cleaner wrasse
JF-Expert Member
- Apr 5, 2013
- 9,076
- 10,106
Fungu lote langu
Kwenye Fungu la Kumi haitakiwi kuongeza wala kupunguza.Nikizidisha au nikipunguza Kuna shida?
Kwa nini?Kwenye Fungu la Kumi haitakiwi kuongeza wala kupunguza.
Fungu la kumi ni upigaji kanisani.Wakuu embu tuwe waelewa na turuhusu akili zetu zifanye kazi. Fungu la 10 kutoa ama kutotoa sio kosa. Fungu la 10 pia inafahamika kama Zaka.
Zaka yaani fungu la 10 ilikuwa ni SHERIA kwa wana wa Israel. Ilikuwa ni lazima itolewe kwa kila Myahudi. Na ilikuwa inatolewa ili kuwezesha makuhani, kusaidia wahitaji nk haikuwa ni pato la mtu mmoja binafsi kama ilivyo leo ktk makanisa mengi hasa ya kipentecoste.
Agano jipya linafafanua kwa habari ya mtu kutoa kwa HIYARI, kile ambacho MOYO wako kinakupa amani kutoa kwa ajili ya Mungu na sio SHERIA tena kama ilivyokuwa kwa Wayahudi na ndio maana kuna mkanganyiko ndani ya makanisa, madhehebu, kuna wanaoamini ktk ZAKA na kuna wanaoamini kwamba Mungu ameruhusu mtu atoe kwa Moyo kama lisemavyo agano jipya.