Furaha na haki sawa kwa wote

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
FURAHA NA HAKI SAWA KWA WOTE

Waasisi wa The Civic United Front(CUF-Chama Cha Wananchi) walikutana katika Ukumbi wa Starlight Hotel, Mjini Dar es Salaam tarehe 20-21 Novemba 1992 walitoa Tamko ambalo ni Utangulizi wa Katiba ya Chama Chetu. Katika Tamko hilo walieleza kuwa:-

"Sisi Watanzania tuliokutana Dar es Salaam kwa muda wa siku mbili, tarehe 20-21 Novemba 1992 tunaamini kuwa Haki za Binadamu na Haki za Watu, kama zilivyotangazwa katika Tangazo la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa , na HATI ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika juu ya Haki za Binadamu na Haki za Watu , ndiyo msingi wa Sheria na Kanuni zinazotakiwa kuongoza nchi....

Tumeamua kuunda Chama hiki, THE CIVIC UNITED FRONT(CUF-Chama Cha Wananchi), kwa nia ya kuwaunganisha watu wa Tanzania wenye kuamini kwa dhati juu ya kuwepo kwa demokrasia ya kweli ambapo wananchi wenyewe ndio wenye mamlaka, madaraka na uamuzi wa mwisho kuhusu mambo yao na nchi yao.

Tumechukua uamuzi huo wa kihistoria ili kutekeleza Imani yetu juu ya Haki za Binadamu na Haki za Watu, kwa kutumia itikadi, au falsafa yetu mpya itakayojulikana kwa jina la UTAJIRISHO, yenye Maana pana ya Haki Sawa kwa Wote na Neema kwa Wote.

ITIKADI YETU NI UTAJIRISHO
 
ACT ....ndo nini kama kichwani mawimbi yamekaa vibaya unaweza pita kimya kimya ...Tz hakuna chama kinaitwa CAT kuwa makini unatutia aibu Hapa Jf.
Kile cha mapaka. Wewe ndio huna akili huelewi mambo upo kizamani eti ACT ndio nn kama hujui uliza sio kisebengo kama mwali wa kizaramo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kile cha mapaka. Wewe ndio huna akili huelewi mambo upo kizamani eti ACT ndio nn kama hujui uliza sio kisebengo kama mwali wa kizaramo

Sent using Jamii Forums mobile app



Tz hakuna chama kinaitwa CAT ,,,kama kipo naomba moderator wanipe ban ...ukiwa ccm sijui unapagawa kichwa , mkuu tafuta chakula kwanza lazima hii ni njaa
 
CAT ....ndo nini kama kichwani mawimbi yamekaa vibaya unaweza pita kimya kimya ...Tz hakuna chama kinaitwa CAT kuwa makini unatutia aibu Hapa Jf.

Jamaa alimaanisha ACT Wazalendo....!!!
Inaonesha hata hiyo USSR ukimwambia aeleze maanake ni Giza! Kazi kwelikweli.
 
Back
Top Bottom