Furaha inaweza kununuliwa?

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
FURAHA INAWEZA KUNUNULIWA?

Kila mtu anataka furaha kwenye maisha yake. Hata wale ambao wanafanya makosa, wanafanya hivyo wakiamini yatawaletea furaha. Hakuna mtu ambaye atapewa kati ya furaha na mateso na akachagua mateso, labda awe na matatizo yake binafsi.

Sasa baada ya watu kulijua hili, wamekuwa wakilitumia vibaya kwako wewe.Wafanyabiashara na makampuni wamekuwa wakitumia hitaji hilo la furaha kukushawishi wewe ununue zaidi bidhaa au huduma zao.

Wanachokifanya ni kuitangaza bidhaa au huduma yao kama chanzo kikuu cha furaha. Ya kwamba ukitumia tu utakuwa na furaha kubwa.Na katika matangazo hayo hutumia picha au watu ambao wanaonekana kuwa na furaha sana.

Kwa kuona wale wana furaha, basi na sisi tunashawishika kwamba tukinunua bidhaa au huduma ile tutakuwa na furaha kubwa. Tunanunua bidhaa au huduma ile, na ndani ya muda mfupi tunajisikia raha, sio furaha. Lakini baada ya muda huo mfupi kuisha, mambo yanarudi pale pale, bado hatuna furaha.

Leo nataka tukumbushane jambo muhimu sana kuhusu furaha, tunakumbushana kwa sababu tulishajadili hili mara nyingi. Hakuna kitu chochote unachoweza kununua kikakupa furaha. Kwa kifupi, furaha hainunuliwi. Kama mtu anakuambia nunua hiki utapata furaha, kimbia haraka sana, maana anachotaka kufanya ni kukutapeli.

Kama hapo ulipo sasa, kwa maisha unayoishi na kazi au biashara unayofanya, huna furaha, basi hakuna kitu chochote ambacho unaweza kununua leo na kikakupa furaha. Hakuna. Furaha ni kitu ambacho kinaanzia ndani yako. ni kitu ambacho kinatoka ndani ya nafsi yako, bila ya kujali unamiliki nini kwenye wakati huo.

Furaha ni zao la maisha unayoishi, mchango wako kwa wengine, na kuridhika na kazi au biashara unayofanya na sio zao la nini unamiliki. Ni kweli kumiliki vitu ambavyo ni muhimu kwako kunafanya maisha yawe bora na maisha yakiwa bora unakuwa na furaha.

Lakini tunarudi kwenye jambo la msingi kwamba hakuna kitu ambacho ukienda kununua sasa hivi basi utapata furaha, unaweza kupata tu raha ya muda mfupi, lakini sio furaha.
Furaha ni kazi ya ndani kwako mwenyewe, usidanganyike kuinunua.
 
Mimi naamin furaha ya mtu huja pale mambo ama shughuli zake anazozifanya zinapofanikiwa hivyo kufanya ndoto zake kuwa kweli...Haijalishi uthamani wa ndoto hizo mwingine atapata furaha baada ya kitalu chake cha mchicha kumea na mwingine baada ya kununua Vogue na mwingine baada ya dili zake kufanikiwa.
 
Mimi naamin furaha ya mtu huja pale mambo ama shughuli zake anazozifanya zinapofanikiwa hivyo kufanya ndoto zake kuwa kweli...Haijalishi uthamani wa ndoto hizo mwingine atapata furaha baada ya kitalu chake cha mchicha kumea na mwingine baada ya kununua Vogue na mwingine baada ya dili zake kufanikiwa.
Asante kwa mawazo yako pia. Ni mazuri.
 
Lakini tunarudi kwenye jambo la msingi kwamba hakuna kitu ambacho ukienda kununua sasa hivi basi utapata furaha, unaweza kupata tu raha ya muda mfupi, lakini sio furaha.

Kwani furaha ya muda mfupi siyo furaha?

Furaha ni lazima tu iwe ya muda mrefu?

Na muda mfupi na mrefu ni kiasi gani hasa?
 
Nilipata kusoma kitabu cha David mailu anasema you can find happiness through the jungle of your inner self.
 
Mi nikiwa na pesa Tu nakua na furaha balaa,isipokuwepo hakuna furaha kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom