FT: Simba SC 0-0 Mogadishu CC | Kigali Pele Stadium | CECAFA Kagame Cup | 25.7.2026

FT: Simba SC 0-0 Mogadishu CC | Kigali Pele Stadium | CECAFA Kagame Cup | 25.7.2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,226
Reaction score
17,977
Leo Jumamosi Julai 25 ni zamu ya Tanzania ambapo vigogo wawili, Simba SC na Singida BS kutoka Kundi B watakuwa dimbani kwa nyakati tofauti.

Anaanza Singida BS dhidi ya Jamusi FC kutoka Sudan Kusini... kisha saa 1:00 usiku ni Mnyama Simba SC mwenye vifaa vipya dhidi ya Mogadishu City ya Somalia

1784972712826.png
 
View attachment 3636584
Simba itapigwa vibaya sana
 
Mothus Cooper hata Simba kumpa nafasi ya kucheza leo ni heshima kubwa. Inatosha sana kwake arudi tu Botswana. Kiungo wa ushambuliaji muda wote umegeukia golini kwako hapana aisee. Hata kama ni majaribio sio kwa uchezaji ule maana wachezaji wa design yake wapo wengi Tanzania. Aliyemleta aambiwe tu wazi ni mchezaji wa kawaida sana na Simba imeshafika "level" nyingine kabisa.

Ni mtizamo tu
 
Doumbia naogopa kusema kitu juu yake mpaka nimuone akiwa amepewa dakika 60+ na dakika zote hizo akiwa na mafundi wa Simba pale mbele.

Kelvin Nashon ameonyesha ana uwezo mkubwa hasa ikizingatiwa hakuanza na mafundi.

Ila yule mwamba sijui wa kuitwa Keletso jamaa yupo vizuri. Pale Simba wamesajili.

Ni mtizamo tu.
 
Full Time (FT) Simba 0 Mogadishu City 0!

Mechi iliyotangulia:
Singida Black Stars 0 Jamuzi kutoka Sudan Kusini 2!!

Kwenye hili naipongeza timu yangu ya Yanga kwa kuyapotezea haya mashindano.
 
Back
Top Bottom