ndoa ya mtu, unless by subsequent reasons! Wanaweza kudumu au wasidumu inategemea na wao wenyewe na maelewano yao!!
Kwani wewe hujui kwamba kuna baadhi ya wanaume wana akili za kushikiwa!.............. Hata wewe mwenyewe ni shahidi wa yale yanayoulizwa na baadhi yao humu MMU..............