Full Text: Hotuba ya Prof. Kahigi iliyozua mjadala bungeni hadi bunge kuahirishwa...

lengo kuu la kutaja taja majina ya watu hapa ni kutaka kupotosha ukweli wa video ya lwakatare akipanga ugaidi...watanzania wa leo si wa kudanganywa


Nahisi wewe ni mmoja wa hawa hapa chini!!!

Mheshimiwa Spika, ushahidi wenyewe ni kwamba baada ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA kutuhumiwa kwamba anahusika na ugaidi na video yake kurushwa kwenye mitandao ya kijamii, Muhidin Issa Michuzi, ambaye ni mpiga picha wa Rais, Ikulu, aliandika barua-pepe kwa Salvator Rweyemamu, Prosper Mbena, Hamis Mwinyimvua, Liberatus Mulamula, Msafiri Marwa, Laurent Ndumbaro na wengine ambao ni watumishi wenzake wa Ofisi Binafsi ya Rais akiwapongeza kwa kazi nzuri na ya ziada waliyoifanya ya kutengeneza video ya Lwakatare, na kuwaeleza kuwa hiyo ni kete kubwa kwao hivyo lazima waipigie kelele sana.
 
Katika kikao cha bunge leo jioni zilikuwa zikisikika sauti za chini kwa chini za wabunge wa CDM wakimpa maelekezo mh.prof Kahigi jinsi ya kutoa hoja.Je ni kweli Mh.Prof hajui namna ya kutumia kanuni za Bunge?
 
Kanuni za Bunge bado zinawapa watu wengi ugumu namna ya kutumia(hasa wabunge wapya) ila icho c kipimo cha uwezo wa uelewa wa mtu katika kujenga na kupambanua hoja Bungeni.kubwa ni kujua hoja ya muhusika inatija kwa Taifa?kuliko mtu akajua kanuni zote kisha akawa anaongea pumba tu.
 
Nothing personal, I doubt his level of education, huwezi kuwa professor halafu umekaa kama goigoi! hata kusoma tu hotuba ya upinzani ilikuwa ikimpa shida sana, halikuwa anakwama kwama na vigugumizi kibao.

Rai yangu kwa CHADEMA, wawape watu wenye huwezo wa kuwika, wampe jogoo ZITTO hawe anawika hapo bungeni! Hoja zao zitakuwa na uzito kutokana na msomaji anavyokubalika.
 
Acheni ushabiki ile hotuba ilikua imebadilishwa mda ule kutokana na Kiti kutaka baadhi ya vitu viondolewe mfno ishu ya Lwakatare na UWT,kwaiyo ni waz kama kitu kimebadilishwa ghafla na unatakiwa soma mbele za watu ni dhaili kukoseakosea kutakuwepo bana.
 
Nothing personal, I doubt his level of education, huwezi kuwa professor halafu umekaa kama goigoi! hata kusoma tu hotuba ya upinzani ilikuwa ikimpa shida sana, halikuwa anakwama kwama na vigugumizi kibao.

Rai yangu kwa CHADEMA, wawape watu wenye huwezo wa kuwika, wampe jogoo ZITTO hawe anawika hapo bungeni! Hoja zao zitakuwa na uzito kutokana na msomaji anavyokubalika.

Mtampigia sana promo Ighondi ZZK lakini hawezi kuepuka ushiriki wake kwenye ng'oa meno movement.
 
mi huyu profesa kwa kweli ameniacha hoi hata hotuba imemtoa nishai kusoma,tena kiswahili!
chadema hii kasoro next time ifanyieni kazi,tumieni watu makini
 
Nadhani Prof anakigugumizi sasa
kumbukeni watu wenye kigugumizi wana hasira
wanapokosolewa,hasa pale alipoambiwa
kuna kurasa zibadilishwe.

Ikawa kama ana Misimisi
Yaani petron iliyochanganyika na maji.

Yuko sawa.
 
Hivi na mh. MULUGO naye ana kigugumizi au ndo haijui nchi yake au hajui kusoma kabisa kwasababu kutoka Zanzibar mpaka Zimbabwe mbona aliteleza sana.
 
Kilichonisukuma kuweka CV hii ya professor Kahigi, ni post moja hapa kwenye forum iliyokuwa inamdhihaki msomi huyu wa namna yake, hili jambo limenikera sana. Unajua kuwasikiliza waropokaji kama Mwigulu na Lusinde tumejikuta tunasahau kwamba si hulka ya wasomi kuropoka ili waonekane wanajua sana kama wanavyofanya wakina Mwigulu. Ujumbe wangu kwa watanzania wenzangu ni tusiruhusu akili ndogo kutawala akiri kubwa, itatufikisha pabaya.

[h=2]Member of Parliament CV[/h]


GENERAL
Salutation
Honourable
Member picture
1659.jpg

First Name:
Prof. Kulikoyela
Middle Name:
Kanalwanda
Last Name:
Kahigi
Member Type:
Constituency Member
Constituent:
Bukombe
Political Party:
CHADEMA
Office Location:
-
Office Phone:
+255 767 340172
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
kkahigi@parliament.go.tz
Member Status:
Current Member
Date of Birth
4 August 1950
EDUCATION
School Name/Location
Course/Degree/Award
Start Date
End Date
Level
Michigan State University-USA
PhD
1982
1988
PHD
University of Dar es Salaam
M.A (Linguistic)
1976
1977
MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam
B.A (Education)
1973
1976
GRADUATE
Mkwawa Secondary School
A-Level Education
1971
1972
HIGH SCHOOL
Kahororo Secondary School
O-Level Education
1967
1970
SECONDARY
Rubondo Primary School
Primary Education
1963
1966
PRIMARY
Iyengamuliro Primary School
Primary Education
1959
1962
PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name
Position
From
To
The Parliamnet of Tanzania
Member-Bukombe Constituency
2010
2015
Kalamazoo College, USA
Lecturer
1987
Michigan State University
Tutor
1980
1982
University of Dar es Salaam
Lecturer
1976
2010
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location
Position
From
To
Chama Cha Mapinduzi
Member of Political Committee(Abiyani University)
2007
2010
TANU/University
Chief Editor
1975
1976
PUBLICATIONS
Description
Date
Prof. K.Kahigi: Structural and Cohesion, Dimensions of Style, RECALL,University of Gent,Belgium.
1998
Prof.K.Kahigi: Misingi ya Kusoma,CBP Tanzania.
2003
Prof.K.Kahigi: Kunga za Ushairi,TPH Dar es Salaam, Tanzania.
1982
Prof. K. Kahigi: Sumbwa-English-Swahili Dictionary, LOT Project,University of Dar es Salaam Tanzania.
2008
Prof. K.Kahigi: Structural and Cohesion, Dimensions of Style, RECALL,University of Gent,Belgium.
1998
Prof.K.Kahigi: Misingi ya Kusoma,CBP Tanzania.
2003
Prof.K.Kahigi: Kunga za Ushairi,TPH Dar es Salaam, Tanzania.
1982
Prof. K. Kahigi: Sumbwa-English-Swahili Dictionary, LOT Project,University of Dar es Salaam Tanzania.
2008
Prof. K.Kahigi: Structural and Cohesion, Dimensions of Style, RECALL,University of Gent,Belgium.
1998
Prof.K.Kahigi: Misingi ya Kusoma,CBP Tanzania.
2003
Prof.K.Kahigi: Kunga za Ushairi,TPH Dar es Salaam, Tanzania.
1982
Prof. K. Kahigi: Sumbwa-English-Swahili Dictionary, LOT Project,University of Dar es Salaam Tanzania.
2008
Prof. K.Kahigi: Structural and Cohesion, Dimensions of Style, RECALL,University of Gent,Belgium.
1998
Prof.K.Kahigi: Misingi ya Kusoma,CBP Tanzania.
2003
Prof.K.Kahigi: Kunga za Ushairi,TPH Dar es Salaam, Tanzania.
1982
Prof. K. Kahigi: Sumbwa-English-Swahili Dictionary, LOT Project,University of Dar es Salaam Tanzania.
2008
 
hili ni lile tamko la Marando, haina haja ya kusomwa tena bungeni
WEWE NA RAFIKI YAKO "ATONGWELE" Join Date : 22nd February 2013 Posts : 902 Rep Power : 488 Likes Received: 71 Likes Given:INABIDI MPEWE TUZO YA KUJAZA SEVA KWA UCHAFU.7
 
Bunge lawanusuru mashushushu - Siasa - mwananchi.co.tz

Bunge limefikia uamuzi huo juzi kwa kupiga kura za sauti, kupinga hoja ya Msemaji wa Kambi wa Upinzani katika Ofisi ya Rais (Utumishi), Profesa Kulikoyela Kahigi.


Profesa Kahigi alitaka Bunge liitake Serikali kuchunguza tuhuma hizo na kuwachukulia hatua watuhumiwa hao, suala ambalo liliibua mvutano baina ya Kambi ya CCM na Serikali kwa upande mmoja na upinzani kwa upande mwingine.

Mvutano huo ulitokea juzi wakati Bunge limekaa kama kamati kupitisha kifungu cha mshahara wa Waziri.

Profesa Kahigi alisema kambi yake imetoa tuhuma dhidi ya maofisa usalama wa taifa, kuwatesa watu na kutumika kupanga njama, lakini Serikali imekaa kimya bila kuchukua hatua dhidi ya tuhuma hizo.

“Ninachoomba ni kitu kidogo tu, hoja yangu hapa ni kwa nini Bunge na Serikali havichukui hatua, ninatoa shilingi mpaka mtakapoeleza ni hatua gani mtazichukua dhidi ya tuhuma hizi,” alisema Profesa Kahigi.

Suala hilo lilizua mjadala na kusababisha Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kusema Bunge siyo sehemu ya mashtaka na kwamba, kama kambi hiyo inazijua tuhuma hizo izipeleke polisi huko ndiyo hatua zitachukuliwa.

“Nendeni polisi mpatiwe RB (Kumbukumbu ya taarifa polisi) halafu tuhuma zitafuatiliwa. Hatuwezi kwenda kuwashughulikia hao watu mnaowasema,” alisema.

Chikawe.

Awali, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema tuhuma hizo kisheria zinatakiwa zipelekwe polisi siyo bungeni.

“Hatuwezi tukashughulikia tuhuma kwa kuwa tu mmesema kwamba tuzichukulie hatua,.Naomba wanasheria wenzangu tufuate sheria kwa kuwa tunazijua,” alisema Simbachawene.

Hata hivyo, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) alipinga hilo na kwamba, kazi ya Serikali ni kuchukua hatua dhidi ya tuhuma zinazotolewa bungeni na mahali pengine siyo kuzungukazunguka.

“Zungukazunguka hii inamaanisha Serikali inajua mpango mzima. Nyie wapelekeni mahakamani tutawapa ushahidi, fanyeni hivyo siye tuwape mambo,” alisema Mdee.

Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi) naye alitaka Serikali kushughulikia tuhuma hizo kwa sababu sheria inawaruhusu kufanya hivyo.

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alilihoji Bunge kama linakubali hoja iliyotolewa na mbunge huyo wa Bukombe, sauti za hapana kwa maoni ya Spika zilishinda, hivyo hoja hiyo itatupiliwa mbali.
 
Wana JF naomba video tamkwa ya Lwakatare hivi inapatikana wapi vile, nataka kuisikiliza na mie
 
Back
Top Bottom