Furaha ikawa huzuni.

Furaha ikawa huzuni.

google helper

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
9,667
Reaction score
13,877
Habari wana jamvi.
Ilikuwa miaka ile tukiwa wanafunzi, miezi michache tufanye necta form six. Kipindi hicho voda wana tangazo lao hilo mdada analalamika umenikanyaga( kama una kumbukumbu utajua mwaka). Basi mabweni yoote asubuhi ile tunajiandaa kwenda darasani mara huyu yuko na boxer, huyu uchi, kila mtu na pozi lake wanakusanyika kusikiliza tangazo ili wamsikie huyo mdada anavyolalamika roho zipate raha. Kama unavyojua hakuna demu basi watu wanaona hiyo sauti ndio fursa.

So kwa kuwa muda mfupi tu umebaki kufanya mtihani darasani hakuna saaana issue, watu wanaingia chimbo kila mtu kwake sana sana kupambana na mwanaume physics. Jamaa mmoja mtulivu tu, mkimya mkimya hivi wa PGM, sikuwa namfahamu sana maana tulikuwa tunaonana pindi moja moja hasa physics akaja na redio kwenye chimbo langu. Sijui alipitwa na sauti ya manzi ile asubuhi basi, ametega baada ya taarifa ya habari mchana lile tangazo lijirudie.

Basi redio oooone steriooo mwisho wa Habari, tangazo likapigwa fresh jamaa akafurahiaaa na kucheka sanaa, naona alikuwa anavuta stimu za nyeto jion akienda kuoga. Lahaula matangazo ya vifo yakaanza baada ya tangazo. Mie niko kimya tu pembeni na ugali wangu navuta stimu za pilau ili nile ugali wa kutosha.

Mara ghafla jamaa amekuwa mwekundu baada ya kusikia familia yao inatangaza kifo cha baba ake mzazi. Furaha yoote ikapinduka jamaa analia kwamba weekend alitoroka akaenda home baba ake alikuwa fresh tu. Daaah nilishindwa nimpe huduma gani. Mwanaume analia kwa uchungu hatari, ubaya redio haziruhusiwi, hata tukienda kusema kwa walimu tutasema taarifa kapata wapii?

Ilikuwa bonge la noma. Baada ya wanafunzi wengine kuja na kujua tukio zima basi tukampeleka bwenini, tukampa ushauri konki akatulia, ili kuepusha taaruki tukamwambia ajikaze mpaka kesho yake ndugu zake lazima waje kutoa taarifa. Kweli asubuhi mjomba ake kafika shule kamchukua jamaa wakaenda home.

Nikikumbuka hili tukio alafu nikaona mtu amefiwa na baba au mama namwonea huruma sana. Poleni mlio fiwa
Pole classmate wangu! Japo umepoa kwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom