Fundi ujenzi bora, mwenye bei nafuu njoo unijengee

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,929
Hello habarini za muda huu, poleni na covid-19 popote mlipo, natafuta fundi bora, atakayenipa makadilia mazuri ya kusimamisha (namaanisha boma tupu) kwanza, nyumba mahitaji yafuatayo

vyumba viwili (kimoja master),
Sebure kubwa+dinning
Jiko+store
Choo+bafu
Note: vyumba vyote viwili viwe na makabati ya ukutani

Eneo
-lipo dar es salaam (mbezi ya kimara)
-eneo lipo tambalale (sio la kuchonga)
-eneo ni 20m*25m

NINACHOTAKA
-pesa ipo mfukoni
-Nataka kujenga mtindo wa nyumba wa kisasa (usiochukua bati nyingi na mbao nyingi)
-nataka fundi anipe mahesabu ya kusimamisha boma kwanza (pagara).

"FUNDI MWENYE MAKADILIO YANAYOTEKELEZEKA NA GHARAMA NAFUU NAMPATIA KAZI HII YA KUNIJENGEA"

Hii ni hapo chini ni mfano wa nyumba ninayoitaka

Note: naanza kwanza na boma, kwa kuwa pesa yangu sio nyingi na nimejichanga mnoo kuipata. Unaponipa bei jaribu kuzingatia kuwa mimi ni mkulima mdogo wa jembe la mkono, usiniumize sana.

Karibuni sana, kwa ushauri na mapendekezo.
View attachment 1436491View attachment 1436494

colmanassey_iamtanzarch_20200423_055824_0.jpg

colmanassey_iamtanzarch_20200423_055824_1.jpg
 
Una shilingi ngapi ? Mbzii ya kimara udongo Wa mfinyanzi una kazi kubwa kwenye msingi .Weka Wewe una shilingi ngapi budget na eleza kiwanja kiko eneo tambarare au mwinuko? Upatikanaji Wa vifaa vya ujenzi ukoje, mfano.mchanga, kokoto, tofali, maji nk
 
Ilo eneo mkuu upatikanaji wa vifaa ni jambo jepesi sana, maana maduka ya vifaa vya ujezi (kokoto, mchanga, cement) vipo karibu kabisa

Sent using komputa mpakato
 
Fanya hivi weka ramani ya nyumba hiyo.ni kazi yako tafuta mchoraji kisha njoo tena eleza unataka contractor Wa kujenga nyumba yote au unataka vifaa na kila kitu utatoa wewe na kuvileta site ikiwrmo.kukiweka kiwanja saw a yaani leveling nk kazi ya fundi iwe kujenga tu
Nataka fundi wa kujenga tu, material kwangu

Sent using komputa mpakato
 
Hii ndiyo changamoto kubwa mkuu. Kuvuja na kkuweka uchafu juu ya paa.

Rahisi kuhifadhi wanyama nyoka...paka n.k
ooh ok, mnanishaurije wakuu, niachane na mfumo huu niende na mfumo wetu wa kawaida wa paa la kushuka, ushauri wenu ni wa muhimu mnoo.
 
ooh ok, mnanishaurije wakuu, niachane na mfumo huu niende na mfumo wetu wa kawaida wa paa la kushuka, ushauri wenu ni wa muhimu mnoo.
Kwa uzoefu hiyo ndiyo changamoto niijuayo mkuu... ila wahandisi na mafundi nadhani watakuwa watu sahihi wa kukupa mwongozo.
 
Mzee unanishaurije, maana ndio format ya nyumba nilioipenda sana

Sent using komputa mpakato
Kimuonekano ni nyumba nzuri ila changamoto ndio hizo,kuna majirani zangu wamejenga muundo huo kama 3,changamoto walizokutana nazo ndio hizo.Cha kufanya,wasiliana na fundi na akupe majibu ya kuridhisha hayo maji huko mwishoni mwa ukuta atakuwa anayakusanyaje?na pia akuthibitishie hiyo changamoto haitakuwepo,vinginevyo utaijenga hiyo nyumba na utaichukia kipindi cha masika. Hata wanaojenga gorofa tunawashauri wasiezeke kwa zege...kwa sababu kuna muda inafikia na kuvujisha maji.Ndio maana magorofa mengi kwa sasa yanaezekwa kwa paa/vigae.
 
Hii ndiyo changamoto kubwa mkuu. Kuvuja na kkuweka uchafu juu ya paa.

Rahisi kuhifadhi wanyama nyoka...paka n.k
Pia paa kukanyagwa kanyagwa kwa ajili ya usafi ni tatizo;inapunguza uimara na kuongeza uvujaji, ndio hivyo vitu vizuri vina changamoto zake
 
  • Thanks
Reactions: amu
ooh ok, mnanishaurije wakuu, niachane na mfumo huu niende na mfumo wetu wa kawaida wa paa la kushuka, ushauri wenu ni wa muhimu mnoo.
Ukipata fundi mzuri anaweza akakujengea vizuri na hilo tatizo lisiwepo;uzuri wa huo muundo,unatumia mbao na bati chache,na kwa sababu bati zinafunikwa,unaweza tumia haya mabati ya kawaida
 
  • Thanks
Reactions: amu
Changamoto ya hizi nyumba huwa ni uezekaji; nyingi huwa zinavuja. Kwa kukushauri, nunua tofari kwanza 2500pcs, weka mchanga tipa 2, nunua simenti mifuko 50,ita fundi anaweza kuanzia 1.5M+
Mkuu unajua uswahilini watu wanajengaje? Hua wanachukua hizo tofali 2500 x 300tshs = 750,000 hio ndo hela fundi anatakiwa kulipa fundi yeyote yule hua anajilipa kwa style hio
 
Ukipata fundi mzuri anaweza akakujengea vizuri na hilo tatizo lisiwepo;uzuri wa huo muundo,unatumia mbao na bati chache,na kwa sababu bati zinafunikwa,unaweza tumia haya mabati ya kawaida
Hivi mvua ikinyesha maji hayatuami huko juu kwenye bati? Au kuna kua na mabomba ya kutoa maji pembeni
 
Mkuu unajua uswahilini watu wanajengaje? Hua wanachukua hizo tofali 2500 x 300tshs = 750,000 hio ndo hela fundi anatakiwa kulipa fundi yeyote yule hua anajilipa kwa style hio
Ni kweli kule gharama ni ndogo mkuu,ila ukitaka nyumba nzuri na itakayokushawishi upaite nyumbani na sio bandani tumia mafundi wabobezi watakaokujengea vizuri na uwalipe vizuri pia. Changamoto ya ujenzi ina mambo mengi,mwingine anaweza akakuinulia msingi nyumba ikasimama na ikaonekana nzuri ,mwingine anaweza kujenga ata msingi usionekano na nyumba kuonekana banda. Hivyo hivyo hata katika upauaji...mwingine atakuwekea mteremko wa kawaida usiovutia na kuna wengine wanaweka mteremko mkali wa kuvutia.Nashauri atafute mafundi wabobezi ambao wamejenga kitu kizuri na awalipe vizuri wamfanyie kitu cha maana.
 
Hivi mvua ikinyesha maji hayatuami huko juu kwenye bati? Au kuna kua na mabomba ya kutoa maji pembeni
Huwa wanaweka gata za plastiki (PVC) au za zege (concrete),wengine wanaunganisha bati na tofali ambayo ni makosa;sasa katika kutumia hiyo mifumo wapo wanaofanikisha isivuje na wapo wasiofanikisha na inavuja.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Back
Top Bottom