Fumbo: Huko Ndani Kuna Nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fumbo: Huko Ndani Kuna Nini?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ms Judith, Apr 15, 2012.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  1.
  Wapendwa nijuzeni, huko ndani kuna nini?
  Tangu zama nilidhani, huko ndiko utamuni,
  ni punde nimebaini, si kutamu asilani,
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  2.
  Kiumbe huyu makini, hakomi kurandaranda,
  Amfumapo mwandani, huparamia kitanda,
  Kasiye kama tufani, hutupia mbali mkanda,
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  3.
  Na kazi anayo mwenzi, miguno na mashauzi,
  Ka’ kufumbata konzi, kiumbe utamuenzi,
  kwini ataitwa manzi, kingi ataitwa mwanzi,
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  4.
  mwanzi ukitiwa pake, pumzi huenda mrama,
  yatisha hayo makeke, vigori hupata homa,
  eti imefika mwake, ya nini tena hujuma?
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  5.
  Ikishaingia mwake, ndipo huanza hujuma,
  Mithili ya mrusha teke, kiumbe hurudi nyuma,
  achomoa mwanzi wake, si haki bali dhuluma,
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  6.
  ikiwa ndani kutamu, vipi mwanzi usidumu,
  Upatemaliza hamu, na kiumbe ajikimu,
  faidi hiyo karamu, manzi asijelaumu,
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  7.
  Kama ndani kuchungu, kwa nini asibaki nje?
  Heri kuchapwa virungu, ndani katu usionje,
  Wasikupate machangu, peponi mbuga uchanje,
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  8.
  Kuingia na kutoka, ndo mchezo wa kikubwa!
  Mwapata vipi mizuka, hata kukacha ubwabwa?
  Na mwisho wake mwachoka, hamkomi nyie wakubwa!
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  9.
  Naleta kwenu wazo, siku zote mfurahi,
  Mtaimaliza mizozo, yale mambo ya kuwahi,
  Mtakipata kitulizo, kama wenzenu wa Bahi,
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  10.
  Ukiingia ‘sitoke, ukitoka ‘siingie!
  Yako ashiki ufyeke, na mwandani uringie,
  Vigori wasiteseke,maisha wafurahie!
  Huko ndani kuna nini, wapendwa nijuzeni

  nawatakia tafakari njema ya fumbo hili na weekend njema

  mbarikiwe sana wapendwa,

  Glory to God!
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hahahaah akaaaaa bwana unatafrani za weekend weye!lol
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ms Juddy, mara hii unaanza sema kunani?
   
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  haya bwana ila Jddy wewe mtundu.lol
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante Miss Judith ..uk ndani kuna fumbo
  UKIWEZA TEGUA..
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Ms Judith nakusalim ikiambatana with Love,
  haki katu hujatenda kwa hilo hapo above,
  Ujuvi mie sina natapa elewa kama ni yale ya Love,
  Sote tupate faidi hebu fumbua fumbo above.

  BTW Shairi lako la kweli napenda nijifunze Uandishi,
  Hatua itafuata kuelewa nini malengo ya Mwandishi,
  hapo sasa nasema wana JF watakoma kwa wangu Uandishi,
  hahahaha... Miss Judy hope sija baka sheria za Uandishi.
   
 7. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  I was going to ask the same questio,but i don't think she meant that!
   
 8. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,125
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  hii kali eti mwanzi ukitiwa pake.
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Nahisi anashangaa mbona mme habanduki huko ndani, kunani??

  Umeshawahi sikia msemo wa 'Men are like rats, always searching for a hole'

   
 10. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  haha, its not personal, ni vijimambo tu vya weekend vimenipitia kichwani mpendwa!

  ndo hapo sasa mpendwa!

  kama ni kutamu mbona wanatoka nje punde tu wakishaingia? kama kuchungu, mbona wavutia kasi namna ile? nadhani hima waje wenyewe hapa watutegulie.

  haha, dont take it personal!

  yap mpendwa,

  tusaidie kutegua fumbo basi, please!

  haha, hiyo kwenye bold nimeipenda sana, kama kuna ukweli vile!

  mwacheni Mungu aitwe Mungu!

  mbarikiwe sana wapendwa,

  Glory to God!
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  @Ms Juddy, uzuri wa wanamme wanajua kuna wife matirio, wakishawaweka ndani tu wanarudi kwenye kutafuta new holes.

  That's how their brain works I guess.
   
 12. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Duh

  Huko ndani kunani.., kweli ni vigumu kujua... Huenda kwako ndani.., sio sawa na kwangu.

  Anyway sometimes tunaweza kuona mlango tukazani tunaingia ndani kumbe tunatoka nje, lakini ukweli ni kwamba hata kule kwenye mazuri mabaya pia yapo, ukipata mazuri zaidi ya mabaya ni kushukuru Mungu.., na kama mpo wawili ndani kwenye furaha (raha uwa zaidi) na kwenye shida (shida hupungua kwa sababu inakuwa shared).

  It depends kama umeingia mlango wa ndani au mlango wa choo
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  subalkheir ADii, na love ndilo kusudi,
  nimekusoma kwa bidii, beti zako za stadi,
  fumbo mie sirudii, kusoma usikaidi,
  saizi yako hilo ADii, shamsham ka zawadi

  swali langu li bayana, kiumbe kantatiza,
  ndani na nje ka laana, hasa kukiwapo kiza,
  pumzize zinapobana, hawezi hata puliza,
  saizi yako hilo ADii, shamsham ka zawadi
   
 14. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Sun mimi naamini kila entrance ina mazuri na mabaya.... Pale penye mazuri ina maana kuna alie weka hayo mazingira ya Mazuri kuwepo hadi ikakurahisishia mhusika. Na pale penye mabaya you have an obligation ya kujaribu badilisha na boresha mazingira yawe mazuri.... Hivo naweza sema at the end of the day.... Ndani kuna kila kitu mabaya na mazuri.... Ni jinsi wewe tu mhusika utavoamua, dedicate kuhakikisha mazuri yakukimbilia wewe na sio mabaya tu.
   
 15. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,125
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Hiyo wife material unavyoikazania hebu tupe darasa ndo wapoje hao wasije kuwa waloimbwa na ace hood.
  @mis jud
  ntarud ngoja nkaumize ndonga ila always home sweet home na our homes is where our heart is and always kwa wanaume our heart is somewhere between legs. MWANZI PAHALA PAKE LOH.
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Ukitaka faulu Ms J, tambua love sio kusudi,
  Ukitaka jibu kamili, elewa ngono ndio kusudi,
  ndani nje kama laana, ukute wala sio lake kusudi,
  ila tu zake tamaa, yamfanya onekana na kusudi.

  Kiumbe majibu hana, bure utajikondesha,
  waweza mjua hasa, na bado akakuendesha,
  kama ndani arudi, basi tambua wamkosha,
  kama nje atabaki, huna budi ni kujiondosha.
   
 17. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa ni jukumu la wote wawili kuhakikisha mazuri yanakuwa mengi kuliko mabaya..., lakini mara nyingine kama ni mmoja tu ndio anajaribu hupelekea shughuli kuwa ngumu (au almost impossible), uvumilivu ni muhimu.., sababu huko ndani kuna milima na mabonde sio plain surface. (huko ndani kunani..., :) )

  Kwahio cha muhimu ni wote kujaribu kufanya all you can kufanya shida na matatizo kuvumilika.., na kama mmoja hafanyi wajibu wake, ni wajibu wa mwingine kujaribu kila linalowezekana and hope mwenza atakuwa na busara na kuona umuhimu wa kuishi kwa amani na uzuri.

  After all a problem shared is half a problem na what is the use of FURAHA (Happiness) if it cant be shared
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Wife matirio wanatofautiana kati ya mtu na mtu.
  Ni matarajio ya mtu kwa mkewe.

   
 19. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,125
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Endelea kumwaga vitu kwan naamin kila mtu anataka kizuri hayupo mtu anayetarajia apate mapepe.
   
 20. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hi MS Judith
  vipi ndoa imejibu????????
  Ubarikiwe
   
Loading...