Führeprinzip policy and Hitler regime

Führeprinzip policy and Hitler regime

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
362
Reaction score
909
KUPITIA SERA YA "FÜHRERPRINZIP" NCHINI UJERUMANI HATIMAE ADOLF HITLER ALIKUWA UJERUMANI NA UJERUMANI IKAWA HITLER.

Na Comred Mbwana Allyamtu
Sunday -23/9/2018

Sera hii ya "Führerprinzip" neno linalotokana na lugha ya kijerumani likimanisha "Hiltler ni chaguo la Mungu na wajerumani Mungu kawaletea chaguo kwa ukombozi wao", sera hii ilipata nguvu nchini Ujerumani kufatia madhira ya baada ya vita ya kwanza ya dunia, hivyo kufatia mateso ya Ujerumani kushindwa vita vya kwanza vya dunia iliwafanya wajerumani kujiona wapweke maana dunia iliwanyanyasa kwa kutozwa fain na kunyagwanywa maeneo yake ya utawala. Kupitia haya yote na kuibuka kwa Hitler waliona kuwa "Hitler ni ujerumani na Ujerumani ni Hilter", hii ikawa ndio msingi wa kila kitu nchi Ujerumani (Führerprinzip).

Baada ya Adolf Alös Hitler kuchaguliwa kama chancellor na Raisi Paul von Hindenburg mwezi January 30, 1933, baada ya ushindi kwenye uchaguzi mapema mwaka huo ambapo chama cha Nazi kiliibuka kidedea Adolf Hitler akaanza kuweka misingi ya dola la Ki-Nazi.

Wafuasi wa Hitler wakachoma bunge (Reichstag) hii ilikuwa mbinu ya kisayansi ya siasa ili Hitler aweze kuzibiti dola, tukio la uchomaji wa moto bunge ulitafsiliwa kuwa wapinzani wa serikali yake kuhusika tukio hili lilitokea mwezi February 28, 1933, kufuatia hali hiyo chama cha Nazi kikaanza kupoka haki za kijamii kwa wananchi, ikatolewa amri ya hakuna kuandamana na hakuna mikutano ya siasa hii ilitokana na hali ya hatari kufuatia bunge kuchomwa moto.

Haki hizo zilizopigwa marufuku ambazo Hitler alizizuia zilikuwapo kwenye katiba ya Ujerumani iliyoitwa "Weimar",watu walikuwa kimya hakuna aliyesema, hata viongozi wa dini walikaa kimya kama vile hawaoni kinachoendelea.Kuanzia hapo nchi ikawa ya kipolice makada wa chama cha Nazi walioitwa ‘’SS’’ na walinzi wa Dola la Ki-Nazi wakawa na mamlaka zaidi ya police wa taifa hata wakawa wanakamata kamata hovyo, kanisa halikuseama kitu lilikaa kimya misiri ya moto ulioshika kwenye jangwa la barafu.

Hitler na dola lake walitekeleza mateso ya kutisha kwa wale viongozi wa vyama vya upinzani kwa kuteswa, kuuwawa kikatili na wengine kufungwa na kapotelea huko mfano tu ni chama cha ki-Communist na Social Democratic Party ambapo viongozi wao waliuwawa na wengine kapotelea kusiko julikana bila kusahau Wafanya biashara wa Israeli waliishi maisha ya hofu na kufunguliwa mashitaka na kutiwa vizuizini na kubaguliwa, hakuna aliyepona lakini ajabu hakuna aliyekemea kwani wengi waliona kuwa mateso hayo yalikuwa kwa walikuwa waislaeli tu.

Miaka miwili ya mwanzo ya uchancellor wa Hitler alianza kuzima makali ya vyama vya siasa na kwa kutumia sera yake mpya ya kushirikisha vyama kwenye serikali ya (Gleichschaltung) kwa shabaha ya kuvimaliza nguvu vyama vya upinzani huku wale waliokataa walinyakuliwa na kufichwa wasionekane tena mpaka leo.

Serikali ya KiNazi ikaanza kuwaondoa makazini watu wenye asili ya Kihayudi waliondolewa kwenye biashara ,Serkali ya Kinazi ikapiga marukufuku vyama vya wafanyakazi, hakuna aliyesema neno hapo serikali ilivipiga marufuku vyama vya wafanyakazi kwa kisingizio kuwa walikuwa wana shilikiana na vyama vya upinzani kudidimiza taifa. Pia hakuna aliyesema neno kwani waliona kuwa wanaoshughulikiwa ni vyama vya wafanyakazi.

Baada ya bunge kuwa butu na kukaliwa na spika kibaraka aliyefuata maelekezo ya Hitler hatimae mwezi March 23, 1933 ilipitishwa sheria mpya ya Bunge la ujerumani (Reichstag) ambapo sheria hiyo ilikaimisha shughuli zake zote za kibunge kwenye baraza la mawaziri la Hitler. Katikati ya mwezi July, Chama cha Nazi kikawa chama pekee Ujerumani chenye nguvu na kilicho ruhusiwa kitaifa. Hatimae katiba ya taifa la Ujerumani ikawekwa pembeni na ikawa mwendo wa matamko tu kwenda mbele (Chonselor decree), Hapo spika wa nchi akashituka na kuipigia kelele serikali ya Hitler ikamdaka kisha alipotea hadi leo.

Kuanzia hapo ikawa sifa zote ikawa ni kwa Adolf Hitler akiitwa kiongozi wetu mpendwa (Führer) huku wafuasi wa chama cha Nazi walipaza sauti zao na kusema "wewe Hiltler ni zawadi ambayo Mungu ametupa, Hiltler ni ujerumani na Ujerumani ni Hilter", hii ikawa ndio msingi wa kila kitu nchi Ujerumani (Führerprinzip) Hitler akawa ndiyo mwongozo wa kila kitu nchini Ujerumani, picha zake zikawekwa kila kibra za ibada zao, na kauli mbiu yao ya Führerprinzip ikawa ndio mwongozo kwenye familia, uchumi, chama na serikali ya Ujerumani.

Kumbuka wakati wote huo wazee wa ujerumani walikaa kimya ni pamoja na raisi wa nchi hiyo ndugu Hindenburg, baada ya kifo cha Hindenburg August 1934, Hitler akajiongezea mamlaka na akapoka madaraka yote ya taifa hilo ikiwa ni pamoja na kufuta madalaka ya uraisi na akawa kiongozi mkuu na chancellor mwenye mamlaka makubwa nchini Ujerumani. Majenerali wa jeshi la Ujerumani walitakiwa waape kiapo cha uaminifu na utii mbele yake.

Wakati taifa linashituka tayali nchi yao inaingia kwenye vita vya pili vya dunia, vita ambavyo wajerumani huvikumbuka mpaka leo ikiwa ni vita iliyo waacha na maumivu makubwa ya Ujerumani kutengana na kuzaliwa mataifa mawili. Nje ya maafa na mdororo wa uchumi bado vidonda vya Hitler vingali vikiishi mioyoni mwa Ujerumani hadi sasa.

Je huyu Adolf Hitler ni nani mpaka awafanye wajerumani kushindwa kumzuia toka mwanzo? Mpaka kuibuka na kufanya Ujerumani kudidimia kwenye mikono ya udikiteta?

ADOLF HITLER NI NANI?

Adolf Alois Hitler alizaliwa nchini Austria mwaka 1889, akaingia shule ya sekondari mwaka 1900 lakini hakufaulu,hivyo alishindwa kuendelea na masomo. Lakini alijaribu tena kurejea shuleni, zamu hii katika shule ya uchoraji iliyojuilikana kama Akademia ya Usanii ya Vienna akafeli tena.

Baada ya kifo cha wazazi wake alikosa msaada wa familia akakaa kwa muda katika nyumba kwa ajili ya watu wasio na makazi.Tangu alipohama nyumbani aliacha kufuata dini ya mama yake,Klara, akachukia moja kwa moja Kanisa Katoliki kwa kuliona halipendelei Wajerumani. Mwaka 1913 alihamia Munich katika jimbo la Bavaria (Ujerumani). Mnamo Agosti 1914,wakati wa mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia,alijitolea kwa jeshi la Bavaria ambapo kutokana na bidii na ukakamavu wake alipanda cheo na kuwa praiveti. Hatimae Mwisho wa vita mwaka 1918 alipanda nakuwa na cheo cha koplo.

Baada ya vita kuisha Hitler alikosa kazi lakini aligundua kipawa chake cha kuhutubia watu,akajiunga na siasa na kuingia katika chama kidogo cha Nazi (NSDAP) alikopanda ngazi haraka kutokana na uwezo mkubwa wa kuongea. Adolf Hitler alivutiwa sana na Benito Mussolini, kiongozi wa kifashisti wa Italia,aliyefaulu kuingia madarakani mwaka 1922 kwa kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya wafuasi wake waliofanya maadamano makubwa ya kuelekea Roma.

Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya Bavaria kama mwanzo wa utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin, lakini alishindwa na alikamatwa na kuhukumiwa kwa kosa la uasi na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano, ingawa alitumikia miezi tisa tu. Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf" ("Mapambano Yangu") alikojaribu kueleza imani na siasa zake.Humo alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi yake ya ubaguzi wa kiyahudi na namna walivyo changia Ujerumani kushindwa vita ya kwanza ya dunia.

Baada ya kutoka gerezani alirudia kwanye siasa. Alijitahidi kujihusisha na siasa na kuanza kushika ngazi za utawala wa chama cha (NSDAP) akagombea uongozi na akakubaliwa kuwa kiongozi mkuu wa chama. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili vilivyovaa sare vikifanya mazoezi kama wanamgambo na kuwa tayari kupigana na maadui wa kisiasa wakati wa maandamano. Kikundi cha cha kwanza ni kikundi cha SA ("Sturmabteilung" "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi sana kikawavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia. Kikosi cha pili kilikuwa na watu wachache kilichoitwa "SS" ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi.

Chama chake kikaimalika sana na kikufaulu hadi 1929,wakati ambapo uchumi wa dunia pamoja na wa Ujerumani ulipoporomoka vibaya.Mamilioni waliachishwa kazi na kuona njaa.Katika hali hiyo watu walianza kupigia kura vyama vyenye itikadi kali. Hapa sasa ndio tunaanza kupata jibu ni kwanini Hitler aliungwa mkono na kushinda na hatimae kuonwa kama mkombozi wa wajerumani.

Katika uchaguzi wa mwaka 1930 kura za NSDAP ziliongezeka kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na dhaifu, kufuatia hali hiyo hatimae Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% na kuwa chama chenye kura nyingi zaidi nchini na chama kikubwa katika bunge la Reichstag. Katika hali hiyo viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza Hitler katika serikali mwaka 1933, Kufatia hali hiyo kizaza kikaanza.

Hatimae Tarehe 30 Januari 1933 Hitler akawa Chansela wa Ujerumani. Ujerumani ikapatwa na mara moja alichukua nafasi kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza madarakani wakaanza kupata cha mtamakuni.

Kufatia utawala wake Ujerumani ikapita mengi sana ambayo nimeyaeleza huko juu, na hatimae Ujerumani kuingia kwenye vita vya pili vya dunia. Yapo mengi sana ya kueleza katika utawala wake ikiwa ni pamoja na kuanzisha uvamizi kwenye mataifa jirani jambo lilopelekea kuibuka vita kubwa sana ya dunia.

Pamoja na utawala wa kidikteta (dictatorial) yapo mazuri yake anayotajwa kuifanyia Ujerumani ikiwa ni pamoja na maendeleo makubwa kwenye technolojia ya jeshi kwa kuvumbuliwa tank za mafuta, siraha nzito, ndege za kivita, na makombora ya masafa marefu, pia kwenye kada ya afya yapo mengi sana yaliyofanyika huku miundombinu ya taifa lake ikiimarika sana pamoja na kumaliza tatizo la ajira nchini mwake.

Kufatia dunia nzima kutikiswa na utawala wa Adolf Hitler hatimae dunia ikapatwa na vita ya Pili ya dunia iliyopelekea kutamatishwa kwa utawala wa Hitler na kuwa mwisho wa utawala wa kidikteta wa enzi wa Berlin kutamatishwa, mwisho wa vita ya Pili ya dunia ndio ulikuwa mwisho wa Adolf Hitler na kuibuka utata juu ya kifo chake.

JE ADOLF HITLER ALIKUFA VIP?.

Kiongozi mkuu wa Urusi Josef Stalin mapema miaka ya 1948 aliomba ushahidi juu ya kifo cha Hitler, alisikika akisema "Isingekuwa rahisi kumuuwa Hitler wala Hitler kujiuwa huyu yu'hai". Taarifa za ushahidi wa Hitler na mkewe Eve kuwa hai zilianza kupenya.

Habari za kushtusha zilisambaa kwamba dakika za mwisho wa mapigano Hitler na mkewe walitoroshwa kwenda kwenye pori zito huko Argentina. Mnamo tarehe 29 April 1945 kupitia tundu refu la siri lililokuwemo ndani ya handaki tukufu lilitumika kumpenyeza Hitler hadi baharini, ambapo U-boat no 502 (underground boat nambari 501) lilikua likiwasubiri kuwasafirisha bahari hadi Argentina ambako walipokelewa na mgeni wao raisi Juan Peron (Raisi wa Argentina) pamoja na mkewe Evita. Ikumbukwe serikali ya Hitler ilidhamini uchaguzi uliomuweka madarakani Juan kuwa kiongozi wa mabavu wa Argentina.

Hitler, mkewe na binti yao waliishi maisha ya kifahari sana kwenye miji mbalimbali nchini Argentina hadi mwaka 1955, ambapo Eva na bintiye Ursula walimwacha Hitler na kuelekea Neuquen. Hitler alifariki kifo cha kawaida sana mwaka 1962.

USHAHIDI JUU YA KIFO CHA HITLER

Mwaka 2010 kikosi cha Marekani cha kiinteligensia cha CIA kilitoa taarifa za siri ya juu (declassified information), andiko lenye kurasa 792 zikieleza uhalisia juu ya nadharia ya kifo cha Hitler na kubainisha kua kikosi maalumu cha Marekani kilisaini kumtorosha kwa siri Fuhrer Hitler mafichoni. Hakuna uthibitisho wowote wa mwili wa Hitler sehemu yoyote duniani baada ya vita ya Pili ya dunia.

Marshall Zhukov, kiongozi wa jeshi la Urusi alizungumza na waandishi wa habari na alinukuliwa akisema "We never identified the body of Hitler, I can say nothing about about his fate. He could have flown away from Germany at the last moment" "Hatukufanikiwa kuutambua mwili wa Hitler, siwezi kuzungumza chochote kuhusu mauti yake. Yawezekana alitoroka dakika za mwisho kabisa".

Simulizi ilibadilika mwaka 1968, Warusi walipoamua kufukua kilichoaminika kuwa ni mabaki ya mwili wa Hitler yaliyochomwa moto. Walifanikiwa kupata fuvu lenye tundu la risasi, taya na meno ya Hitler. kwa muda mrefu serikali ya Urusi haikutaka kupeleleza mabaki hayo, hadi ilipofika 2009 ambapo serikali iliridhia uchunguzi ufanyike.

Jopo la wataalamu wa mifupa, vinasaba na akiolojia likiongozwa na Bellanton walifanya uchunguzi wa mabaki hayo. Matokeo yaliuduwaza na kuustaajabisha ulimwengu. Hapakuwa na sampuli yoyote iliyoendana na DNA ya Hitler, fuvu lile liligundulika kua lilikua la mwanamke mrembo sana mwenye umri wa miaka 39-40. (Wala hakuwa Eva, mke wa Hitler).

Je Fuvu lilitokea wapi? Lilikuwa na nani? Kwanini Warusi walilihusisha na Hitler? Vyovyote vile, vipimo na majibu ya uchunguzi viliuwa porojo zote kuhusu kujiuwa kwa Hitler. Njia ya Panya ya Wanazi. Viongozi wengi wa juu Nazi walioshiriki katika utawala wa damu wa Ujerumani walitoroka mafichoni baada ya WW2, kwa msaada wa mitandao ya siri ikiwemo Odessa (wa Ukraine), kanisa katoliki pamoja na Taasisi ya siri ya Marekani. Wamwaga damu mashuhuri kama Josef Mongele na Adolf Eichman walikimbilia katika nchi za kidikteka kama Chile na Argentina.

Mnamo mwaka 2014 Simon Dunstan na Gerrard Williams waliandika kitabu kiitwacho Grey wolf: The escape of Adolf Hitler (Mbwa mwitu wa kijivu: Kutoroka kwa Adolf Hitler). Kitabu hiki kilibainisha kwa undani kuhusu kutoroka kwa Adolf Hitler na nadharia ya uwongo juu ya kifo cha Hitler. Kitabu hiki kilijumuisha wakazi wa Argentina waliotoa ushahidi wa kumuona Hitler akikatiza mitaa ya Argentina.

Maneno ya mwisho yaliyosikika kutoka kwa Hitler akiwa ndani ya Handaki, alisema " Naamini leo kwamba mwenendo wangu ni kwa mujibu wa mapenzi ya Muumba Mwenyezi Mungu"... Na ndio ulikuwa mwisho wa Adolf Hitler kusikika tena Duniani...


Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
FB_IMG_1557213449900.jpeg
FB_IMG_1557213453958.jpeg
FB_IMG_1557213458651.jpeg
FB_IMG_1557213469890.jpeg
 
Uzi mzuri sana mkuu na unafikirisha sana lakini utashangaa mambo ya kipuuzi yakipata likes nyingi zaidi!!..
 
Back
Top Bottom