Fundi umeme nipo hapa

Fundi umeme nipo hapa

Joined
Feb 17, 2023
Posts
31
Reaction score
37
Habari zenu,
Ni mwaka wa 9 sasa nimekuwa nikizunguka na kampuni X nikiwa kama fundi umeme wa kampuni ilihali sijasomea io taaluma, nimekuwa ni mtu wa kujisomea majarida na vitabu mbalimbali vinavyohusu masuala ya umeme pamoja na kufundishwa na wabobezi wangu.

Nimefanya shughuli za ufundi umeme katika ujenzi wa benki ya CRDB bank Monduli Arusha, Malind fish market Zanzibar, international school of Tanganyika (IST) Masaki DSM, The soul Paje Zanzibar, Catalonia grand Zanzibar, Standard chartered bank posta DSM nikiwa chini ya kampuni X, pia nimefanya kazi ya wiring, kufunga vifaa vya umeme na kutatua matatizo ya shoti za umeme katika nyumba za makazi na sehemu za biashara.

Hatujapata tenda kwa sasa, mwenye uhitaji wa fundi umeme ata kuniunganisha na kampuni nipo tayari.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.

febujinji20@gmail.com
0684487043 whatsapp
 
Sasa hapo umekosa kitu kimoja tu, VETA pita pale kajinoe kidogo, upate gamba baada ya hapo, utaongeza Imani Kwa waajiri sawa kazi utapata lkn pale itakapotokea dosari kwenye kazi ndo utajua umuhimu wa gamba! Fanya hivyo mkuu! All the best!
 
Back
Top Bottom