Fundi ujenzi bora, mwenye bei nafuu njoo unijengee

Ni kweli kule gharama ni ndogo mkuu,ila ukitaka nyumba nzuri na itakayokushawishi upaite nyumbani na sio bandani tumia mafundi wabobezi watakaokujengea vizuri na uwalipe vizuri pia. Changamoto ya ujenzi ina mambo mengi,mwingine anaweza akakuinulia msingi nyumba ikasimama na ikaonekana nzuri ,mwingine anaweza kujenga ata msingi usionekano na nyumba kuonekana banda. Hivyo hivyo hata katika upauaji...mwingine atakuwekea mteremko wa kawaida usiovutia na kuna wengine wanaweka mteremko mkali wa kuvutia.Nashauri atafute mafundi wabobezi ambao wamejenga kitu kizuri na awalipe vizuri wamfanyie kitu cha maana.
Mkuu ukishakua na ramani ya nyumba kila kitu kinakua wazi maana huo ndo mfumo wa ujenzi wa nyumba kwa Tanzania hii hao unaowaita professional wote wanafanya kwa mfumo huo ingawa gharama zitakua juu ila watajenga kwa kupigia hesabu tofali husika
 
Huwa wanaweka gata za plastiki (PVC) au za zege (concrete),wengine wanaunganisha bati na tofali ambayo ni makosa;sasa katika kutumia hiyo mifumo wapo wanaofanikisha isivuje na wapo wasiofanikisha na inavuja.
Sawa mkuu hizi ndo wanaziita contemporary housing sio?
 
Mkuu ukishakua na ramani ya nyumba kila kitu kinakua wazi maana huo ndo mfumo wa ujenzi wa nyumba kwa Tanzania hii hao unaowaita professional wote wanafanya kwa mfumo huo ingawa gharama zitakua juu ila watajenga kwa kupigia hesabu tofali husika
Ni kweli mkuu,kwa upande wangu huwa nikitaka kufanya ujenzi...huwa natembelea majengo yaliyojengwa na kuvutia...baada ya hapo naulizia fundi aliyejenga,baadaye nitawasiliana naye na kumueleza mahitaji yangu kufuatana na ramani niliyonayo,na tunapatana bei na kazi kuanza. Kwa hiyo fundi wa kusimamisha jengo ni mwingine,wa kupaua mwingine,wa plasta anaweza kuwa mwingine,wa urembo pia anakua mwingine n.k na fundi atachaguliwa kutokana na kazi alizofanya huko nyuma....wengi huwa wanakuja na picha(albam) au za kwenye simu.
 
Nilitaka kuandika hivyo kwamba fundi wa msingi ni mwingine, anaefikisha kwenye linta ni mwingine, anae paua ni mwingine..na huo ndo ujenzi sahihi mkuu...ila unajua kwamba hawa wanaojiita mafundi wengi wao sio mafundi bali ni madalali wa kazi i.e walishawahi kua site foreman yani wasimamizi wa ujenzi
 
Unachosema ni ya kweli mkuu,madalali ndio wanapandisha bei. Jaribu kutembelea haya majengo makubwa,bara bara n.k wanaosuka nondo na kusimamisha jengo ni watu wakawaida....ila Engineer yeye anawasimamia tu na kuwapa maelekezo basi,lakini kazi yote imefanywa na watu wa darasa la saba n.k.
 
Mimi principle nilizozitengeneza ni hizi namuuliza fundi je wewe ni fundi akisema ndio namwambia na mimi nitakuwepo site nataka nikuone wewe ukijenga sio unawaelekeza watu hapo kama yeye sio mjenzi lazima akatae either namlipa kwa siku au kwa tofali hela nakaa nazo mfukoni nazitolea mfukoni ukijenga ujenzi wa hivyo huwezi kua na pressure wala stress mkuu kabla sijajua hivi vitu mafundi walikua wananisumbua sehemu ndogo wanataka hela nyingi
 
ha ha ha ha wanasumbua sana,ila unaweza pia kuwatafuta kupitia mitandao ya kijamii,wapo ambao wanatuma kazi walizofanya na zingine zinawaonyesha wakiwa field
 
Hello habarini za muda huu, poleni na covid-19 popote mlipo, natafuta fundi bora, atakayenipa makadilia mazuri ya kusimamisha (namaanisha boma tupu) kwanza, nyumba mahitaji yafuatayo

vyumba viwili (kimoja master),
Sebure kubwa+dinning
Jiko+store
Choo+bafu
Note: vyumba vyote viwili viwe na makabati ya ukutani

Eneo
-lipo dar es salaam (mbezi ya kimara)
-eneo lipo tambalale (sio la kuchonga)
-eneo ni 20m*25m

NINACHOTAKA
-pesa ipo mfukoni
-Nataka kujenga mtindo wa nyumba wa kisasa (usiochukua bati nyingi na mbao nyingi)
-nataka fundi anipe mahesabu ya kusimamisha boma kwanza (pagara).

"FUNDI MWENYE MAKADILIO YANAYOTEKELEZEKA NA GHARAMA NAFUU NAMPATIA KAZI HII YA KUNIJENGEA"

Hii ni hapo chini ni mfano wa nyumba ninayoitaka

Note: naanza kwanza na boma, kwa kuwa pesa yangu sio nyingi na nimejichanga mnoo kuipata. Unaponipa bei jaribu kuzingatia kuwa mimi ni mkulima mdogo wa jembe la mkono, usiniumize sana.

Karibuni sana, kwa ushauri na mapendekezo.
View attachment 1436491View attachment 1436494

View attachment 1436504

Hii nyumba Ipo Goba
 
Mimi ni Architect.Kama huna ramani ya nyumba ntakuchorea bure.tunafanya designing and build.Kazi kama yako tumetoka kuifanya ponde huku kigamboni.Gharama zetu za ujenzi ni Tshs 2,800,000/= Kwa nyumba yenye requirements hizo.Tutaandikishiana mkataba kwa wanasheria kabla ya kazi kuanza.Kwa maelezo zaidi karibu ofisini kwetu kijichi au piga simu namba 0756928360.Hatuna ubabaishaji wa kijinga karibu tufanye kazi.
 
Sasa mkuu haujaona ramani ya jengo unawezaje kusema gharama yako ni 2,800,000?
 
Kwa requirement alizosema na site yake alivyo ieleza na udhoefu nilionao kwenye ujenzi ni rahisi sana kutambua hilo.Pia kwa maelezo yake inaonekana hana mchoro ila ana picha anayotamani nyumba yake ifanane hivyo.ndo maana nikamwambia mchoro nitamcholea bure.
 
Unachosema ni ya kweli mkuu,madalali ndio wanapandisha bei. Jaribu kutembelea haya majengo makubwa,bara bara n.k wanaosuka nondo na kusimamisha jengo ni watu wakawaida....ila Engineer yeye anawasimamia tu na kuwapa maelekezo basi,lakini kazi yote imefanywa na watu wa darasa la saba n.k.
Mkuu labda hujui kaz ya engineer ni kubwa sana kuliko unavyofikir kaz hizo unazoona zinafanya na hao mafundi unaowaita wakawaida nyuma yake kuna proffetionals ambao kaz yao ni design na implimentation kuhakikishwa kilicho designiwa kwny raman ndo kinachojengwa. Tupende kuheshimu proffetional za watu. Mfano halisi ni hiz contemporally house aka nyumba zenye paa lililojifacha changamoto zake km wadau wanavyosema kiuhalisia si changamoto bali ni ujenz unaokosa umakini na usimamizi wa hali ya juu husababisha kuvuja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kawaida vitu vya bei nafuu huwa vinagharama kubwa.Watu wengi huwa wanawalaumu mafundi kumbe kosa ni la client mwenyewe.fundi kazi yake ni kuimplement anachoelekezwa na wataalamu iwe engener au architect.na ubaya wa mafundi wa siku hizi ili kupata kazi atajifanya anaweza kila kitu.
 
Mkuu labda hujui kaz ya engineer ni kubwa sana kuliko unavyofikir kaz hizo unazoona zinafanya na hao mafundi unaowaita wakawaida nyuma yake kuna proffetionals ambao kaz yao ni design na implimentation kuhakikishwa kilicho designiwa kwny raman ndo kinachojengwa. Tupende kuheshimu proffetional za watu. Mfano halisi ni hiz contemporally house aka nyumba zenye paa lililojifacha changamoto zake km wadau wanavyosema kiuhalisia si changamoto bali ni ujenz unaokosa umakini na usimamizi wa hali ya juu husababisha kuvuja

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na wewe mkuu,ila mtu ambaye yuko field ni bora zaidi kuliko yule anayeelekeza
 
Back
Top Bottom