Funguka: Maisha yamekufunza nini?

nimejifunza kuwa wanawake wawe waangalifu maana wanaume wengi wa sasa ni waoga wa maisha hivyo pendo la ndoa ni pamoja na kipato cha mke.

hapo Kweli kuna funzo...
 
Nimejifunza kuwa huweI kuwa njuu siku zote, ndio maana prof jay anasema wangapi walikuwa nazo na sasa hawana na wangapi walikuwa hawana na sasa wanazo concept ninayosema ni hii ni ivi utakuwa juu siku zote na utakuwa chini siku zote maisha mazuri ni kwa kila mtu ata ww masikin leo utaweza kuwa tajiri kesho
 
Nilichojifunza ni kuwa life is how you make it. Ukifikiri negative maisha yanakua magumu. Na ukifikiri positive na kutenda positive maisha yanakua murua.
 

Serikalini ndio watu wanajifunza hivyo? Mhhh
 
Nimejifunza kuamini Mungu yupo ila Dini hazipo kabisa zimeletwa na wazungu na waarabu,nimejifunza kua mkarimu kwa yeyote pia kumshukuru Mungu napopitia magumu, pia kusamehe wanafiki na wachawi wa mitaan japo hua ni ngumu kwangu
Pia nimejifunza kumpenda anaenipenda na kupotezea anaenipotezeaa
Pia hakuna rafiki wa kweli duniani maana kikulacho kinguoni mwako
 
Maisha yamenifunza kutambua hakuna binadamu aliye mwema kwa mwingine 100%
 
Haya ndiyo niliyojifunza;
  1. Furaha katika maisha inajengwa na mtu binafsi, usitegemee binaadam mwenzio akusababishie furaha
  2. Ninaishi na binaadamu na sio malaika, at the same time na mimi ni binaadam sio malaika. Sishangai nikikosewa kwa sababu hata mimi nawakosea binaadam wenzangu. Kikubwa ni kuwa tayari kusamehe
  3. Kujishusha na kuomba msamaha ni sadaka kubwa sana, na ukifanikiwa katika hili hakika utaishi kwa amani
  4. Never say never!Dawa ni kuomba neema ya Mungu kila iwapo leo
 

Well said, Hata Mimi ckukata tamaa mazoezi mpaka kile kitambi kimeisha chote aisee
 
Maisha yamenifunza haya;
1.Hauwezi kumridhisha kila mtu
2.Si kila wakiaminio watu wengi ni sahihi.
3.Mpende adui yako...kuwa mwangalifu na rafiki zako
4.Kushindwa ndiyo mwanzo wa kuweza..
5.Mambo yakiwa magumu...hesabu baraka zako na uwe na moyo wa shukrani
 
Nimejifunza
1.kumtegemea Mungu katika kila jambo,
2.kuwa na upendo kwa Mungu wangu na kwa wanadamu wenzangu,
3.kuishi kwa kuwaheshimu watu wote maana huwezi jua nani atakufaa kwa lipi na kwa wakati upi,
4.kutokukata tamaa,
5.kujipa furaha kwanza maana furaha ya kweli hawezi nipa mtu mwingine ila mimi
5.kuwa na kiasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…