Fundi Tanesco alipukiwa na umeme

Fundi Tanesco alipukiwa na umeme

Nipo hapa kigamboni eneo la kampuni za mafuta tumesikia mlio mkubwa kama wa bomu karibu na kampuni ya mafuta ya MOIL.
Waliotokea upande huo wanasema kuna fundi wa Tanesco amelipukiwa na umeme na amekuwa mwekundu mwili mzima(sidhani kama bado yupo hai) na pia wanasema kuna pikipiki imeungua vibaya.

Tupeni taarifa kamili mliopo upande huo au jirani

UPDATES:
Fundi ameharibika vibaya hadi mifupa mbalimbali katika mwili wake inaonekana,amekimbizwa Muhimbili.

Wamuwahishe mochwari akapoe, pole fundi..
 
Inalilahi .poleni .wafiwa mungu akupe mema .inaogopesha.na mda huu umeme unashoti kigamboni.kuna taa haziwaki.na zingine zinawaka
 
Innalillah wainna ilayrajiun. Jihadi yake kutufikishia umeme umeondoa maisha yake. Mungu amlipe amali zake. Aaammiiin. Mbele yake nasi ni hukohuko na wenye kumbeza hawajui wataondokaje. Mungu tusemehe pamoja na wajinga wetu
 
Inalilahi .poleni .wafiwa mungu akupe mema .inaogopesha.na mda huu umeme unashoti kigamboni.kuna taa haziwaki.na zingine zinawaka

Mkuu upo sahihi kabisa mimi taa yangu ya chumbani nimenunua haijafika hata mwezi sasa ghafla tangu juzi haiwaki tena. Napata wasiwasi vifaa vingine vitaendelea kuwa hai kwa muda gani.
 
Yaani tanzania watu wanafanya kazi kama hizo hatarishi bila protection zozote wallahi!!Maafa matupu!!
 
lock and tag
Ukifanyakazi kwenye umeme unahakikisha umezima wewe mwenyewe na umeweka lock na note ya jina,kazi unayoifanya wakati huo na kampuni uifanyayo na mwisho kwa hapa kwetu aweko mtu wa kuiangalia hiyo lock isivunjwe
Pole fundi ndio ajali kazini, Mungu amsamehe makosa yake
 
Back
Top Bottom