Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,614
- Thread starter
- #61
Nahitaji hiyo fumula ya kutengeza niko mbali
Funza wanaweza kupandwa ukitumia mbinu rahisi na hutumiwa kama nyongeza katika lishe ya vifaranga wadogo.
Hivi ndivyo inavyo fanywa.
1. Changanya damu na matumbo ya mnyama(kwa mfano ng’ombe ama mbuzi) na samadi ya ng’ombe katika chungu kikubwa kilicho wazi.
2. Jaza chungu na 1/3 ya maji.
3. Nzi watataga mayai yao katika mchanganyiko huu na funza wataula.
4. Kiache chungu wazi wakati wa mchana na kifunike wakati wa usiku.
5. Funza wakiwa wakubwa,wakusanye kwa kumwaga maji pole pole kwenye chungu.
6. Funza wataelea na unaweza kuwaosha na kuwalisha kwa ndege moja kwa moja.
7. Kumbuka kukiweka chungu mbali na maeneo ya umma kwani hunuka sana.
Kwenye namba 7; hapo ndo unapotakiwa kutumia Em solution ambayo kazi yake ni kuwakuza haraka na kukata harufu mbaya.